RPC wa Mkoa wa Simiyu aamrisha Mkurugenzi wa Meatu kumtangaza mgombea wa CHADEMA mshindi

na machafuko ya nchi hii yataanzishwa na hao hao wanaodhani kwamba hii nchi wana hatimiliki nayo someni nyakati, tumewachoka
 
Msukuma ni Mnyamwezi pia. JITAMBUE. Sema Wadakama waamke, hapo tutaelewana. Sukuma ni Kaskazini na Dakama ni Kusini. Mtu anayetoka upande wa Sukuma/Dakama anakuwa M-Sukuma/Dakama.

Wasukuma naona taratiibu wanaamka, bado wanyamwezi na wagogo, hawa bado wapo kwenye usingizi wa pono!
 
TAARIFA YA MAAZIMIO YA CHADEMA KWA
VYOMBO VYA HABARI
LEO.

Baadhi ya maazimio ya CHADEMA kuhusu uchaguzi
serikali za mitaa
kama yalivyosomwa na Dr. Slaa
alipozungumza na
waandishi wa Habari.

¤ Suala la kupita bila kupingwa ni kinyume na
Demokrasia na haki
ya msingi ya raia ya kuchagua, hivyo utamaduni
huu ufe nakama
ikitokea basi zipigwe KURA za NDIO na HAPANA.

¤ Viongozi wa CHADEMA waliochaguliwa ikigokea
wanatuhumiwa
kwa vitendo vya rushwa kamwe chama
hakitawavumilia viongozi
hao na tutawachukulia hatua maramoja bila kusita
ikiwemo za ndani
ya chama na hata kuwashtaki mahakamani.

¤ Kamati kuu imezitaka mamlaka zinazohusika
kuwatambua
mabalozi wa CHADEMA katika masuala yote
ambayo yanahitaji wa
ngazi hiyo, ikiwemo utambulisho wa ukazi.
Wanachama wa
CHADEMA hawalazimiki kwenda kupata idhini ya
mabalozi
wanaotokana na CCM kama ambavyo serikali
inataka.

KUHUSU MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2015.

Kamati Kuu ya Chama imepokea kwa masikitiko
taarifa
zinazoonesha kuwa hadi sasa serikali kupitia Tume
ya Taifa ya
Uchaguzi haionekani kujipanga kuweza kufanikisha
uchaguzi mkuu
ujao.

Tayari kasoro nyingi ambazo kama hazitafanyiwa
kazi zitasababisha
vurugu huko tuendako zimeanza kuonekana kwenye
zoezi la
majaribio ya uandikishaji wapiga kura linaloendelea
hadi sasa
Kawe,Kilombero, na Mlele.

Akizungumzia vurugu na vifo na kasoro
zilizojitokeza katika
uchaguzi huo, Dr. Slaa amewalaumu Waziri mkuu
Mh. Pinda na
Waziri wa TAMISEMI Mh. Hawa Ghasia kuwa ndio
chanzo cha
matukio yote katika uchaguzi huo. Hasa kwa
kutunga kwao kanuni
mbovu na miongozo katika sheria ya uchaguzi
Serikali za mitaa
kanuni ambazo zimepelekea mauji katika baadhi ya
maeneo nchoni
hasa kule Nzega kutokea. Hivyo wote hawa
wanapaswa kujiuzulu
wenyewe ama wawajibishwe na Mh. Raisi mara
moja.

Akiyataja maeneo ya Miji midogo ambayo
CHADEMA imeshinda, Dr.
Slaa amesema:

"1. Nkasi - Namanyere
2. Hai - Bomang'ombe.
3.Karatu - Karatu.
4. Arumeru Mashariki - Usa river.
5.Vunjo - Ukawa.
6. Mbeya vijijini - Mbalizi.
7. Mbozi Maghari - Tunduma.
8. Mbozi Mashariki - Mlowo.
9. Kyela - Kyela.
10. Lupa - Makongorosi.
11. Busanda - Katoro.
12. Geita - Geita.
13. Chato - Chato.
14. Kwimba - Ngudu.
15. Karagwe - Kayanga.
16. Bukombe - Ushirombo.
17. Sengerema - Sengerema.
18. Tarime - Tarime.
19. Tarime - Sirari mji mdogo.
20. Rorya - Shirati ( 7/2).
21. Bunda - Bunda.
22. Serengeti - Mugumu 10/10 ( CUF 3).
23. Kahama - Kahama.
24. Bariadi - Bariadi ( 49/43).
25. Kilombero - Ifakara.
26. Magu - Magu.
27. Mbozi - Vwawa.

Sehemu zote hizo CCM ndio chama cha upinzani.
 
wasukuma wanapatika sukuma, wanyantuzu wao wako kiya. hivo sio kweli kuwa wanyantuzu ni sehemu ya wasukuma.
Naona dogo hujui maana ya Kiya na Sukuma!

Sukuma kwa maana halisi ni Kaskazini, Kiya ni Mashariki, Dakama ni Kusini na Ng'weli ni Magharibi. Hivyo hao unaowaita Wanyantuzu ni sehemu ya Wasukuma walioamua kubaki na kuishi huko Mashariki! Hiyo ni sawa na kusema eti Mmachame siyo Mchagga, au Watu wa Usangi kwamba siyo Wapare!!
 
Miaka yote wamekuwa wakitumia nguvu nyingi kukandamiza haki sasa wananchi walio na kipato kidogo wameamka ma kudai haki kwa nguvu.

People's power
 
mkuu hizi kauli zimetundikwa zikinikera sana hawa Watu wanadharau sana wasukuma.Wasukuma wapeni heshima bana mbona hivyo.Mageuzi Tanzania yameanzishwa na wasukuma wengi tofauti Na Watu wanavyodhani, mwaka 1992 Wakati vyama vingi vinaanza viongozi waanzilishi wa vyama walikuwa wasukuma na wachaga

Mwenyekiti wa Cdm-mtei
Katibu Mkuu wa Cdm-Bob Nyanga makani-msukuma
mwenyekiti wa UDP-John Mamose cheyo-msukuma
Katbu mkuu wa Udp-baba yake Lau MAsha-msukuma
Mwenyekiti wa CUF bara-James mapalala-mnyamwezi/sukuma
Katibu Mkuu CUF -misobi mageni

Leo Watu wanakuja kusema eti wasukuma wameamka.uzushi mtupu.

kule bariadi mashariki tangu 1995 ni Udp hadi kesho.Bariadi magharibi tangu 1995-2005 UDP
acheni dharau toeni salute kwa kina ngosha wale ni wanamageuzi

Ahsante mkuu kwa kuweka historia sawa ili heshima irudi, ili na hao wanaofikiri wameamka, waamke sasa, LEKAGI GETE E TUJA.
 
Huyo RPC alikuwa aongezee kwa kuwafuta kazi hao mapoliccm walioburuzwa kwend kubandika matokeo ya uwongo.Na halafu akawahoji walipewa kiasi gani kisha hela azichukue yeye ,eei mambo kuzidiana eti !
 
Hizi kauli za kuhisi wasukuma walikuwa wamelalaa si sahihi mkuu. Nakumbuka uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995, John Cheyo alishinda ubunge huko bariadi mkoani shinyanga wakati huo, wakati huohuo mkio mnayofikiri imeamka kama arusha na mbeya hawakuwa na mbunge hata mmoja wa upinzani. Na bado mpaka leo wasukuma hawa wana wabunge wengi zaidi wa upinzani kuliko sehemu nyingine yoyote Tanzania bara.
Hapana kwa mbeya umekosea mwaka 1995 Mbeya mjini walishinda NCCR.
 
Back
Top Bottom