Rubani auchapa usingizi ndani ya ndege

Huu usafiri natumia kwa sababu tu nakuwa sina namna, ila mimi sijawahi kabisa kuizoea ndege, ningekuwa mimi humo nafikiri hali yangu ingekuwa mbaya mno

Na ndio maana kabla ya kuruka tahadhari hutolewa ki utu uzima. Ila ni usafiri salama kuliko yote.
 
Hakuna ndege inayobeba abiria ikiwa na rubani mwanafunzi.Huyo ni co-pilot ambaye nayeye ni rubani certified sema ana masaa machache..

Hawa wapakistan nao ni ushamba unawasumbua ndege ikishafika cruising altitude wanaweka autopilot kila rubani na kitanda chake wanadozi
 
hiyo ni ajali ya ndege ya Aeroflot Flight 593 ikitokea moscow kwenda hong kong ambapo rubani aliwaalika watoto wake waje cockpit ili waone jinsi ndege inavyoendeshwa. both first officer na mwenzake walikuwa wazembe kuruhusu hali hiyo kutokea. unfortunately wote waliangamia.
 
Kumbe hata kwenye ndege wanaachiana deiwaka
 
Islamabad to london ni parefu sana so ni obvious aliiweka ndege ktk auto pilot na huyu mwanafunzi ni mwanafunzi kwa jina tu ila atakuwa vizuri kabisa!
 
Nauliza hivi hizi bajaji/pangaboi(bomberdia) zetu zina hiyo auto-piloting?
 
Habari nyengine zinavotiwa chumvi! Rubai mwanafunzi kaachiwa arushe ndege? Tangu lini mwanafunzi akaachiwa arushe ndege yenye abiria ndani? Hao abiria walijuaje kama huyo mwanafunzi? Halafu pilot kulala ni kawaida mbona huku akimuachia first officer aenselee na kazi. Hili gazeti limekosa habari nini?
 
we acha umbea 305 pipa la watu hao halipushiwi na watu wawili kwa Cabin kuna watu kama watatu mpaka watano
wanakuwa katika majukumu mbalimbali na ranks tofauti. nadhani mtoa maada alikuwa anazungumzia replacement ya captain
 
Hyo ya dege kubwa hvo kuwa na marubani wawil tu nalo geni masikioni mwangu.. hata ikitokea ameenda chooni lazima abaki mtu wa kusoma alert system, na inategemea huyu mwanafunzi ni wa level gan, Kama ni junior au sinior trainee
 
Huu usafiri natumia kwa sababu tu nakuwa sina namna, ila mimi sijawahi kabisa kuizoea ndege, ningekuwa mimi humo nafikiri hali yangu ingekuwa mbaya mno
Aiseee!! Kumbe tuko wengi

Nkipandaga huo usafir na meli
Hua naanza kutubu thambi zang
Mapemaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…