Rushwa anayoiona Sumaye: Takukuru mpo wapi?

Great thinkers, nimeshawishika kuandika maono yangu ili kupata mawazo yenu wadau.
RUSHWA adui wa haki, ni maneno ya Mwalimu na kila mwenye utashi. siku za karibuni viongozi wengi hasa wa CCM waliopo na walioondoka madarakani wanalalamikia rushwa ilivyokithiri ndani ya CCM, Kikwete, Nape, Sitta, Mukama, Sumaye. hao ni watu wazito katika chama ambao tulitegemea kama ingekuwa RUSHWA inawakera wangechukua hatua haraka sana. Lakini kwa maneneo hayo inaonyesha RUSHWA ni sehemu ya CCM. Kiongozi mmoja alisema sera ya kuvuana magamba sio ya chama ni ya Nape tu. maana yake kwenye CCM ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na RUSHWA ni sehemu ya chama.

Hoja yangu ni kwamba, Je, CCM wana dhamira ya dhati kweli ya kupigana na UFISADI na RUSHWA wakati wenyewe ni waumini wa RUSHWA???? na je wataikomboa nchi hii kwenye majanga ya RUSHWA na UFISADI wakati wenyewe ni waumini wa hayo????? kama wanatoa RUSHWA kuingia kwenye NEC, je kupata URAISI au UBUNGE si itakuwa balaa? na hizo pesa zao watazirudisha vipi???? kama sio rasilimali zetu hizi hizi??

nafikiri dawa ni waache watumie rushwa yao weeee kwenye uchaguzi wapigwe chini kwa aibu tuone jinsi watakavyorudisha hela zao.

Nawasilisha mtazamo wangu
 
Nimemsikiliza kwa makini Mh. Waziri Mkuu Mstaafu kwa heshima (si kwa kashfa ya kutuibia wananchi), Mh. Fredrick Sumaye akieleza kwamba rushwa ndani ya chaguzi za CCM si tatizo jipya ispokuwa la sasa limekuwa la aina yake kidogo kwani ni rushwa ya "Kimtandao" ambapo mtu anaweza akawa sehemu nyingine lakini aka-influence uchaguzi wa watu anaowataka toka sehemu nyingine ya nchi so long kwamba watakaochaguliwa atakuja kuwatumia huko mbeleni.Swali ninalojiuliza, kama hivi vitu vipo dhahiri kihivi mpaka akina Sumaye wanavizungumza hadharani na hatujasikia mtu yeyote amekamatwa na rushwa na kuhukumiwa kwenye chaguzi za CCM, je kweli kuna haja gani ya kuwa na chombo kama Takukuru ambacho kinaendeshwa kwa kodi zetu?Naomba kuwasilisha.
Huyu naye haaminiki hivi angeshinda unec alioutaka angeyaongea haya? Wanasiasa wengi si hasa
 
Habari wana jf,

Kwa yeyote ambaye amekuwa akifuatilia siasa za hapa kwetu anafahamu kuwa CCM inaendesha chaguzi zake za ndani, kinachonisukuma kuleta mada hii ni haya:
1. chama hiki kimekuwa kikijinadi kwa muda mrefu kwamba ni chama makini, kinachokubalika na kupendwa na wanachi, japo kwangu hii ni IRONY, na kwa mantik hiyo, kimekuwa kikijinadi kwamba kipo imara siku zote, hadi viongozi wa chama hiki bila aibu wamejitokeza hadharani kuwa anayesema kinakufa atakufa yeye, kwangu mimi kauili hii ni ya mfa maji na mtu asiye taka kuupokea ukweli na asijejua historia, kwa maana jinsi chama kilivyokuwa kikipendwa na jinsi vyama vingine hasa barani Africa vilivyokuwa na sifa kama ya hiki chama jinsi vilivyopotea.

2.Mbaya zaidi chama ambacho viongozi wake hawaoni wala kusikia, kwani chaguzi zinazofanyika sasa ni aibu tupu kwa hiki chama, na inanisikitisha eti kiongozi anakwenda kufunga mkutano wa jumuia ambayo uchaguzi wake ulitawaliwa na rushwa, kejeli na matusi bila hata tamko moja ambalo litaonyesha kukerwa na jambo hilo,
Kwa mfano, tumesikia na kuona umoja wa wanawake wa ccm tz, tena nafikiri waache kujiita UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA, walivyoendesha uchaguzi wao, ni aibu, rushwa, matusi na mipasho, je hawa bado wanaendelea kuwa na ndoto za kuendelea kutawala nchi hii kirahisi rahisi, kwangu mimi ni kutudharau watanzania, chama kinakuwa kama watu wanaong'anga'nia mali za urithi, shame!

3. Chaguzi hizi, zinaonyesha jinsi watu hawa wanavyotumia pesa kupata uhalali wa kutawala wala si kuongoza kuanzia ngazi zote, kama ndani ya chama Rushwa ni utamaduni, vipi chaguzi za nje, hivyo haya yanatuthibitishia jinsi wanvyoiba kura, wanakanyaga sheria za uchaguzi na kutoa rushwa.

4. Hizo pesa wanazonunua kura wanazitoa wapi?, kwa mfano tumekuwa tukisikia kwenye hizi chaguzi za ndani kuwa wanatoa hadi laki 5, kwa mtu, wanatoa wapi kama si fedha zetu walima mihogo?

5. Chama hiki tawala kimeonyesha wazi kuwa hakina nia ya dhati hata kidoogo ya kupambana na rushwa ndani ya nchi hii, na pia TAKUKURU ni agent mwingine wa kuendeleza rushwa na kuhalalisha posho za watu kwa kisingizio cha kupambana na rushwa. Haiwezekani taarifa zote ambazo ziimekuwa zikiripotiwa juu ya rushwa kwenye chaguzi hizi isiweze kumkamata hata mtuhumiwa mmoja.

6. Huu ni wakati wa msajili wa vyama vya siasa nchini kujitafakari mchango wake katika kuendeleza uozo ndani ya nchi hii, kwa mfano amepata kujitokeza kwamba chama kitakachoonekana kuleta vurugu atakifuta (kama anamadaraka hayo) aseme basi hata kwa vyama vinavyoendeshwa kwa rushwa vifutwe kwani havina tija kwa watanzania vinginevyo yeye tutaaendelea kumuOna ni agent wa CCM tu.

MWISHO:
ccm itakufa tu, hata kama sio leo kesho, kwani dhamiri ya mpiga kula wa leo asiyetumika, mwenye uchungu na nchi hii, asiye na ajira wakati vilaza watoto wa vigogo wanakazi za juu, mwenye uchungu na elimu yetu, mwenye uchungu na kodi zetu mwenye uchungu na ardhi yetu, madini yetu, mwenye kukerwa na mabilion yanayotoroshewa uswis hata waacha mpite 2015 kwani itakuwa ni vita ya uovu na usafi na kamwe giza halizidi nuru!
 
Back
Top Bottom