DOKEZO RPC Arusha, tatua hii kero ya kuomba hela inayoshamiri kwa Trafiki

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Jun 30, 2013
10
19
RPC Arusha tunaomba ingilia hili suala la traffic Police Arusha wamekuwa ni kero kusimamisha magari na kuomba hela.

Inakuwa kama hela ni haki yao uwe na kosa ama huna kosa. Arusha ni mji mdogo unaweza simamishwa mara tatu katika safari moja kila kona traffic wapo na wote wataomba hela.

Hii ni kero

=======

Baadhi ya maeneo yenye changamoto hii ni:

Barabara ya Moshi Arusha
Barabara ya Monduli maeneo ya Shamsi
Barabara ya Njiro Maeneo ya Fire
Barabara ya Ngaramtoni
Maeneo ya Laska Zone

Soma Arusha: Kero ya Rushwa ya Mdau yamfikia RPC; aapa kutowaonea haya Trafiki wala Rushwa. Je, kauli za maapizo zinatosha?
 
RPC Arusha tunaomba ingilia hili suala la traffic Police Arusha wamekuwa ni kero kusimamisha magari na kuomba hela.

Inakuwa kama hela ni haki yao uwe na kosa ama huna kosa. Arusha ni mji mdogo unaweza simamishawa mara tatu katika safari moja kila kona traffic wapo na wote wataomba hela.

Hii ni kero
Kuna pumbavu Moja leo alikosa cha kucharge,japo alitaka rushwa.Tulitukana sana
 
RPC Arusha tunaomba ingilia hili suala la traffic Police Arusha wamekuwa ni kero kusimamisha magari na kuomba hela.

Inakuwa kama hela ni haki yao uwe na kosa ama huna kosa. Arusha ni mji mdogo unaweza simamishawa mara tatu katika safari moja kila kona traffic wapo na wote wataomba hela.

Hii ni kero
Kuna kikosi cha yule mama mwenye matege wanakua na nissan,yan unaweza kutana nao hata saa 12 asubuhi sijui wanalala kwenye gari....pia kuna mubi traffic na kikosi chake nao ni fujo na tochi yao kuvizia watu
 
HAhahaha. Ni hatariiii. Na nissan lao bovuuuuuuu.... alafu wanatuambia sisi magari yetu mabovu. Wakati lao la kutupa kabisa skrepa.... muba na tochi lake msumbufu kweli. Ila tochi imebaki moja kwa mkoani na ingine usa... ukishaikuta labda bypass, basi ujue kule moshi - arusha roaf kweupeeeee and vice versa
 
Yaani mji wa Arusha kwa wingi wa traffic utasema nchi ipo kwenye emergency state..

Mbaya zaidi hao traffic hawana AIBU kabisa, wanaweza kukukomalia eti hujalipa BIMA, wakati ni uongo..yaani wengi wao, ni watu wa AJABU kabisa
 
Kuna kikosi cha yule mama mwenye matege wanakua na nissan,yan unaweza kutana nao hata saa 12 asubuhi sijui wanalala kwenye gari....pia kuna mubi traffic na kikosi chake nao ni fujo na tochi yao kuvizia watu
Hahaha naona umewagusa watu wangu😂😂😂
Huyo mama msambaa mwenye matege ninamheshimu mnoo, aliwahi kuamulia ugomvi mbaya sana kati yangu na yule mrangi mshika torch wa kikosi cha Muba kale kajamaa kembaa kofia kubwa kuliko kichwa.

Ilikuwa siku mbaya sana kwangu...hasira nilizokuwa nazo hazikuwa afya zingeniletea matizo makubwa...huyo mama alisaidia sana na hadi leo ni rafiki yangu sana😂

Yes, traffic Arusha ni tatizo kubwa sana but mkielewana pia utajiachia kwa raha zako.
 
Dawa ya kuepuka rushwa za askari wa usalama barabarani ni kukubali kulipa faini kwa kosa ulilokutwa nalo.
 
Hii ni kweli kabisa, imetutokea jana

Wanasimamisha gari na kukutafutia kosa lengo lao uwape rushwa
 
RPC Arusha tunaomba ingilia hili suala la traffic Police Arusha wamekuwa ni kero kusimamisha magari na kuomba hela.

Inakuwa kama hela ni haki yao uwe na kosa ama huna kosa. Arusha ni mji mdogo unaweza simamishwa mara tatu katika safari moja kila kona traffic wapo na wote wataomba hela.

Hii ni kero

=======

Baadhi ya maeneo yenye changamoto hii ni:

Barabara ya Moshi Arusha
Barabara ya Monduli maeneo ya Shamsi
Barabara ya Njiro Maeneo ya Fire
Barabara ya Ngaramtoni
Maeneo ya Laska Zone
Hata barabara ya namanga kila trufic ni kuomba hela tu mapaka unafika namanga.
 
Kama umeombwa unalalamika nini, tafuteni hela jamani unaweza kuta hela yenyewe unayoombwa ni laki 1 tu
 
Back
Top Bottom