'Ruksa' kwa watumishi wa umma kushiriki siasa

Hii sheria ina hatari sana kwa wapinzani tu na itapelekea kuhofisha wanamabadiliko wote.

-kama mnanibishia mtaja nieleza!
 
Sheria ya utumishi wa umma,japo kandamizi, hairuhusu mtumishi wa umma kujihusisha na shughuli za kisiasa wakati huo huo akiwa ni mtumishi wa umma.Ukiamua kuingia katika siasa, basi inabidi uache kazi yako serikalini.

Nakumbuka,kuna wakati alipata misukosuko ya kujihusisha na siasa na mpaka leo sijui swala lile lilimalizika vipi.

Cha ajabu,prof.huyu hivi sasa anaonekana kuwa karibu sana na chama cha ACT katika harakati zake za kisiasa lakini inaonekana ni kama yuko sahihi kabisa.Sasa hapa inakuaje?

Majuzi katika kongamano moja, nilimuona, kupitia ITV, akitoa mada kuhusiana na swala hili lakini binafsi sikuridhika na maelezo yake kwanini yeye hajavunja sheri hii ya utmishi wa umma.

Nachojiuliza,hivi leo hii prof.mwingine wa hapo UD nae akaamua kufanya harakati anazofanya prof.Kitila katika chama kingine mfano CHADEMA,atabaki salama?

Hivi Limbu angeweza kumtuhumu Kitila pamoja na Zitto na Mwigamba kama Kitila hajihusisha na siasa ndani ya ATC-Wazalendo?

Maswali ni mengi kuliko majibu!
 
Katila ni Profesa wa ccm, hana tofauti na Kapuya, Maghembe, Migiro, Muhongo, Bana, JK na wengine
 
Nadhani Prof. Mkumbo hana nafasi ya uongozi yoyote ndani ya ACT, ni mwanachama wa kawaida tu. Sheria haikatazi watumishi wa umma kuwa wanachama ila kuwa kwenye uongozi au nafasi za utendaji ndani ya chama.
 
Wana JF,

Napata shida sana kujua tunaposema ni marufuku kwa mtumishi wa serikali kushiriki siasa wakati wako watumishi wa serikali wanaoshiriki siasa za chama tawala wengine tena hata bila kificho hasa huu wakati tunaelekea uchaguzi mkuu oktoba 25, 2015.

Huku kwetu Jimbo la Rungwe, mkuu wa wilaya Zainabu Mbussi, amekua mstari wa mbele katika kuhakikisha;-

1. Mgombea wa CCM anayemtaka yeye pamoja na kundi lake anapita katika mchakato wa kura za maoni, kuanzia
udwani katika kata zote , hadi ubunge wa jimbo la Rungwe.

2. Kudhoofisha nguvu ya upinzani (hasa Chadema maana upinzani ni Chadema) kwa kuingilia michakato yao ya kupata
wagombea ili wapate wagombea dhaifu, hii alijaribu kata ya Kyimo baada ya kuona waliyemchakachua katika kura
za maoni kahamia Chadema.

Lakini nayeye pia akiwa mtumishi wa serikali, amekuwa akiwatisha watumishi wenzake wa serikali wanaoshiriki siasa za upinzani. So where is the fair ground of this game politics, for those who are civil servants?
 
mimi nadhani hao wakuu wa wilaya na mikoa walitakiwa waongoze wanaccm wenzao tu na suala la kuwaongoza wananchi liachiwe viongozi wengine wa serikali.

Wana JF,

Napata shida sana kujua tunaposema ni marufuku kwa mtumishi wa serikali kushiriki siasa wakati wako watumishi wa serikali wanaoshiriki siasa za chama tawala wengine tena hata bila kificho hasa huu wakati tunaelekea uchaguzi mkuu oktoba 25, 2015.

Huku kwetu Jimbo la Rungwe, mkuu wa wilaya Zainabu Mbussi, amekua mstari wa mbele katika kuhakikisha;-

1. Mgombea wa CCM anayemtaka yeye pamoja na kundi lake anapita katika mchakato wa kura za maoni, kuanzia
udwani katika kata zote , hadi ubunge wa jimbo la Rungwe.

2. Kudhoofisha nguvu ya upinzani (hasa Chadema maana upinzani ni Chadema) kwa kuingilia michakato yao ya kupata
wagombea ili wapate wagombea dhaifu, hii alijaribu kata ya Kyimo baada ya kuona waliyemchakachua katika kura
za maoni kahamia Chadema.

Lakini nayeye pia akiwa mtumishi wa serikali, amekuwa akiwatisha watumishi wenzake wa serikali wanaoshiriki siasa za upinzani. So where is the fair ground of this game politics, for those who are civil servants?
 
Baada ya mh rais kuteua makada wa chama chake kuingia kwenye utumishi wa umma, na kuteua watumishi wa umma kwenye vyeo vya kisiasa maana yake ni kwamba lile zuio la kuwakataza watumishi wa umma kutojihusisha na siasa limetenguliwa rasmi, hawa wanasiasa walioingizwa kwenye utumishi wa umma kwa sababu ya ukada wao ni lazima watafanya siasa mahali pa kazi, maana yake kuanzia sasa tutegemee kupata huduma ofisi za umma kwa misingi ya vyama.
Lakini vilevile kuna watumishi wa umma wameteuliwa vyeo vya kisiasa kama ukuu wa mkoa na wilaya hawa nao wataenda kufanya siasa ikiwemo kuingia kwenye vikao vya vyama vyao.

Jambo pekee linalo nisikitisha ni rais kukataa siasa ili hali yeye anafanya siasa, naiona Tanzania ya viwanda.
 
Mnapenda sana kuzunguka huku na kule lakini tatizo ni kwamba mmerithishwa na mamvi. Tokea muanze kuzungusha mikono hamtulii tena
 
Wanajeshi wanaapishwa kuwa wakuu wa Wilaya na mikoa wakiwa wamevaa kombati za jeshi,tukumbuke Mkuu wa Wilaya ni mjumbe wa kamati ya siasa ya Ccm Wilaya....mwanajeshi/mwanasisasa/mwanasisiemu.

Ile falsafa ya kuwaambia akina jk,kinana,chiligati,Makamba waweke vyeo vya kijeshi pembeni hata kama wamestaafu iko wapi?

Hawa wanajeshi watakuwa wakimtii rais kama amiri jeshi anayetoa amri za kijeshi au kama civilian president?
Na kama jeshi haliruhusu siasa...je hawa wameacha Kazi za jeshi?
Rais akiwafukuza watarudi jeshini? Wakirudi watakumbana na adhabu za kutofatilia amri za amiri jeshi Mkuu?

Kikiingia chama kingine madarakani, hawa wanajeshi wanaokaa kwenye kamati za siasa za Ccm watarudi kambini ?sheria za jeshi zinazuia uanachama kwenye vyama,je kuingia kwenye vikao vya Ccm na kupanga mikakati ni sawa?
 
Sina uhakika kama kuna anayejua nchi hii inapelekwa wapi
Juzi DC wa Iringa amekataza mtu yoyote kumkosoa Baba Nanihino kwenye wilaya "yake"
 
Back
Top Bottom