JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,462
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Bi.Queen Sendiga amepiga marufuku wanandoa kuachana na kuwaagiza viongozi wa serikali za Vijiji na Kata mkoani humo, kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha kwenye vyombo vya dola vijana ambao watabainika kushindwa kulea watoto wao na kuzitelekeza familia zao majumbani.
Bi.Sendiga ameyasema hayo wakati akizindua zahanati ya Kijiji cha Mpona, kilichopo wilayani Sumbawanga, iliyojengwa kwa nguvu za wananchi.
Chanzo: ITV
Bi.Sendiga ameyasema hayo wakati akizindua zahanati ya Kijiji cha Mpona, kilichopo wilayani Sumbawanga, iliyojengwa kwa nguvu za wananchi.
Chanzo: ITV