RPC wa Mkoa wa Simiyu aamrisha Mkurugenzi wa Meatu kumtangaza mgombea wa CHADEMA mshindi

Wasukuma naona taratiibu wanaamka, bado wanyamwezi na wagogo, hawa bado wapo kwenye usingizi wa pono!

Hizi kauli za kuhisi wasukuma walikuwa wamelalaa si sahihi mkuu. Nakumbuka uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995, John Cheyo alishinda ubunge huko bariadi mkoani shinyanga wakati huo, wakati huohuo mkio mnayofikiri imeamka kama arusha na mbeya hawakuwa na mbunge hata mmoja wa upinzani. Na bado mpaka leo wasukuma hawa wana wabunge wengi zaidi wa upinzani kuliko sehemu nyingine yoyote Tanzania bara.
 
Viashiria vyote vinaonesha kwamba ubabe wa ccm ndio utakaoleta machafuko hapa nchini.
Mkuu umenena aisee maana wao ndio wanalianzisha alafu mkipaniki mnaambiwa mnahatarisha amani, kumbe msababishi ni yule anaewanyooshea wenzake mkono kwamba wanavunja amani
 
Wasukuma naona taratiibu wanaamka, bado wanyamwezi na wagogo, hawa bado wapo kwenye usingizi wa pono!
Mkuu hawa walishaamka siku nyingi, tatizo wapo wengi inapotokea wachache wanaokuja mjini wakafanya blunder inaonekana kama wapo nyuma lakini ukweli hawapo hivyo
 
Hizi kauli za kuhisi wasukuma walikuwa wamelalaa si sahihi mkuu. Nakumbuka uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995, John Cheyo alishinda ubunge huko bariadi mkoani shinyanga wakati huo, wakati huohuo mkio mnayofikiri imeamka kama arusha na mbeya hawakuwa na mbunge hata mmoja wa upinzani. Na bado mpaka leo wasukuma hawa wana wabunge wengi zaidi wa upinzani kuliko sehemu nyingine yoyote Tanzania bara.

mkuu hizi kauli zimetundikwa zikinikera sana hawa Watu wanadharau sana wasukuma.Wasukuma wapeni heshima bana mbona hivyo.Mageuzi Tanzania yameanzishwa na wasukuma wengi tofauti Na Watu wanavyodhani, mwaka 1992 Wakati vyama vingi vinaanza viongozi waanzilishi wa vyama walikuwa wasukuma na wachaga

Mwenyekiti wa Cdm-mtei
Katibu Mkuu wa Cdm-Bob Nyanga makani-msukuma
mwenyekiti wa UDP-John Mamose cheyo-msukuma
Katbu mkuu wa Udp-baba yake Lau MAsha-msukuma
Mwenyekiti wa CUF bara-James mapalala-mnyamwezi/sukuma
Katibu Mkuu CUF -misobi mageni

Leo Watu wanakuja kusema eti wasukuma wameamka.uzushi mtupu.

kule bariadi mashariki tangu 1995 ni Udp hadi kesho.Bariadi magharibi tangu 1995-2005 UDP
acheni dharau toeni salute kwa kina ngosha wale ni wanamageuzi
 
kufanya mbadiliko ya dhati nguvu ya Umma ni msingi wa Mabadiliko...Mimi naomba hawa wapinzani wajipange kupiga siasa safi...waepuke uchafu/najisi/corruption/ngono/na kila aina ya sifa mbaya! Matumiza mazuri ya fedha, ruzuku yyte inayopatikana huku juu iende kujenga chama kwa ngazi ya chini ambapo wenzetu wameweka mizizi..salam sana
 
Jamaa hivi hujawahi kisikia msemo unaosema mdomo uliponza kichwa kikakatwa.Humu tunschangia tukiwa wengi na wengine wanataka sifa waonekane wanajazba sana.Ila huyo uliyemtukana akikuchukulia hatua ujue utaenda peke yako sisi utatucha tunacoment tu.Jitahidi kuzuia mihemko na jazba.Kiukweli unastahili uwe ndani pale kituoni japo siku moja tu uuze duka la polisi kwa kosa la kushambulia kwa maneno makali na yakuudhi.
 
Hakuna kabila la Wanyantuzu, wote hao ni Wasukuma sasa neno Ntuzu ni jina la sehemu tu ambalo wakazi wake ni Wasukuma! Ntuzu ni moja ya tarafa katika wilaya ya Bariadi. Wasukuma ndo kabila lililokuwa linawaneemesha maccm, safari hii watajibeba!! Zimwi limekata kamba sijui wataponea wapi! Big up kata yangu Mwabusalu nimewakubali!
wasukuma wanapatika sukuma, wanyantuzu wao wako kiya. hivo sio kweli kuwa wanyantuzu ni sehemu ya wasukuma.
 
Hiyo ni Kampeni tosha dhidi ya CCM. Hata wale asiopenda Chadema wanalazimika kukipenda kwa nguvu zote!

huyu mgombea anayo haki ya kukata rufaa sio kazi ya polisi kutangaza matokeo ya uchaguzi.
 
Hizi kauli za kuhisi wasukuma walikuwa wamelalaa si sahihi mkuu. Nakumbuka uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995, John Cheyo alishinda ubunge huko bariadi mkoani shinyanga wakati huo, wakati huohuo mkio mnayofikiri imeamka kama arusha na mbeya hawakuwa na mbunge hata mmoja wa upinzani. Na bado mpaka leo wasukuma hawa wana wabunge wengi zaidi wa upinzani kuliko sehemu nyingine yoyote Tanzania bara.

ilikuwa wilaya ya magu kabla hajakimbilia bariadi wakati huo dr.slaa alikuwa bado ccm. mwaka 1975 nyerere alipata kura za hapana 98% akapindua zikawa za ndiyo mwaka 1977 akaifuta tanu na kuwaleta wazanzibar wa asp ndo ikawa mwanzo wa ccm
 
Back
Top Bottom