Rufaa na Hukumu ya Babu Seya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rufaa na Hukumu ya Babu Seya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 9, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  THE Court of Appeal would on Thursday deliver its judgment in the landmark appeal involving Nguza Viking, alias Babu Seya and his three sons, currently serving life jail terms for raping and sodomising minors about seven years ago.

  Deputy Registrar of the court John Mgeta said in Dar es Salaam today that the parties involved have already been notified.

  The appeal was heard by Justices Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk and Salum Massati. Advocates Mabere Marando and Hamidu Mbwezeleni, represented the appellants.

  Principal State Attorney Justus Mulokozi and Senior State Attorney Yohana Masal, for the republic, called upon the justices to uphold the decision of High Court Thomas Mihayo delivered on January 27, 2005.

  Mr Marando and Mbwezeleni, for the appellants, argued that evidence tendered by the prosecution was insufficient, had lot of contradictions and incredible grounds to clinch conviction of their clients.

  Babu Seya and his sons Papii Nguza, Nguza Mbangu and Francis Nguza, were convicted of rape and unnatural offences allegedly committed between April and October, 2003.

  They submitted that the trial court never conducted examination on the girls aged between six and eight years in order to satisfy itself that they understood the meaning of oath and possessed enough competence of speaking the truth as required by law.

  Such omission, according to the advocates, was fatal and, hence the testimony given by all victims was unsworn evidence and should not only be disregarded but also discounted.

  They cited several authorities to back up the submissions and said, therefore, the offences were not proved.

  The advocates further attacked the judgement given by Principal Resident Magistrate Addy Lyamuya at the Kisutu Resident Magistrate’s Court in Dar es Salaam, saying it was problematic and that they had never seen a judgement of that nature that contained several irregularities which were fatal.

  They also complained on the way both Mrs Lyamuya and High Court Judge Thomas Mihayo treated the defence evidence, saying his clients’ evidence particularly that of alibi was not accorded any weight and they shifted the burden of proof to them to prove their innocence, which was illegal.

  However, the prosecution supported the findings by the trial court and the court in the first appeal.

  Mr Mulokozi admitted that the trial court never recorded the examination of victims before taking their evidence, but that was not fatal to the extent of ignoring their evidence.

  The state attorney told the court that evidence given by the minors was water tight and both the trial court and the first appellate court were right in holding responsible the appellants for committing the offences against the girls of such tender age.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,534
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  mwee papi kocha toka uje utupe rap ya level seat serikali inmekataza kushika bombaaaaa eeeeh.....aaaah
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  siju watatoka!
   
 4. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Well tunawaombea; hivi DNA evidence haikuweza kutumika hapo?
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,684
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  Kipimo hii ilikuwa bado kuja tz. Labda wapime sasa kama bado inaweza kuonyesha what happened
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 42,021
  Likes Received: 37,327
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kesho ndiyo hukumu ya rufaa ya kesi ya Babu Seya na wanae, kwa fikra zako, wataachiwa huru ama wataendelea kusota? Kwa nini?
   
 7. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Baba na Mwana tunaimba na kucheza...........watatoka tu
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Feb 10, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  " mara jaji akasikika akisema Ndugu Nguza mbamgu, Pappii, Francis sio waliobaka hao watoto, na nina waagiza polisi wawalete hapa waliobaka hao watoto.." mara mahakama nzima ikaripuka shangwe na vigelegele, Nguza akapiga magoti chini akamshukuru Mungu.....! mara nikastuka kutoka usingizini, na ndoto yangu ikaishia hapo.
   
 9. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,561
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  adhabu alopata inatosha watatoka sasa
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 42,021
  Likes Received: 37,327
  Trophy Points: 280
  Afadhali hata walikata rufaa..
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,772
  Likes Received: 4,913
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  [​IMG]
  Kesho ndiyo hukumu ya rufaa ya kesi ya Babu Seya na wanae, kwa fikra zako, wataachiwa huru ama wataendelea kusota? Kwa nini? Toa maoni yako!

  http://www.globalpublisherstz.com/
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 43,122
  Likes Received: 27,077
  Trophy Points: 280
  waachie tu. enough 4 them nw.
   
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,772
  Likes Received: 4,913
  Trophy Points: 280
  BABU SEYA KUTOKA JELA KESHO?


  [​IMG]
  Kutoka kushoto, Babu Seya, Papii Kocha, Nguza Mbangu na Francis Nguza wakisikiliza kesi yao mwaka jana.​

  MAHAKAMA ya Rufaa Tanzania kesho inatarajiwa kusoma uamuzi kuhusu rufaa ya mwanamuziki maarufu wa dansi, Nguza Viking na wanawe watatu...
  Nguza maarufu kwa jina la Babu Seya na wanawe wapo jela wakitumikia kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kubaka na kulawiti.

  Kwa mujibu wa notisi waliyopatiwa leo mawakili wa serikali na wa walalamikaji, majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk,na Salum Massati,wataisoma rufaa namba 59 ya mwaka 2005.

  Watu wengi wakiwemo mashabiki wa wasanii hao wanasubiri matokeo ya rufaa hiyo.

  Juni 25, 2004 Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kusutu, Dar es Salaam, Addy Lyamuya, aliwatia hatiani Babu Seya na wanawe Papii Nguza ‘Papii Kocha', Nguza Mbangu na Francis Nguza.

  Wasanii hao walituhumiwa kutenda makosa kumi ya kubaka watoto wa wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huo huo kati ya April na Oktoba 2003 katika maeneo ya Sinza kwa Remmy, Dar es Salaam.

  Wakili wao, Mabere Marando, amedai kuwa, Hakimu Lyamuya, aliingiza maslahi yake binafsi na hakuwa akizingatia ushahidi uliokuwa ukitolewa na upande wa washitakiwa.

  Marando amedai kuwa, hakimu huyo alitoa kipaumbele kwa mashahidi wa upande wa Jamuhuri na kupuuza mashahidi wa upande wa washitakiwa hivyo kuwanyima haki.

  Kwa mujibu wa Marando, watoto wote waliokwenda mahakamani kuthibitisha kwamba walibakwa au kulawitiwa na washitakiwa walitoa ushahidi bila kiapo isipokuwa mmoja kati ya 10 waliotoa ushahidi.

  Amedai kwamba, watoto hao pia hawakurekodiwa ushahidi wao kabla ya kutoa ushahidi mahakamani jambo ambalo linakiuka sheria.

  Marando amedai kuwa, baadhi ya watoto waliotoa ushahidi walikiri kutomtambua Babu Seya na washitakiwa wengine na kwamba, ripoti ya Daktari ilionyesha kwamba miongoni mwa watoto hao walikuwa ni bikira hivyo kumaanisha kwamba walikuwa hawakufanya kitendo chochote kilichohusiana na mashitaka hayo.

  CHANZO: HABARILEO

  Babu Seya abanwa gerezani


  [​IMG] Chanzo chetu cha habari kilichoko Gereza la Ukonga walikofungwa wanamuziki hao kimesema mara baada ya kurudi gerezani kutoka mahakama ya rufaa, Nguza alizungukwa na wafungwa wenzake na kubanwa na maswali.

  "Baada ya wakata rufaa hao kupelekwa mahakamani Desemba 3 mwaka huu, wafungwa wengi gerezani humo walijua kuwa siku hiyo, Babu Seya na wanaye wataachiwa huru kwa kuwa walishuhudia wakipewa nguo za kiraia lakini walishangaa kuwaona wakivalishwa tena ‘kombati' za wafungwa mara baada ya kurudi," kilisema chanzo hicho.

  Mtoa habari wetu alisema mara Nguza na wanawe walipoingia gerezani, kundi la wafungwa lilimzunguka kila mmoja akitaka kujua kilichojiri mahakamani lakini watoto wake hasa mdogo Francis walikuwa wakibubujikwa na machozi.

  Wakata rufaa hao waliotiwa hatiani miaka mitano iliyopita rufaa yao inaunguruma katika Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam chini ya majaji watatu, Salum Massati, Mbarouk Mbarouk na Bi. Nathalia Kimaro anayeongoza jopo hilo.

  Jaji Kimaro na jopo lake akiahirisha kesi hiyo baada ya kusikiliza utetezi wa mawakili wa wakata rufaa, Mabere Marando, akisaidiwa na Wakili kutoka Zanzibar, Hamidu Mbwelezeni, alisema mahakama hiyo itatangaza siku ya kutoa hukumu hiyo na wakata rufaa kurudishwa gerezani. Adaiwa kuchinja mke watoto wakishuhudia
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Feb 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,772
  Likes Received: 4,913
  Trophy Points: 280
  Kesi ya Babu Seya na wanae, VILIO UPYA


  [​IMG] Katika rufaa ya kesi hiyo iliyovuta umati wa wasikilizaji katika mahakama hiyo, ilianza kuunguruma majira ya saa tatu asubuhi ikiwa na jopo la majaji watatu, Mbarouk Salim, Salum Massati pamoja na Nathalia Kimaro, aliyekuwa akiliongoza jopo hilo.
  [​IMG]
  Kabla ya rufaa ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa, ndugu na jamaa wa familia hiyo walianza kuangua vilio mahakamani hapo baada ya kumuona Babu Seya na wanaye, Papii Kocha, Nguza Mbangu na Francis Nguza wakiamrishwa kushuka kwenye karandinga lenye nambari za usajili STG 6355 na maafande wa magereza.

  Mwanamke mmoja aliyekuwa miongoni mwa waliokuwa wakiangua kilio katika viunga vya mahakama hiyo alisema kuwa, kilichomtoa machozi ni hali za wapendwa wao hao ambao alikuwa hajawaona tangu walipotiwa hatiani, Juni 25, mwaka 2004.

  Mwanadada huyo alidai kuwa, Babu Seya na wanaye wamezeeka kwa asilimia ishirini na tano ukilinganisha na hali waliyokuwa mwaka 2004 kabla ya kuswekwa gerezani.

  Baada ya kupandishwa kizimbani, wakili anayewatetea wakata rufaa hao, Mabere Marando, aliiomba Mahakama hiyo isogeze mbele rufaa kwani awali ilikuwa chini ya Wakili Albert Nyange kabla ya kukabidhiwa kwake Novemba 27, mwaka huu.
  [​IMG]
  Marando alidai kuwa, muda waliopewa ni mfupi mno hivyo kuiomba mahakama kutoa muda zaidi ili kuichambua kesi hiyo kwa ajili ya kuwatetea wateja wake.

  Marando ambaye kabla ya kuanza kusikilizwa rufaa hiyo, aliongeza sababu zaidi za rufaa hiyo ambapo zilifikia jumla ya sababu 19 pamoja na sababu zilizowasilishwa awali na Wakili Nyange.

  Wakili Mkuu wa Serikali katika Rufaa hiyo, Justus Mulokozi alikubaliana na Marando katika hoja hiyo na kusema kuwa hata yeye ameshindwa kuzipitia sababu zilizoongezwa na Marando kwani zimemfika muda mfupi kabla ya kuanza rufaa hiyo.

  Baada ya Wakili Mkuu wa Serikali kukubaliana na hoja ya Marando, Jaji aliyekuwa akiliongoza jopo hilo, Nathalia Kimaro, aliiahirisha kesi hiyo hadi Desemba 3, mwaka huu, ambapo wakata rufaa hao watafikishwa tena mahakamani hapo ambapo Babu Seya na wanaye walirejeshwa katika Gereza la Ukonga.

  [​IMG]
  Hii ni rufaa ya pili kwa kesi hiyo ya Babu Seya na wanaye, baada ya ile ya kwanza iliyowasilishwa mwaka 2005 kukataliwa mbele ya Jaji Thomas Mihayo wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambaye aliikataa na kukubaliana na hukumu iliyotolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Addy Lyamuya, Juni 25, 2004.
   
 15. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Baba yetu uliyembinguni, jina lako litukuzwe. Tunajua ya kwamba wewe ndiye muweza na muumba wa vyote vilivyomo humu duniani. Wewe ndiye uliyewapa watawala wetu mamlaka waliyonayo.

  Tunatambua ya kwamba hakuna ajuaye ukweli halisi wa mambo aliyoyafanya babu Seya na familia yake isipokuwa wewe Mwenyezi Mungu.

  Ndugu zetu hawa wameshakaa jela yapata miaka mi 5 wakitumikia kifungo cha maisha kwa makosa yanayowakabili.

  Tunakuomba BWANA, mapenzi yako yatimizwe katika suala linalowakabili. Leo ni siku ya hukumu yao. Tunaomba uwepo wako uwafunike mahali walipo. Sisi kama wanadamu tunapenda kuwaona tena wakiwa ni familia huru.

  Tunajua wameshajifunza kwa muda huo waliokaa huko! BWANA Mungu, mapenzi yako na yatimizwe. Sio kama tupendavyo sisi ila tunaomba kikombe kinachoikabili familia ya Babu Seya kiwaepuke.

  Tunashukuru kwa kuzidi kuwafariji na kuwapa afya njema kwa kipindi chote walichokaa huko jela. Tuna amini ya kwamba leo utatenda Muujiza, na watakuwa huru.

  Ndilo ombi letu katika jina la YESU Kristo na Mwokozi wetu, AMEN.

  You will always be the Almighty God
   
 16. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #16
  Feb 11, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,855
  Likes Received: 893
  Trophy Points: 280
  tenda haki baba mungu kila mtu kwa fungu lake,amen.
   
 17. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #17
  Feb 11, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  surely, HE does!
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Feb 11, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  Tunaomba haki itendeke
  Kama wanamakosa kweli waadhibiwe na kama wako katika haki ,,yeye ndo muweza wa wote
   
 19. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #19
  Feb 11, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Amen,
  I believe whenever there's light, there's NO darkness!
   
 20. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #20
  Feb 11, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,667
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Tupeni updates mliopo Dar.
  I wish them out
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...