Rukwa: Ndege yanusurika kugonga Bajaji iliyokuwa ikikatisha uwanja wa ndege

Sidhani kama unajua ulichokuwa unaandika!! Hahahaaaa....!! JF Daaah


Standard ya Ulimwengu wa Aviation, ni lazima anaetua na ndege apewe ishara na mtu aliye ardhini, HILI NI LA LAZIMA LAZIMA LAZIMA! sasa sielewi unachosema.
 
huo niuwanja wa ndege au uwanja wa gulio LA wananchi...kwoahiyo na bombardier huwa inaturuti mpaka hapo au...?? nifahamishe mdau maana mimi sielewi
 
86d23cffe76af0cea904b0a8b0f56c50.jpg
Katika hali isiyokuwa ya kawaida watu watatu wamenusurika kugongwa na ndege walipokuwa wakisafiri kwa bajaji iliyokuwa ikikatisha uwanja wa ndege wa Sumbawanga mkoani Rukwa ambapo rubani wa ndege hiyo alifanikiwa kuepusha ajali kwa kuipaisha ndege juu upepo wa ndege ukasababisha bajaji hiyo kupinduka na kujeruhi abiria waliokuwemo.

Kukosekana kwa uzio imara katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga kunaweza kusababisha ajali mbaya kutokana na mazoea ya kukatisha katikati ya uwanja wa ndege kwa watembea kwa miguu, baiskeli, pikipiki, magari na hata mabasi madogo ya wanafunzi na abiria kama ambavyo mwishoni mwa wiki imetokea sintofahamu baada ya ndege moja kunusurika kupata ajali ya kugonga Bajaji iliyokuwa ikikatisha uwanja wa ndege hiyo ikitaka kutua.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema ilikuwa majira ya saa nne na dakika ishirini asubuhi ndege ilipokuwa ikitaka kutua uwanjani hapo, rubani alibaini kuwepo kwa bajaji na kupaisha ndege lakini upepo mkali uliweza kupindua bajaji ambayo ilisamasoti mara kadhaa na kuwajeruhi waliokuwa ndani.

Chanzo: Channelten
His inch aibu kweli kweli mamlaka inayohusika ndio imeshindwa kujenga uzio jamani tumefika pahali sasa kila wazo au amri mpaka itoke juu ndipo hapo utaona kila mtu tumbo joto
 
Mkuu mbona pale uwanja wa ndege wa bukoba ndege ilishawahi kumuua mwendesha baiskeli?? Uwanja wa ndege umepakana na barabara na hauna uzio wakati wa kupaa ika vuka ile runway malaa paaaa!!! Sijui kama hata marehemu alilipwa kwani walisema yeye ndio ameigonga!!! Wakati kuna barabara kubwa tu ya magari kwenda kashai na Nyamkazi!! Ila siku hizi waliihamisha hiyo barabara na kuweka uzio.
Na tena pesa zipo za kuhamisha barabara hiyo zaidi maana INA magari mengi na watu wengi
 
Yaani bado Watanzania wanaishi mjini na hawajui matumizi ya Uwanja wa ndege na athari za kukatiza Uwanja wa ndege kwa chombo cha moto!

Vv
 
Subirini uwanja wa Chato ndiyo mtaona jinsi visa kama hivi vitakavyo kuwa vingi. Uwanja wa chato utakuwa malazi ya ng'ombe na punda maana ndege huko zitakuwa ndege moja kila baada ya miezi nane
 
Subirini uwanja wa Chato ndiyo mtaona jinsi visa kama hivi vitakavyo kuwa vingi. Uwanja wa chato utakuwa malazi ya ng'ombe na punda maana ndege huko zitakuwa ndege moja kila baada ya miezi nane
Bwihi
 
Sumbawanga hakuna uwanja wa ndege.Uwanja uliokuwa ujengwe sumbawanga Pinda aliuhamisha ukajengwa wilayani mpanda kwao enzi hizo akiwa waziri mkuu na mpanda ikiwa wilaya ya mkoa wa rukwa.
In short ule hauna sifa ya kuwa uwanja wa ndege.
Pale sumbawanga ccm hakuna ilichofanya cha maana kwa manispaa ile maana hata barabara za mjini ni majanga tu.
Ingefaa uwanja wa ndege ujengwe huku moro gerezani au nambogo nje ya mji kidogo kama ilivyofanyika kwa mbeya mjini.
 
Miaka ya nyuma nikiwa huko tulikuwa tunatupa taka huko karib na uwanja....kwa juu karibu na rukwa retco
 
Miaka ya nyuma nikiwa huko tulikuwa tunatupa taka huko karib na uwanja....kwa juu karibu na rukwa retco
Mwanzon mwa uwanja ndege zinakoanzia kushuka...my be saiv umeboreshwa ila kwa miaka hiyo ulikuwa bdo
 
Back
Top Bottom