RUKWA: CHADEMA imemfuta uanachama na kumvua udiwani wa kata ya Majengo, Dickson Mwanandenje

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Rukwa, kimemfuta uanachama na kumvua udiwani, Dickson Mwanandenje aliyekuwa diwani wa kata ya Majengo wilaya Sumbawanga mkoani hapa.

Mwenyekiti wa Chadema mkoa huo, Shadrack Malila maarufu Ikuwo amesema leo Agosti 11 kuwa Baraza kuu la Chadema mkoa wa Rukwa lililokutana jana limeridhia kwa kauli moja kumfuta uanachama diwani huyo.

Amesema sababu ya kumfuta uanachama diwani huyo, ni usaliti ndani ya Chadema.

Amesema mara ya mwisho alipanda jukwaani katika mkutano wa hadhara wa mbunge wa Sumbawanga mjini, Aeshi Hilaly na kumsifia mbunge huyo na chama chake (CCM).

"Sisi tuna ushahidi wa kutosha kupitia ‘Clip’ alishiriki mkutano wa Mbunge wa CCM katika kata ambayo sio ya kwake (Mazwi) na kummwagia sifa mbunge huyo kwamba ameleta maendeleo kwenye jimbo hilo hususani kata ya majengo inayoongozwa na Mwanandenje, kitu ambacho sisi tumetafsiri ni usaliti"amesema.

Amesema kuwa kupitia taarifa za kiintelejensia wamebaini alikuwa kwenye mipango ya kujiunga na CCM kwa dau la zaidi ya Sh 20 milioni hivyo walikuwa kwenye mazungumzo ya mwisho na walipanga kumtangaza katika moja ya mikutano yao ya kisiasa.

Akizungumzia taarifa hizo Mwanandenje amesema kuwa yeye hana taarifa ya kufutwa uanachama wa Chadema japo amesikia tu mitaani.
Akijibu tuhuma zilizoelekezwa kwake, Mwanandenje amesema kushiriki mkutano wa Mbunge sio dhambi ya kufanya avuliwe uanachama na hizo za kuwa katika mchakato wa kujiunga na CCM zimejaa ukakasi tu.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Hamid Njovu alipohojiwa amesema amezisikia taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii lakini kama zitawasilishwa rasmi ofisini kwake ndipo wataangalia kanuni na taratibu zinasemaje kama chama kikimfuta uanachama diwani wake.
 
pigo lingine hili kwa chadema, mwanandenje alikuwa kakihama chama muda mrefu tu..ilibaki kujitangaza mbele ya wanahabari

kata ya majengo smbawanga inarudi ccm uchaguzi wa marudio
 
Sisi tuna ushahidi wa kutosha kupitia ‘Clip’ alishiriki mkutano wa Mbunge wa CCM katika kata ambayo sio ya kwake (Mazwi) na kummwagia sifa mbunge huyo kwamba ameleta maendeleo kwenye jimbo hilo hususani kata ya majengo inayoongozwa na Mwanandenje, kitu ambacho sisi tumetafsiri ni usaliti"amesema.

Hii ndo sababu yaaani inafanya twende tukarudie uchaguzi,lakini kuna mtu alienda hadi ikulu na hakufuzwa uanachama...!!!
 
Kama hizi ndiyo sababu za kufukuzwa basi ,Waitara yupo sahihi.

Kusifia maendeleo ni usaliti??
 
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Rukwa, kimemfuta uanachama na kumvua udiwani, Dickson Mwanandenje aliyekuwa diwani wa kata ya Majengo wilaya Sumbawanga mkoani hapa.

Mwenyekiti wa Chadema mkoa huo, Shadrack Malila maarufu Ikuwo amesema leo Agosti 11 kuwa Baraza kuu la Chadema mkoa wa Rukwa lililokutana jana limeridhia kwa kauli moja kumfuta uanachama diwani huyo.

Amesema sababu ya kumfuta uanachama diwani huyo, ni usaliti ndani ya Chadema.

Amesema mara ya mwisho alipanda jukwaani katika mkutano wa hadhara wa mbunge wa Sumbawanga mjini, Aeshi Hilaly na kumsifia mbunge huyo na chama chake (CCM).

"Sisi tuna ushahidi wa kutosha kupitia ‘Clip’ alishiriki mkutano wa Mbunge wa CCM katika kata ambayo sio ya kwake (Mazwi) na kummwagia sifa mbunge huyo kwamba ameleta maendeleo kwenye jimbo hilo hususani kata ya majengo inayoongozwa na Mwanandenje, kitu ambacho sisi tumetafsiri ni usaliti"amesema.

Amesema kuwa kupitia taarifa za kiintelejensia wamebaini alikuwa kwenye mipango ya kujiunga na CCM kwa dau la zaidi ya Sh 20 milioni hivyo walikuwa kwenye mazungumzo ya mwisho na walipanga kumtangaza katika moja ya mikutano yao ya kisiasa.

Akizungumzia taarifa hizo Mwanandenje amesema kuwa yeye hana taarifa ya kufutwa uanachama wa Chadema japo amesikia tu mitaani.
Akijibu tuhuma zilizoelekezwa kwake, Mwanandenje amesema kushiriki mkutano wa Mbunge sio dhambi ya kufanya avuliwe uanachama na hizo za kuwa katika mchakato wa kujiunga na CCM zimejaa ukakasi tu.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Hamid Njovu alipohojiwa amesema amezisikia taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii lakini kama zitawasilishwa rasmi ofisini kwake ndipo wataangalia kanuni na taratibu zinasemaje kama chama kikimfuta uanachama diwani wake.
Chadema wamemfuta uanachama lakini hawana uwezo wa kumvua Udiwani bali Udiwani unavuliwa na Katiba. Hapo Chadema hawaoni kwamba wanaongeza gharama za uchaguzi kwa kuwatwisha mzigo Watanzania lkn angehama mwenyewe kungeanza propaganda nyingi, oooh CCM wamemnunua,oooh hii ni kuwatwisha mzigo Watanzania kugharamikia uchaguzi. Naiona Chadema inayokufa kibudu...!!
 
🤣🤣🤣🤣🤣
Si Mbunge wake

Sasa mumeanza na kuoneana wivu.. haya aende CCM
Na pia wajue labda alitaka kuondoka kihivyo.. kama ni kweli wanayodai juu yake. Wamemurahisishia gemu
 
upinzani wa Tanzania ni wa ajabu marekani ilioingia Vita kumpiga Saddam Hussein,Osama Na Ghadafi vyama vyote marekani tawala Na upinzani walikuwa kitu kimoja.Tanzania mpinzani kuzaa Na mbunge wake ambaye ndiye mwakilishi wake ili ampe kero azipeleke bungeni ni kosa.Chadema kuna tatizo kubwa kwa hiyo eneo mbunge akiwa CCM diwani Chadema huyo diwani haruhusiwi kupeleka kero zake kwa huyo mbunge iwe kwenye mikutano ya hadhara ya mbunge,ofisini au nyumbani kwake?Huyu diwani kaonewa kama akipewa barua awaburuze mahakamani chadema kwa kumdhalilisha
 
Back
Top Bottom