Rudeboy ashauri wanaume pia kukataa uhusiano wowote wa kimapenzi na mwanamke fukara!

Los santos

JF-Expert Member
Jan 14, 2021
1,085
2,383
Paul Okoye, maarufu kama Rudeboy kutoka kundi la muziki wa Afrobeats la PSquare amezua gumzo mitandaoni baada ya kuwashauri wanaume pia kukumbatia hulka ya kukataa mpenzi wa kike asiye na hela, kama wanavyofanya wanawake wengi.

Ifahamike kwamba idadi kubwa ya wanawake wakati wa kufanya chaguo la mwanamume wa kuingia katika uchumba naye, wengi huangalia kigezo cha ‘mwanamume mwenye hela’ na kama huna hela mtoto wa kiume unakataliwa papo hapo.

Sasa Rudeboy anahisi kwamba ni wakati wanaume pia waanze kufuata mkondo huo, akisema kuwa kama wanawake wanavyochagua mwanamume mwenye hela wakati wao hawana chochote cha kuchangia katika mapenzi, basi pia wanaume waanze kuchagua ‘mwanamke mwenye hela’ na kama hana akwende zake pia.

Msanii huyo kupitia instastory yake aliwauliza wanawake watajihisi vipi ikiwa wanaume pia wataanza kuchagua wanawake wenye hela, je wengi wao watapata wapenzi kweli ama wataishia pia kulia.

Rudeboy alisema kwamba wanaume wengi wanapitia aibu zilizokithiri mikononi mwa wanawake wanapopeleka ombi lao la kutaka mapenzi, wengi huishia kusimangwa na kutukanwa vibaya kisa hawana hela.

“Tafadhali wanaume wenzangu, acheni kuoa wanawake mafukara… kwenu nyinyi wanawake, hiyo inaeleweka aje? Mbona kila wakati mnawaaibisha wanaume kisa ufukara? Nafikiri ni wakati wanaume waanze kuchumbiana na wanawake wenye haiba zao kupitia hali zao za kifedha,” Rudeboy alisema.
FB_IMG_1716629364150.jpg
 
Wanawake ndio ombaomba?
 
Oohh kwahiyo na wanawake nao waanze kuangalia tabia njema, na ujuzi wa kufanya kazi za nyumbani kwa wanaume, kama ambavyo wanaume wanaangalia sifa hizo kwa wanawake au hajafikiria hilo

By the way wanawake wengi wanafuata pesa kwa wanaume, kwa sababu wanajua wanaume wengi hawana mapenzi ya dhati, wanaume wengi wanadate kwa ajili ya ngono tu wakishakuchoka wanakuacha

So mwanaume hana cha kupoteza ila mwanamke anakuwa kapotezewa muda wa kuolewa na kuzidi kuongeza mileage ya papuchi tu, kwahiyo wanawake nao wakaona waanze kuwapotezea pesa wanaume, ili hata wakiachwa walau nao waambulie kitu wasiachwe mikono mitupu
 
Mwanamke fukara unamuonea huruma unamuo, mbeleni anakusaliti kwa lijamaa lenye hela. Unashindwa uue yupi kati ya wawili hao walioharibu ndoa, unaamua isiwe taabu unamuacha mwanamke akaolewe na mwenye hela kiu yake itulie
 
Back
Top Bottom