Rufiji: Bonde lilolaaniwa na wanasiasa wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rufiji: Bonde lilolaaniwa na wanasiasa wetu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Game Theory, Jul 20, 2009.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Apparently bonde la Rufiji lina uwezo wa kulisha Afrika Mashariki nzima endapo litatumiwa vizuri na mamlaka husika limetandawaa katika mikoa ya Pwani, Lindi, Morogoro, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Dodoma na Singida!

  Bonde hili lina utiriri wa rasilimali ambazo ni chachu ya uchumi wa nchi hii...lakini wanasiasa wote inluding waziri wa sasa wa KILIMO hawataki kuelezea mkakati gani wanao ili wa utilize hii rasilimali ulionayo

  Tunaambiwa kuwa kilimo ndcho kitatukwamua lakini watawala hili hawataki kulisema linapofikia suala la BONDE LA RUFIJI


  Naona waziri mkuu Pinda ameamua kulivalia njuga hili suala la kilimo na who knows maybe watakuwa na mikakatmaalum kuhusus hili bonde lakini hilo hatulijui kwa sababu ofisi ya waziri mkuu haina website kama ilivyo ofisi ya JK hivyo hatujui mipango ya serikali yetu japo wanachukua kodi toka kwetu


  Kwa mujibu wa taarifa za shirika la Chakula na Lishe (FAO) kuna hekta zisizopungua 622,622,400 zifaazo kwa kilimo cha kiangazi (cha umwagiliaji) katika bonde lote la mto Rufiji.  Ambapo bonde la Usangi limemega hekta 208,000 kati ya hizo, Ruaha napo pakameza hekta 5,800 huku Kilombero paliichukulia hekta 329,600 na Rufiji chini yakiwa na hekta 70,000.


  Halafu mtu anakwambia kuwa Bongo kuna njaa sisi tutoe wapi njaa ili hali tumejaaliwa Bonde la Rufiji?
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  hii ndo Tanzania ambayo wanasiasa wamekuwa wajuaji sana kwa kuleta kauli mbiu mpya kila siku zinazohusu kilimo kama vile kilimo kwanza na nyinginezo ila kimsingi uwekezaji wa maana katika kilimo bado, nia aibu maeneo kama hayo ya rufiji yameachwa tu then tunakimbia kuomba chakula cha msaada... ole wako tanzania.
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  hakuna strategic plan ya kilimo

  wazara ya Kilimo haina website

  Rais hana website

  wizara ya mipango hazina website

  ofisi ya waziri mkuu haina website

  and no one cares
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Serikali inayo strategy ya kilimo. Ni kuwakabidhi Wasaudi eka laki tano watulimie mpunga.
   
 5. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Watulimie mpunga au SISI tuwalimie wao mpunga?

  Utashangaa watu watapigwa viboko na mpunga wote ukaishia Saudia.

  Wala sitoshangaa baadae kusikia SAUDIA ni NCHI YA TATU DUNIANI kwa kilimo cha mpunga (ULIOLIMWA TANZANIA).

  You go figure!
   
 6. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Right on Jasusi.
   
 7. Insurgent

  Insurgent JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2009
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 469
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kuna wengine wanakimbilia kuwapa wageni maeka ya mapori ili walime "bio-diesel". Vipaumbele vyetu vina walakini...
   
 8. K

  Kleptomaniacs Member

  #8
  Jul 21, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nani kawaambia hawana mkakati na bonde la Rufiji? nenda kashuhudie SEKAB, BIOSHAPE, Waturuki na wengineo kibao wanavyopigana vikumbo huko Rufiji, maeneo yote kuanzia Mloka mpaka karibu na Ikwiriri, kutoka njia panda ya kuja Utete ambako wapo waturuki eti wakilima mahindi mpaka vijiji vinavyopakana na Utete. Kote huko jamaa wame earmark! nyie mwala raha mjini wengine na mabox ulaya na marikani! Mkwere hana mchezo anataka kuiendeleza Pwani bwana!
   
 9. K

  Kleptomaniacs Member

  #9
  Jul 21, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tena hao BIOSHAPE wao tayari washaweka base pale Kilwa na mijatrofa inastawishwa kama kawa, uliza walichofanya walipofika huko? walilazimika kwenda na misumeno kwanza kuandaa shamba! hizo mbao walipeleka wapi? nchi tamu sana hii, u come wiz nothing you move wiz something!
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  [quoteNani kawaambia hawana mkakati na bonde la Rufiji? nenda kashuhudie SEKAB, BIOSHAPE, Waturuki na wengineo kibao wanavyopigana vikumbo huko Rufiji, maeneo yote kuanzia Mloka mpaka karibu na Ikwiriri, kutoka njia panda ya kuja Utete ambako wapo waturuki eti wakilima mahindi mpaka vijiji vinavyopakana na Utete. Kote huko jamaa wame earmark! nyie mwala raha mjini wengine na mabox ulaya na marikani! Mkwere hana mchezo anataka kuiendeleza Pwani bwana!] [/quote]

  hakika wasije tu kugusa shamba langu pale.

  Hili Bonde ni zuri sana na utajili asilia wa kutoka kwa Mola. Hakika ndani ya bonde hili kuna maeneo mazuri sana ya kilimo ( kuanzia Mloka ,kilimami, mkongo na kuelekea utete, na kukatisha toka mkongo mpaka ikwiriri, Namwage, mpaka mohoro.

  Vile vile kuna maeneo mazuri sana ya Uvuvi kama kwenye Delta yaani kuanzia visiwa vya pombwe,sarali, mnekeya na kiongoloni.

  Kuna maeneo mazuri sana kwa uwindaji kuanzia kipo, stigo mpaka kule mbuyu kemp.

  Hakika kuna ndugu yangu Bw HAFFIF huwa nikija dar basi lazima akanitembeze huko na nimepata Heka 200 maeneo ya bonde la Nyamwage nakusudia kulima Mpunga.

  Prof Idris Mtulia (Mbunge wa Rufiji) na Mh Malumbo (Mbunge wa Kibiti) wanajitahidi sana kufanya mambo ila wanahitaji msukumo zaidi kupata wawekezaji

  na
   
 11. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  hakika wasije tu kugusa shamba langu pale.

  Hili Bonde ni zuri sana na utajili asilia wa kutoka kwa Mola. Hakika ndani ya bonde hili kuna maeneo mazuri sana ya kilimo ( kuanzia Mloka ,kilimami, mkongo na kuelekea utete, na kukatisha toka mkongo mpaka ikwiriri, Namwage, mpaka mohoro.

  Vile vile kuna maeneo mazuri sana ya Uvuvi kama kwenye Delta yaani kuanzia visiwa vya pombwe,sarali, mnekeya na kiongoloni.

  Kuna maeneo mazuri sana kwa uwindaji kuanzia kipo, stigo mpaka kule mbuyu kemp.

  Hakika kuna ndugu yangu Bw HAFFIF huwa nikija dar basi lazima akanitembeze huko na nimepata Heka 200 maeneo ya bonde la Nyamwage nakusudia kulima Mpunga.

  Prof Idris Mtulia (Mbunge wa Rufiji) na Mh Malumbo (Mbunge wa Kibiti) wanajitahidi sana kufanya mambo ila wanahitaji msukumo zaidi kupata wawekezaji

  na
   
 12. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Cha kusikitisha na kushangaza ni kuwa bonde hilo bado kabisa halijaguswa itakikanavyo kwa madai kuwa eti uwezo wa Taifa wa kugharamia "miradi mikubwa" ya umwagiliaji ni mdogo hasa ikizingatiwa kwamba miradi hiyo inahitaji "fedha nyingi" za kigeni kununulia zana za kilimo.

  Aidha, hoja nyingine inayotolewa na mamlaka husika (Rufiji Basin Development Authority - RUBADA) ni kuwa eti, nchi hii ina upungufu wa wataalam wenye ujuzi na uzoefu wa muda mrefu wa kuendesha mashamba ya umwagiliaji! Hata hivyo, mamlaka hiyo inakiri kwamba tatizo hilo linazidi kupungua jinsi miaka inavyokwenda lakini haioneshi kivitendo ukweli wa kauli hiyo.

  Cha kujiuliza zaidi juu ya hoja hizo mbili ni kuwa endapo serikali inaweza kuikarabati Ikulu kwa mabilioni ya shilingi, kununua magari ya anasa na kuwajengea makasri ya kifahari "waheshimiwa" vipi ikose fedha za kuendeleza kilimo cha kiangazi katika bonde hilo ambalo sehemu zake nyingi hazihitaji mitambo yoyote ya gharama kubwa, kwani umwagiliaji wake ni wa nguvu za mtiririko wa maji?
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  Jul 21, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  Akilini mwa viongozi wetu wengi strategy sahihi ya kuendeleza nchi yetu ni kuita wawekezaji.Hata kwenye mambo ambayo tunayaweza, tumejiwekea imani kuwa hatuyawezi. Sasa sisi tunaweza nini? That is sad story!!
  By the way ile hela ya chai wizara ya fedha haiwezi kusaidia kuanzisha website ambazo zitazifanya wizara zetu ziwe na access? Maana nimepania kweli kupata ajira wizara ya fedha kubana matumizi ya kunywa chai kila siku. Inakula kwangu mjini hapa!!
   
 14. B

  BondJamesBond Member

  #14
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  no one cares...
   
Loading...