Rubani huyu anastahili pongezi

Ichwampaka

Senior Member
Nov 19, 2018
135
109
Habari hii haikuandikwa na vyombo vingi vya Habari. Mwezi March mwaka huu (2021) Kulikuwa na ndege aina ya Airbus A380-800, ilikuwa inasafiri kutoka Tanzania kwenda Tanzania Mpya . Ndege hii ilikuwa na rubani mkuu na Rubani msaidizi . Ilijaa abiria waliokuwa na matumaini makubwa ya kufika waendako, maana katika safari hii rubani aliwahakikishia abiria kuwa wakifika Tanzania Mpya shida zao zote zitakuwa zimeisha kabisa, na watakuwa wakitembea vifua mbele.

Marubani hao hasa rubani mkuu alijaa ushujaa na matumaini, kiasi kwamba, abiria walikuwa hawana wasiwasi wowote kuhusu safari hiyo. Na walikuwa na uhakika wa kufika hiyo safari yao. Lakini, wakiwa angani rubani mkuu akapata hitilafu ya kiafya, kiasi cha kutoweza kumudu kuendesha hiyo ndege.

Kulikuwa mtafaruku mkubwa sana wa abiria, hawakujua wafanye nini, na wengi walijua ndio mwisho wa maisha yao na hata yale maisha mazuri waliyoahidiwa kule hayakuwa na maana tena, suala lilikuwa ni uhai wao.

Na kwa vile rubani mkuu alikuwa sio mtu wa kuchukua likizo, au kwenda mapumzikoni ; wakati wote alikuwa anaendesha hii ndege, abiria wengi ndani ya ndege hata ndugu zao waliokuwa katika nchi ya Tanzania , walijua huyu rubani msaidizi hataweza kupokea usukani na kuishusha ndege salama.

Tetesi eti baadhi ya crew members na abiria wakajaribu kuomba msaada kutoka ardhini kama inawezekana kumleta rubani toka chini aletwe na ndege kisha isogelee hii Airbus halafu rubani asokomezwe kupitia dirishani aingie kuendesha hii ndege.

Nasikia wataalamu wengine wakasema haiwezekani, maadamu huyu rubani msaidizi yupo, yeye ndiye mwenye jukumu la kupokea usukani. Muda wote huu wa tafrani huyu rubani msaidizi alikuwa yupo bize akihangaikia uhai wa rubani mkuu, wala hakujishughulisha na hii kadhia akili yake ilikuwa namna ya kumuokoa rubani mkuu na bosi wake mambo ya kuwa anatakiwa Kuchukua nafasi ya rubani mkuu hayakuwepo kichwani mwake wala haikuwa kipaumbele chake.

Baada ya kuona rubani mkuu ametwaliwa na Mungu, rubani msaidizi akarudi kutoka kwenye cockpit na kuwatangazia abiria kuwa rubani mkuu ameshatwaliwa, huku akifuta machozi ya uchungu, akijitia nguvu na moyo kwa usaidizi wa Mungu AKATANGAZA kuwa yeye kama rubani msaidizi hana wasi wasi atashika usukani na ndege itafika Tanzania Mpya salama na yale maisha waliyoaihidi yatafikiwa bila shida.

Wale abiria walipigwa na butwaa kwa ujasiri na utulivu wa rubani msaidizi alivyokuwa anaelezea hili jambo. Wote walinyamaza kimya, hakuna hata aliyekuwa anapiga tena kelele. Rubani msaidizi akarudi kwenye cockpit ghafla ndege iliyokuwa inacheza cheza na kuyumba yumba ikaanza kupata utulivu. Ndege ikachukua momentum ikatulia angani safi kabisa, abiria wengi wakapiga makelele ya shangwe kumshangilia rubani mpya, ghafla kwenye spika ikatoka sauti ya rubani kuwa tupo kwenye maombolezo ya rubani mkuu. Abiria wakatulia na wengine kushika rozali kumuombea rubani mkuu.

Kwa kuwa ilikuwa ni sheria ndege kuendeshwa na rubani mkuu mwenye sifa za zaidi, utaratibu ukafanyika mamlaka za ndege, anga nk wakampa rubani msaidizi cheo na wadhifa kamili wa rubani mkuu akiwa huko huko angani, na kwa unyenyekevu mkubwa akakipokea bila mbwembwe wala kudemka.

Rubani mkuu akawatangazia abiria kuwa destination ya safari anaifahamu fika kwasababu yeye alishiriki kuiandaa na kuipanga, ile baadhi ya coordinates za kutufikisha huko atazibadilisha kidogo ili safari iwe nyepesi na ikiwezekana tufike haraka. Kwa hiyo njia ndege itakayopita sasa inawezekana isiwe sawia na ile iliyotangazwa na rubani mkuu wa kwanza aliyetwaliwa na Mungu.

Pia akatangaza kubadilisha crew wengine, ili kuendana na njia mpya, ila hakuna aliowafukuza kutoka kwenye ndege. Wengine walipumzishwa, na wengine wakahamishiwa sehemu zingine lakini ndani ya ndege. Hivi sasa ndege imetulia inaenda vizuri na abiria wamefurahia rubani mpya anavyoendesha ndege yao. Japo baadhi ya abiria imekuwa ngumu kuamini kuwa rubani wa mwanzo ameshatwaliwa na sasa yupo rubani mwingine. Hili ni suala la muda tu, baadaye watazoea.

Mimi nadhani katika haya tumpongeze sana huyu aliyekuwa rubani msaidizi, kitendo cha kupokea usukani wa ndege, na kufanikiwa kutuliza abiria na ile taharuki, wasiwasi na sintofahamu ni jambo KUBWA SANA SANA. Kama ameweza kutuliza ndege, na abiria na crew wenyewe wamekubali, nina uhakika mambo mengine atayamudu kwa kiwango cha hali ya juu. Tuendelee kumuombea, kumpa sapoti na tuache kumpa maneno ya kumkatisha tamaa, lugha mbaya, majina mabaya na kubeza kila anachokifanya.

Tukiendelea hivi hata Mungu atachukia maana tutakuwa ni watu tusio ridhika, tunataka kila kitu kiwe kama tunavyotaka sisi. Basi kama tunataka kila kitu kiwe kama tunavyotaka sisi, basi na sisi tukautafute huo URUBANI ili tutende tunavyoona siye
 
Hivi wewe hata kwa macho tu umewahi kuiona Airbus A380- 800 series?

Acha kufananisha hii ndege na mamifano yako yasiyo na kichwa wala miguu.

Eti abiria wakashikwa na butwaa wasijue la kufanya, kukawa na mtafaruku mkubwa wa abiria, chaaaaaaaa! We unaota wewe
 
ah, sasa fasihi gani isiyofikirisha hii?!!! yaani mstari wa tatu au nne tu tayari umeshajua mwandishi anaelekea wapi, si bora ungeandika kawaida tu
 
^Nchi inayoongozwa kwa kutegemea tu fikra, falsafa, sera, mitazamo na matamko kutoka London & Washington, bila kupanga na kujiwekea falsafa yake na mikakati ya kujitegemea yenyewe, hakika kabisa, haielekei kokote^ ~ JKN.
 
Ni SHERIA TU KUWE NA CAPT NA F/O
ELSE WOTE WANANYANYUA NDEGW NA KUISHUSHA
 
Habari hii haikuandikwa na vyombo vingi vya Habari. Mwezi March mwaka huu (2021) Kulikuwa na ndege aina ya Airbus A380-800, ilikuwa inasafiri kutoka Tanzania kwenda Tanzania Mpya . Ndege hii ilikuwa na rubani mkuu na Rubani msaidizi . Ilijaa abiria waliokuwa na matumaini makubwa ya kufika waendako, maana katika safari hii rubani aliwahakikishia abiria kuwa wakifika Tanzania Mpya shida zao zote zitakuwa zimeisha kabisa, na watakuwa wakitembea vifua mbele.

Marubani hao hasa rubani mkuu alijaa ushujaa na matumaini, kiasi kwamba, abiria walikuwa hawana wasiwasi wowote kuhusu safari hiyo. Na walikuwa na uhakika wa kufika hiyo safari yao. Lakini, wakiwa angani rubani mkuu akapata hitilafu ya kiafya, kiasi cha kutoweza kumudu kuendesha hiyo ndege.

Kulikuwa mtafaruku mkubwa sana wa abiria, hawakujua wafanye nini, na wengi walijua ndio mwisho wa maisha yao na hata yale maisha mazuri waliyoahidiwa kule hayakuwa na maana tena, suala lilikuwa ni uhai wao.

Na kwa vile rubani mkuu alikuwa sio mtu wa kuchukua likizo, au kwenda mapumzikoni ; wakati wote alikuwa anaendesha hii ndege, abiria wengi ndani ya ndege hata ndugu zao waliokuwa katika nchi ya Tanzania , walijua huyu rubani msaidizi hataweza kupokea usukani na kuishusha ndege salama.

Tetesi eti baadhi ya crew members na abiria wakajaribu kuomba msaada kutoka ardhini kama inawezekana kumleta rubani toka chini aletwe na ndege kisha isogelee hii Airbus halafu rubani asokomezwe kupitia dirishani aingie kuendesha hii ndege.

Nasikia wataalamu wengine wakasema haiwezekani, maadamu huyu rubani msaidizi yupo, yeye ndiye mwenye jukumu la kupokea usukani. Muda wote huu wa tafrani huyu rubani msaidizi alikuwa yupo bize akihangaikia uhai wa rubani mkuu, wala hakujishughulisha na hii kadhia akili yake ilikuwa namna ya kumuokoa rubani mkuu na bosi wake mambo ya kuwa anatakiwa Kuchukua nafasi ya rubani mkuu hayakuwepo kichwani mwake wala haikuwa kipaumbele chake.

Baada ya kuona rubani mkuu ametwaliwa na Mungu, rubani msaidizi akarudi kutoka kwenye cockpit na kuwatangazia abiria kuwa rubani mkuu ameshatwaliwa, huku akifuta machozi ya uchungu, akijitia nguvu na moyo kwa usaidizi wa Mungu AKATANGAZA kuwa yeye kama rubani msaidizi hana wasi wasi atashika usukani na ndege itafika Tanzania Mpya salama na yale maisha waliyoaihidi yatafikiwa bila shida.

Wale abiria walipigwa na butwaa kwa ujasiri na utulivu wa rubani msaidizi alivyokuwa anaelezea hili jambo. Wote walinyamaza kimya, hakuna hata aliyekuwa anapiga tena kelele. Rubani msaidizi akarudi kwenye cockpit ghafla ndege iliyokuwa inacheza cheza na kuyumba yumba ikaanza kupata utulivu. Ndege ikachukua momentum ikatulia angani safi kabisa, abiria wengi wakapiga makelele ya shangwe kumshangilia rubani mpya, ghafla kwenye spika ikatoka sauti ya rubani kuwa tupo kwenye maombolezo ya rubani mkuu. Abiria wakatulia na wengine kushika rozali kumuombea rubani mkuu.

Kwa kuwa ilikuwa ni sheria ndege kuendeshwa na rubani mkuu mwenye sifa za zaidi, utaratibu ukafanyika mamlaka za ndege, anga nk wakampa rubani msaidizi cheo na wadhifa kamili wa rubani mkuu akiwa huko huko angani, na kwa unyenyekevu mkubwa akakipokea bila mbwembwe wala kudemka.

Rubani mkuu akawatangazia abiria kuwa destination ya safari anaifahamu fika kwasababu yeye alishiriki kuiandaa na kuipanga, ile baadhi ya coordinates za kutufikisha huko atazibadilisha kidogo ili safari iwe nyepesi na ikiwezekana tufike haraka. Kwa hiyo njia ndege itakayopita sasa inawezekana isiwe sawia na ile iliyotangazwa na rubani mkuu wa kwanza aliyetwaliwa na Mungu.

Pia akatangaza kubadilisha crew wengine, ili kuendana na njia mpya, ila hakuna aliowafukuza kutoka kwenye ndege. Wengine walipumzishwa, na wengine wakahamishiwa sehemu zingine lakini ndani ya ndege. Hivi sasa ndege imetulia inaenda vizuri na abiria wamefurahia rubani mpya anavyoendesha ndege yao. Japo baadhi ya abiria imekuwa ngumu kuamini kuwa rubani wa mwanzo ameshatwaliwa na sasa yupo rubani mwingine. Hili ni suala la muda tu, baadaye watazoea.

Mimi nadhani katika haya tumpongeze sana huyu aliyekuwa rubani msaidizi, kitendo cha kupokea usukani wa ndege, na kufanikiwa kutuliza abiria na ile taharuki, wasiwasi na sintofahamu ni jambo KUBWA SANA SANA. Kama ameweza kutuliza ndege, na abiria na crew wenyewe wamekubali, nina uhakika mambo mengine atayamudu kwa kiwango cha hali ya juu. Tuendelee kumuombea, kumpa sapoti na tuache kumpa maneno ya kumkatisha tamaa, lugha mbaya, majina mabaya na kubeza kila anachokifanya.

Tukiendelea hivi hata Mungu atachukia maana tutakuwa ni watu tusio ridhika, tunataka kila kitu kiwe kama tunavyotaka sisi. Basi kama tunataka kila kitu kiwe kama tunavyotaka sisi, basi na sisi tukautafute huo URUBANI ili tutende tunavyoona siye
ulijuaje kama alikuwa bize kuokoa maisha ya boss wake na sio kuyaangamiza kabisa?

kwa namna anavyoendesha ni wazi hakuwa na nia njema kwa boss wake
 
Daaah naona rubani amedhibiti ndege barabara......marubani wakongwe walijaribu kuitikisa lakini kawaonyesha umakini wake mkubwa sana. Hongera sana rubani
 
Miaka miwili baadaye wengi wanakubali kuwa rubani ameimuda ndege na umahiri wake unaanza kupita hata viwango vile............................................maana hata upande wa pili wamekubali
 
Ndege inaenda vizuri sana; changamoto ni za kawaida kabisa. Hongera rubani mkuu. Usiogope wapingaji na wanye maneno ya kubeza hata wakiwa wao marubani, watajibeza wenyewe maana hiyo ni hulka.
 
Back
Top Bottom