Rubani wa Helikopta iliyombeba Raisi wa Iran aligoma kutii maelekezo ya kiongozi wa msafara aliyekuwa mbele akasababisha kifo cha Raisi

Shotocan

JF-Expert Member
Nov 21, 2023
2,889
6,097
Msafara wa Raisi wa Iran ulikuwa na Helikopta tatu moja ikiongoza msafara ikiwa na walinzi na Maafisa usalama wa Irani na Maafisa wengine wa serikali ya pili katikati ilikuwa imembeba Raisi wa Iran na waziri wa mambo ya nchi za nje na imamu mkubwa wa Iran ikiendeshwa na pilot Mwanajeshi mwenye cheo kikubwa kijeshi na uzoefu kuliko marubani wote kwenye hizo helikopter zote na helikopta ya tatu nyuma ilikuwa ya walinzi na Maafisa usalama wa Taifa wa iran na Maafisa wengine

Helikopta ya kwanza na ya tatu ilikuwa zilikuwa zikiendeshwa na askari Wenye vyeo vya chini kuliko rubani wa helicopter ya Raisi

Sasa wakiwa kwenye msafara helikopta ya mbele iliona mbele kuna hali ya hewa sio nzuri.Mtu aliye mbele huona vizuri kuliko wa nyuma.Basi akawasiliana na marubani wote wa helikopta zote kuwa wazipandishe juu helikopta zao Hali ya hewa mbele mbaya wanyanyanyue juu helikopta zao .Akawa anarudiarudia kitendo ambacho kilimkera rubani wa helikopta ya Raisi akaona kama kero kama vile yeye na uzoefu wake hajui akaamua kuzima mwasiliano ya Helicopter yaani Transponder na kukataa kutii maagizo

Helikopta ya mbele ya kwanza mbele ikaongeza kupaa juu zaidi na ya tatu lilikuwa nyuma ikapaa juu zaidi
Ya Raisi rubani akagoma kupaa juu zaidi akabaki vilevile kiwango Cha upaaji uleule hajafika mbali akakutana na Hali ya hewa mbaya marubani wenzie walioongeza kiwango Cha kupaaa wakatua Salama
 
Mmejuaje hayo yote ilihali walifariki wote?
Helikopta mbili zilizotua Salama wameongea na Mkuu wa utumishi serikali aliyekuwa helikopta ya mbele aliongea na vyombo vya habari kuwa mawasiliano ya helikopta ya Raisi yalizimwa lakini hizo mbili wakiendelea kuwasikiana kama Kawaida na zote zilikuwa zinaonana zikipaa juu zaidi wanaonana ila wakafika mahali Ile ya Raisi wakawa hawaioni sababu iliingia kwenye ukungu mzito Kwa rubani kugoma kutii kupaa elevation ya juu zaidi na akawa kazima transponder wakati njia yote Walikuwa na mawasiliano helikopta zote
 
Mmejuaje hayo yote ilihali walifariki wote?
Ndege na hata helicopter muhimu huwa zinarekodi mazungumzo na actions zote za marubani kwenye safari. Sehemu alikopaa juu zaidi, pataonekana, mijadala iliyokuwepo itasikilizwa, kama aliwasha taa au kupiga kona kali, kiwango cha mafuta, kasi ya upepo angani, unyevu, n.k.

Bado helicopter mbili kwenye msafara zilifika na walihojiwa. Hamna kigumu kujulikana hapo
 
Ningependa kujua hivi jeshini Amri hutoka juu tu au inaweza kutoka kwa mtu alie chini yako???
Rubani wa mbele wa helikopta cheo kidogo aliona Hali ya hewa mbaya mbele hakutoa amri alishauri tu kuwa mbele hakuko Vizuri helikopta za nyuma ya katikati ya Raisi na ya walinzi wa nyuma zipae juu zaidi

Ushauri waweza zingatiwa au kukataliwa ukitolewa na mtu cheo kidogo

Rubani wa helikopta ya Raisi mwenye cheo kikubwa akaamua kukataa ushauri wa askari pilot mwenye cheo kidogo kuliko yeye hakumpa amri alitoa ushauri
 
Back
Top Bottom