Rungwe tuna wabunge bubu!

Wazo zuri sana, lakini wabunge wa kuhamashisha new ideas hatuna.

Nachokiona msiwalaumu wabunge tu, hata ninyi wananchi mnawaweza kuanza kwa kuandika wazolenu na kuliwasilisha kwa waziri husika, huwa napatwa simamanzi kununu mkungu wa ndu chini ya Tsh 5000 wakati Mkungu huohuo ukiuku Dar bei yake ni above 20K
 
Nachokiona msiwalaumu wabunge tu, hata ninyi wananchi mnawaweza kuanza kwa kuandika wazolenu na kuliwasilisha kwa waziri husika, huwa napatwa simamanzi kununu mkungu wa ndu chini ya Tsh 5000 wakati Mkungu huohuo ukiuku Dar bei yake ni above 20K
Unachosema ni kweli akini inaelekea hujafika Rungwe.
Miundombinu ya barabara ni balaa!
Watu wanamkumbuka Mwalimu Nyerere kwa barabara moja tu kueekea Malawi.

Hakuna kabisa al weather roads kuekekea kule waliko wananchi.
Sehemu kama Mwakaleli, Itete, Masebe, Ikuti, Mpuguso-Lutengano, Masoko-Mbambo, sehemu zote hizi hazijui barabara za lami.

Bila uwekezaji wa miundombinu ungehimizwa na wabunge wetu hawa, watu wasingehamia Mbeya kuwekeza.
 
Mbunge wenu kapangiwa kazi ya kusema ndioooooooooo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Unasema mtu asafiri kwa bodaboda km 33, mbona ni mateso?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cha.muhimimu watu kupanga pamoja shughuli za maendeleo.
 
Mbeya nzima kuna wabunge wawili kam sio watatu

Rungwe hamna wabunge

Kyela hamna mbunge

Mbeya vijijini hamna mbunge

Mbalali hamna mbunge


Mkoa wa songwe angalau tunaona vijana wakijitahidi namna ya kuishi na jamii ila nao

Ileje hamna mbunge
 
Labda huko kwenu lakini kwetu busokelo mambo safi tunakunywa tunalala tunaamka tunachuma chai, tunauza maziwa kwa asas tunapata pesa wewe ulitaka tununue ndege?
Umesahau mananasi


Ila mkuu utajikiaje siku mbunge wako akitafuta mfadhili aweze kujenga kiwanda cha juisi ila tupandishe thamani ya matunda yetu hapo busokelo
 
Nimekaa nimejiuliza sana hili swali kuhusu Wahaya na Wanyaki. Lakini kama ulivyoniambia Mind-Set ndiyo tatizo kubwa.
 
Umesahau mananasi


Ila mkuu utajikiaje siku mbunge wako akitafuta mfadhili aweze kujenga kiwanda cha juisi ila tupandishe thamani ya matunda yetu hapo busokelo
Hayo ndiyo mawazo ya kimaendeleo tunayoyataka siyo kukaa unaponda tu viongozi mitandaoni. Mimi nina hekari mbili za miparachichi ya kisasa Kule next season naanza kuvuna rasmi na soko ni la uhakika, kuna halmashauri zina hali mbaya hapa nchini hata huduma za kawaida za kijamii ni kitendawili
 
rungwe yote ifanywe jimbo moja kuanzia kyela mpaka busokelo halafu apewe Tulia Akson muone maendeleo ya kweli,
Si jimbo litakuwa kubwa sana ??
Halafu kuna hatari moja kubwa, kama mbunge atakuwa mzembe ina maanisha kuanzia Kyela hadi Rungwe kutakuwa na umasikini. Yabaki hivihivi tu.....
 
Hahaha, hii kali, hili lina ukweli wowote ule ?

Ukiishi mmkoa wa Mbeya utajua kwanini makabila mengine hayawapendi Wanyaki, ingawa wao hawakubali yani kama Wakoloni walivyowapendelea Wachaga na Wahaya wao wakajiona ndo wanajua kutawala makabila mengine, kiujumla Wanykyusa ni watu wenye kiburi na dharau awe mwanamke au mwanaume awe na pesa au asiwe na nazo kwao ni kawaida
 
Viongizi wetu bubu na mabomu ya mkono tutaendelea kuwananga popote pale kama hawafanyi kazi watarajiwayo kufanya.

La kwanza barabara ya kufungua wilaya kimaendeleo.
Katumba~Lwangwa ~Itete~Mbambo~Masoko~ Tukuyu barabara hii ni kilio cha miaka nenda rudi.
Wabunge wetu kimya utafikiri nao ni watazamaji tu.
 
Tukuyu-bujela-ijigha masukulu hadi kyela.. barabara na huduma zingine za jamii zina hali mbaya.
 
Wazo zuri sana, lakini wabunge wa kuhamashisha new ideas hatuna.
Kuhamasisha maendeleo siyo kazi ya wabunge. Kama mnasubiri masihi ashuke awahamasishe basi mtasubiri sana sana. Rungwe na Tukuyu kwa nilivyoona haraka mbali na kilimo, mnaweza kuanzisha shughuli za viwanda vidogo vidogo kama alivyosema mkuu kapalamsenga.
Jaribuni kuiga mfano wa Mufindi kule Iringa, ambako hali yake ya hewa inafanana kwa asilimia kubwa na Rungwe na Kyela. Wao pale wana viwanda vingi na hivyo bidhaa zinatoka mashambani na kuuzwa moja kwa moja viwandani hapo hapo. Bidhaa kama chai inaenda Chai Bora, magogo yanaenda kule Sao-Hill au kiwanda cha mgololo.
Hili limepelekea wakulima kupata sana nafuu, na Mafinga kuwa soko kubwa sana ambalo wafanyabiashara wa Afrika Mashariki wanafurika hasa kwenye biashara ya magogo. Rungwe kama mtaamua kutengeneza viwanda vya kusindika chakula mbona mtafika mbali sana na kutakuwa na soko kubwa sana maana badala ya kupata kadhia ya usafirishaji basi mtakuwa mnauza viwandani huko huko. Hili inabidi liende sambamba na kujitahidi kuanzisha mazao mapya ya chakula.
Pili, Rungwe na Kyela kuna vivutio vingi sana vya utalii, kule Arusha wazawa wengi wamejikita sana kwenye biashara ya utalii kwanini ninyi hamuangalii hizi fursa ?? Ukitoka lake Ngosi na useme ulale Tukuyu huwezi kupata hata hoteli na lodge nzuri. Nini tatizo ?? Mkuu Consigliere kasema mindset inabidi zibadilike....
 
Nimekaa nimejiuliza sana hili swali kuhusu Wahaya na Wanyaki. Lakini kama ulivyoniambia Mind-Set ndiyo tatizo kubwa.
Ngoja niwaache Wahaya, niwaongelee Wanyakyusa. Wanyakyusa ni watu wa kusaidiana ila si watu wa kunyanyuana. Wanyakyusa (wanaoishi nje ya kwao) husaidiana kwa tahadhari sana, anayekusaidia huwa makini kuhakikisha hauji kumzidi hapo baadaye na ikitokea ukaonyesha mwekekeo wa kumzidi basi anaweza akakuanzishia tifu from no where, mara upo Pol8si mara Mahakamani. Hao ndiyo Wanyakyusa wa ugenini.
Na wanaposaidiana huwa wanahakikisha anakufahamu na kawaida kuna ubaguzi miongoni mwao.
Wanapokuwa na vikao vyao usitarajie utamkuta wa Keko Magurumbasi amechanganyikana na wa Upanga.
Kuhusu kunyanyuana huwa hawajadili mipango ya maendeleo ya kwao bali huibua mijadala ya majungu tu na kupingana kusiko na tija. Hawawezi kufikiria kwenda kusaidia shule, barabara au hospital, hawajadili mazingira ya elimu, afya n.k wanayopitia watu wa kwao sababu tu watoto au familia zao haziishi huko. Walio kwenye nafasi hawawezi kujenga ushawishi wa mipango kadhaa ya kimaendeleo ikafanyike kwao sababu hawai fikirii jamii ya kwao na watu wao, bali huwaza na kuishia katika level ya familia au ndugu tu.
Wanapenda sana sifa kwa kujisifia maendeleo ya kwao yaliyoletwa wakati wa mkoloni wakati wao hawajachangia hata moja. Akina Mwandosya ndiyo hao wanazeeka na sasa wanahitaji kupumzika. Lakini kwa bahati mbaya sana hakuna aliyeiga na kufuata mfano wake, mbaya zaidi walikua busy kujifanya wapo karibu na Mwandosya na wanamfahamu sana. Moyo wake na intelligence yake anazeeka nayo.

Kuna wakati Wanyakyusa likikua ni kabila la kujivunia, lakini siyo hawa Wanyakyusa wa hivi sasa, sijui wametengenezwa maabara!! Wamepausha na kuupoteza kabisa unyakyusa asilia.
 
🙂
Sasa watu kama wewe, masopakyindi ,Red Giant kwanini msiende kufanya mambo huko kiongozi ?? Kama leo hii Wanyakyusa mkiamua kurudi kejenga kwenu, Rungwe itafika mbali mno maana kama kusoma wengi wenu mmesoma sana.
Mkuu nafikiri siasa siku hizi ni pesa zaidi. Mfano mbunge wa Rungwe(Saul) ni mtu Tajiri, wa Busokelo huko naye si haba. Kingine we mwenyewe kuna siku ulisemaa umeacha kujihangaisha na matatizo ya Tanzania🙂, system sucks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…