Mkuu wa Mkoa wa Manyara: Wanafunzi wasirudishwe nyumbani kwa kukosa hela ya kuchangia chakula

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
Mkuu wa Mkoa Manyara.jpg
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amepiga marufuku Wanafunzi kurudishwa nyumbani na kushindwa kuendelea na masomo kwasababu ya Wazazi kushindwa kuchangia chakula Shuleni.

RC Sendiga ametoa agizo hilo wakati akiongea na Wananchi wa Kata ya Galapo ambapo amesema suala la Watoto kula Shuleni haliwezi kuepukika "Maelekezo ya Serikali ni marufuku Mzazi kukwepa jukumu la Mtoto kula Shuleni lakini ni muhimu Wazazi na Kamati za Shule zikae pamoja kujadili namna bora ya kuwahudumia Wanafunzi chakula Shuleni kulingana na hali ilivyo na sio Walimu kupanga utaratibu wanaoutaka wao, sitaki kusikia Mtoto anafukuzwa Shule, waiteni Wazazi mtengeneze Kamati maalumu kwa ajili ya kuratibu namna ya upatikanaji wa chakula Shuleni"

Hatua hiyo imekuja baada ya Wananchi kulalamika Wanafunzi kurudishwa nyumbani kwa kushindwa kuchangia chakula Shuleni ambapo Mzazi mmoja amesema “Watoto wapo mtaani wamefukuzwa Shuleni, Wazazi hawana chakula, Mzazi anaenda kununua Kilo moja akale yeye na Watoto na apeleke Shule, atapata wapi? hatuna kazi wala vibarua na mavuno shambani hakuna kumekauka, tunaomba hili ulifanyie kazi Mama"
 
Kwaiyo watakula nini?
 
Mzazi ambaye serikali imemhurumia kwamba hawezi toa ada ya day tsh 40000 mpaka 50000 eti huyo huyo amudu gharama za kupeleka mahindi gunia 2 maharage debe 2 na hela za mpishi elfu 50 shuleni kwa ajili ya mtoto wake.Serikali ione namna nzuri ya kuratibu michango hii kwa sababu kila shule inajipangia . Lasivyo muda si mrefu tutaanza kushuhudia watoto wakiacha shule kwa wingi baada ya wazazi kukimbia michango ambayo ni uncontrolled
 
Back
Top Bottom