Mkuu wa Mkoa Mara aagiza wazazi wa watoto 70 waliokeketwa wakamatwe

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Mkuu wa Mkoa wa Mara Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee tarehe 10/1/2023 ameliagiza Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Tarime/Rorya kuwakamata wazazi/walezi wa watoto 70 waliokuwa wamekimbilia AFTGM Masanga kukwepa ukeketaji na baadaye kurejeshwa kwa wazazi wao baada ya kipindi cha ukeketaji kupita.

Mara.jpg

Akizungumza katika nyumba salama zilizopo katika Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Mzee amelitaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara na Kanda Maalum ya Tarime/ Rorya kuwakamata viongozi wa Serikali za Vijiji na Mitaa ambamo mabinti hao walikuwepo kwa kutokutoa taarifa za matukio ya ukeketaji kwa Mamlaka zinazohusika kabla hata baada ya ukeketaji.

“Haiwezekani wazazi na viongozi wa vijiji na mitaa wanaoishi na hawa watoto waache watoto ambao walishakimbia kukeketwa bila ya wao kutoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika ili kuwanusuru watoto hao au kuwachukulia hatua watu wote wanaohusika na ukeketaji” alisema Mheshimiwa Mzee.

Aidha, Mkuu wa Mkoa amewataka viongozi wa Serikali, Siasa, Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs) katika Mkoa wa Mara kujitathmini kuhusu namna wanavyosaidia au kukwamisha mapambano dhidi ya ukeketaji katika Mkoa wa Mara.

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Mara amelaani tamko lililotolewa hivi karibuni na wazee wa mila wa koo za Wakurya kuruhusu ukeketaji kuendelea hata baada ya msimu wa kawaida wa ukeketaji kuisha na kufanya matambiko ya kuruhusu ukeketaji kuendelea katika kipindi ambacho kilizoeleka sio cha ukeketaji.

“Tamko hili la wazee wa mila linarudisha nyuma jitihada za Serikali na wadau wa maendeleo kupambana na ukatili wa kijinsia na hususan ukeketaji katika Mkoa wa Mara, hatutakubali kuwavumilia, tutawachukulia hatua wote watakaohusika” alisema Mheshimiwa Mzee.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara Mheshimiwa Patrick Chandi Marwa ameeleza kuwa wananchi wa Mkoa wa Mara wanatakiwa kulipa umuhimu suala la kupambana na ukatili wa ukeketaji kwa wasichana na wanawake.

Amewashauri wazee kuendeleza mila nzuri zenye kuleta maendeleo ya jamii na kuacha mila mbaya kama za kukeketa wanawake kutokana na athari za mila hizo katika jamii.

“Tatizo kubwa ni kuwa mwanamke akitahiriwa anaolewa haraka, kuna umuhimu wa kutoa elimu zaidi kwa wanaume ili waache kuoa wanawake waliokeketwa na wote wanaojihusisha na ukeketaji wa wanawake ”alisema Mheshimiwa Chandi.

Mheshimiwa Chandi ameeleza kuwa wazazi wengi wanapenda watoto wao wakeketwe kwa sababu ya matumaini kuwa watoto wao wataolewa na watapata mali nyingi na hususan ng’ombe.

Katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa aliambatana na Kamati ya Usalama ya Mkoa, Kamati ya Usalama ya Wilaya za Tarime, Serengeti na Butiama, baadhi ya maafisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Menejimenti za Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Serengeti na Butiama.
 
Sometimes sio kila kitu ni kukamata na kuweka mahabusu... Hizo gharama nani atazibeba? Serikali inapambana kupunguza mahabusu magerezani kuna watendaji wanapambana kuongeza

Swala la ukeketaji ni la kimila zaidi na lina mizizi mirefu, inahitaji muda, elimu hekima na maarifa ya staha kubwa kuwaelimisha wazazi na jamii waweze kubadili mitazamo yao juu ya swala zima la ukeketaji

Kama watoto walikimbia na wamerudi na kupokelewa na wazazi wao kwa amani hakuna haja tena ya kuanza tena kuzivuruga familia kwa kuwakamata wazazi wao.. hili ni tukio la kukosa maarifa na hekima pia
 
Anayejua FAIDA ZA KUKEKETA atuwekee hapa maana pengine tunalaumu bure Mila hiyo bila kujua faida zake.
 
Nyege zetu zimelala kwenye kisimi...ivo kikikatwa tunabaki watumwa wa ngono...tunafanywa hatujisikii chochote ivo hata wazo la kusaka mchepuko linakuwa hakuna kisimi changu kilipasuliwa na pikipiki
kisimi changu kilipasuliwa na pikipiki
Pole sana rafiki lakini hivyo vya kung'olewa na ajali huwa vinabakia kidogo! Ajali sometimes zina huruma sana
 
Nyege zetu zimelala kwenye kisimi...ivo kikikatwa tunabaki watumwa wa ngono...tunafanywa hatujisikii chochote ivo hata wazo la kusaka mchepuko linakuwa hakuna😭😭😭😭 kisimi changu kilipasuliwa na pikipiki🙇
Basi ni Mila za uonevu Kwa mwanamke na hazipaswi kuendelezwa ni sahihi Kwa serikali kukataza Mila potofu kama hizo
 
Viongozi uchwara wanawekeza ktk ukamataji badala ya elimu bila Kikomo kwenye jamii husika Mambo yakimila yanahitaji hatua mbalimbali kutumika ili kupelekea kupunguza au kuondoa kabisa desturi yao
 
Ni udhalilishaji wa mbususu huo! Tunakemea vikali na kulaani hicho kitendo.
 
Sometimes sio kila kitu ni kukamata na kuweka mahabusu... Hizo gharama nani atazibeba? Serikali inapambana kupunguza mahabusu magerezani kuna watendaji wanapambana kuongeza...
Kwa ushauri wako Basi tatizo hili halitafikia mwisho...hivi jomba nikuulize..wewe unakubaliana na vitendo hivi..na je unadhan ukilichukulia Jambo Hilo kiwepesi unadhan litakwisha..kumbuka suala hili ni la kimila, kijadi..hizi mentality za Hawa jamaa usipotumia nguvu kidogo kuzibadilisha hutafanikiwa.

Yes mazungumzo na wao lazima yaendane na amri na Sheria za nchi..waelewe...wakikaidi amri wachukuliwe hatua tu hakuna jinsi...lazima watii Sheria bila shuruti..tuelewane hapa..tulaani vitendo hivi kwa nguvu zote...ova
 
Na ukikutana na aliyekeketwa utajikamua mpaka ukome na hakuna utakapomfikisha popote.
 
Back
Top Bottom