RPC Geita: Ofisi za Kata sio Kituo cha Polisi

RPC Geita: Ofisi za Kata sio Kituo cha Polisi

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,281
Reaction score
7,703
Jeshi la polisi mkoa wa Geita limepiga marufuku watendaji kuanzisha vituo vya polisi katika ofisi za kata bila kuwa na vibali kutoka serikalini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamshna Msaidizi Mwandamizi Safia Jongo ameyasema hayo jana wakati wa muendelezo wa semina ya polisi jamii pamoja na watendaji wa kata wa mkoa wa Geita iliyoratibiwa na mgodi wa dhahabu wa GGML.

Kamanda Jongo alisema kuwa ili kiwe kituo cha polisi ni lazima kikidhi vigezo ambavyo vinaweza kulaza mahabusu na sio katika ofisi za kata.

Aidha katika hatua nyingine kamanda Jongo amekemea tabia ya polisi jamii kujifanya polisi kamili na kuchukua sheria mkononi kitu ambacho hata askari kamili haruhusiwi kufanya.

Jongo aliongeza kuwa semina hii itawawezesha watendaji pamoja na polisi jamii hawa kwenda kutoa huduma kulingana na misingi waliyoipata katika mafunzo.

Sambamba na hilo jeshi la polisi limetoa onyo kwa wazazi ambao wanatabia ya kuweka picha za watoto wadogo mitandaoni kwamba suala hilo linatafsiriwa kama ukatili wa kijinsia kwani wao hawajaridhia kufanya hivyo.

Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la polisi dawati la jinsi Wilfred Willa alisema kuwa kuweka picha mtandaoni bila ridhaa ya mtoto ni unyanyasaji wa kijinsia ambapo mzazi atakuwa na kesi ya kujibu endapo mtoto atashtaki hapo baadae.
 
Back
Top Bottom