Mkuu wa Mkoa wa Simiyu atoa siku 7, watoto 24,000 waandikishwe shule

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk. Yahaya Nawanda, ametoa siku saba kwa uongozi wa Wilaya ya Maswa mkoani humo, kuhakikisha unakamilisha kuandikisha watoto 24,000 wanaotarajiwa kuanza masomo ya darasa la kwanza na awali wilayani humo.

Aidha, Dk. Nawanda amemuagiza Mkuu wa Polisi pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo, Aswege Kaminyoge, kuwakamata watu wanaovamia na kulima maeneo ya shule wilayani humo.

RC Nawanda ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Maswaqq, inayolenga kuzifikia wilaya zote za mkoani hapa.

Akiwa katika Shule ya Sekondari Nyalikungu, Kinamwigulu, Buchambi na Zanzui, RC Nawanda ameonya kamwe hatapokea miradi yenye changamoto.

Chanzo: EATV
 
Hongera sana serikali, kuna wakati watoto walitaka kuandikishwa lakini shule hazikuwepo, leo shule zinatafuta wanafunzi,
Hongera sana
 
Back
Top Bottom