Tangu mwanzo tulionya hapa hakuna kesi sababu ushahidi wa tuhuma dhidi ya washtakiwa unakatika njiani. Haiwezekani ukawashtaki waliopokea fedha na kuzigawa ukawaacha wale waliozitoa benki kuu hii ni akili ya kitoto kutaka kuhangaishana. Kama serikali inawaogopa hao vigogo ni heri wakawaachia hawa ili ijulikane wazi tushaliwa na kila mtu abebe msalaba wake. Kesi ya rushwa ili mtu apatikane na hatia ni lazima akamatwe mtoaji na mpokeaji kinyume na hapo hakuna kesi. Huyo mwendesha mashtaka anasema upelelezi haujakamilika ndiyo maana yake nini? Jibu ni moja tu aliyezitoa hizo fedha hakamatiki!Mfanyabiashara James Rugemalila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anahitaji kuonana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ili ampe ushahidi wa nani anayepaswa kukamatwa katika kesi hiyo.
View attachment 656763
December 8, 2017 Rugemarila aliieleza mahakama hiyo kuwa unahitajika ushirikiano baina yake na upande wa mashtaka ili kumbaini mwizi wa Sh.Bil 309 za Serikali.
Mbali ya Rugemarila, Mshtakiwa mwingine ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababishia Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh.Bil 309.
Rugemarila ameyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leornad Swai kudai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba ahirisho.
Baada ya kueleza hayo, Rugemarila alinyoosha mkono ambapo amesema kuwa anaushukuru upande wa mashtaka ulimchukua gerezani na kumpeleka Upanga kwa mahojiano na kumrudisha salama gerezani.
“Leo nimekuja na ushahidi, hivyo naomba nikutane na DPP ili niweze kumsaidia kumjua mwizi anayepaswa kukamatwa, kwani lengo letu ni kuonyesha kuwa tupo Innocent,” alieleza Rugemarila.
Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Shaidi alimtaka Rugemarila kuwasiliana na mawakili wake ili waandike barua ya kuwasilisha kwa DPP kuhusu suala hilo la ushahidi wake, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi January 5, 2018.
Chanzo: Millard Ayo
Mkuu umenikumbusha kile kibwagizo cha winbo " who let's the dogs out"
Hayo majina yakimfikia unadhani atafanya nini??Kumbe waliiba kweli na mwizi wanamjua? Sasa wapelelezi wanavyosema ushahidi haujakamilika wana maana gani? Habari hii imfikie JPM.
Kwani wewe haumjui yule aliyekuwa kigogo kabisa na alisema hadharani kuwa pesa za escrow siyo za umma!Kumbe anamjua huyo mwizi eh!
Hapo sasa patamu,ngoja tukae mkao wa kula.Mfanyabiashara James Rugemalila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anahitaji kuonana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ili ampe ushahidi wa nani anayepaswa kukamatwa katika kesi hiyo.
View attachment 656763
December 8, 2017 Rugemarila aliieleza mahakama hiyo kuwa unahitajika ushirikiano baina yake na upande wa mashtaka ili kumbaini mwizi wa Sh.Bil 309 za Serikali.
Mbali ya Rugemarila, Mshtakiwa mwingine ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababishia Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh.Bil 309.
Rugemarila ameyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leornad Swai kudai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba ahirisho.
Baada ya kueleza hayo, Rugemarila alinyoosha mkono ambapo amesema kuwa anaushukuru upande wa mashtaka ulimchukua gerezani na kumpeleka Upanga kwa mahojiano na kumrudisha salama gerezani.
“Leo nimekuja na ushahidi, hivyo naomba nikutane na DPP ili niweze kumsaidia kumjua mwizi anayepaswa kukamatwa, kwani lengo letu ni kuonyesha kuwa tupo Innocent,” alieleza Rugemarila.
Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Shaidi alimtaka Rugemarila kuwasiliana na mawakili wake ili waandike barua ya kuwasilisha kwa DPP kuhusu suala hilo la ushahidi wake, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi January 5, 2018.
Chanzo: Millard Ayo
Hawajui mlivyo!!Angemtaja hapo hapo alipopata nafasi ya kuongea.
Hawajui mlivyo!!
Kweli eenh!?Eeeeeeh siko hivyo mimi sipo nao kabisa...