Rufaa ya Lema kusikilizwa leo

Rufaa ya Lema kusikilizwa leo

Status
Not open for further replies.

WOWOWO

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2011
Posts
599
Reaction score
457
Bila shaka leo ndiyo kucheka au kulia tena kwa Wananchi wa Arusha Mjini. Jopo la Majaji likiongozwa na Jaji Mkuu linatazamiwa kutoa hukumu ya Rufaa ya aliyekuwa Mbunge wao kipenzi Godbless Lema. Matumaini yetu ni Ushindi kwa wana Arusha hasa ukizingatia rufaa ya Lema imesimamiwa na Wanasheria mahili wa CDM kama Tundu Lisu.Walio Arusha tupeni hali halisi ya Jiji hilo na nini kinaendelea.

Naomba kuwasilisha..
 
Dah, unawahi kitu gani?

Mkuu sioni tatizo la kuwahi hapa, lengo ni kuwa na thread itakayotupa hali halisi ilivyo Arusha kabla, wakati na baada ya hukumu ya rufaa yenyewe kutolewa. Si wote tuko Arusha au Tz, tunatamani tungekuwepo lakini waliopo huko wanaweza kubisa kutupa Live updates na tukapata picha halisi.
 
hasa ukizingatia rufaa ya Lema imesimamiwa na Wanasheria mahili wa CDM kama Tundu Lisu..
Huyu Tundu Lissu basi atakuwa mtenda miujiza, juzi tu kajiunga na utetezi, amefanya kazi ya utetezi siku mbili?
 
Dah!Nilifikiri mahakama imeanza

Mkuu hata mimi nilifikiri hivyo hasa pale nilipoona neno LIVE KUTOKA MAHAKAMANI....! Nadhani kuna wakati tulikubaliana humu kuhusu uanzishaji wa thread za live. Ili kuepuka multiple threads tulisema either mods waamzishe thread moja au mtu ambaye yupo eneo la tukio aanzishe na watu wote wawe wanafuatilia hiyo thread moja. Naona jamaa kaaanzisha ili awe mwanzilishi japo hayupo kwenye hayo makundi! Haya mkuu tuombe mods waifanye hii ya kwako iwe sticky japo kwa leo ili updates ziwe zinatupwa humu.
 
Mkuu hata mimi nilifikiri hivyo hasa pale nilipoona neno LIVE KUTOKA MAHAKAMANI....! Nadhani kuna wakati tulikubaliana humu kuhusu uanzishaji wa thread za live. Ili kuepuka multiple threads tulisema either mods waamzishe thread moja au mtu ambaye yupo eneo la tukio aanzishe na watu wote wawe wanafuatilia hiyo thread moja. Naona jamaa kaaanzisha ili awe mwanzilishi japo hayupo kwenye hayo makundi! Haya mkuu tuombe mods waifanye hii ya kwako iwe sticky japo kwa leo ili updates ziwe zinatupwa humu.

Kweli mkuu!
 
Ieleweke kuwa mawakili wawili ktk kesi hii wamefiwa na baba yao! Kwa hiyo bado haijaeleweka kama kweli hukumu itapitiwa au hapana!
 
dah .. saa 5: 52 asubuhi ....

mkuu tupe update please ... chai na vitafunwa tayari
 
Kaaaazi kweli kweli, let's wat n see
 
Huyu kweli ni mkereketwa halisi..hebu nijiamkia zangu .nilifikiri ni saa tano za asubu na nimechelewa baada ya kuona hii uzi.
 
Mkuu uzi mzuri lkn sio wkt wake na umeanzishwa na mtu ambaye si husika,ingepaswa uzi uanzishwe na mtu aliyeko mahakamani na si wewe ambaye unaetaka watu wa arusha wakupe update! Mods plz futa huu uzi,aanzishe mtu aliyoko mahakamani.
 
Kutokana na baadhi ya watu kuamini siasa ni mchezo mchafu au wajinga ni chakula cha wasomi kuna tetesi zinazoenea kuwa baada ya G. Lema kuvuliwa ubunge kuna kiasi cha shilingi milioni 80 za chama hazijulikana zilipotelea wapi na wala zilitumika katika shughuli gani ila ili CDM kiendelee kuwa na wanachama viongozi wa juu wamefunika swala hilo.

My take:
kama ni kweli kuna ubadhilifu mkubwa hivyo kunatakiwa mapato na matumizi ya chama kubandikwa katika kila ofisi ya chama ili kuwawekea wanachama imani katika viongozi wao
 
Sasa mbona mnaujaza uzi hata kabla tukio halijajili.?
 
Mod futa uzi huu, haiwezekani tutende kinyume cha makubaliano, nitaenda mahakamani mie, futa futa tafadhali
 
Unanitafutia Ban, nilifikiri kumekucha kumbe bado
 
Hizo pesa zote alizipata wapi? Yeye ni mweka hazina wa chama? Hii kitu naona kama haiwezekani mwanachama mmoja kujimilikisha kiasi chote hicho cha fedha. Ingekuwa ni zile za kukusanya labda lakini kwamba kwa kuwa Mbunge alikuwa na access na kiasi chote hicho cha pesa!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom