Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 222
- 529
Nelson Mandela alifungwa gerezani kwa miaka mingi kutetea haki za Waafrika wa Afrika ya Kusini na waliomtesa gerezani wakawa wamemuongezea ujasiri na kuipa nguvu jamii ya Afrika kusini kujitetea na mateso ya Mandela yakaleta baraka Afrika Kusini
Mwimbaji wa wimbo wa "wanatuona nyani" aliyekamatwa na kuwekwa ndani na RPC wa Mbeya huenda akawa chachu ya viongozi wa sanaa na utamaduni kuanza kufuatilia tungo za wasanii wa kizazi kipya ambazo zimejaa matusi na kuhamasisha ngono tu ambazo watoto wadogo walioko shule ndio wanazipenda na viongozi wanawapa majukwaa makubwa na kuwashangilia bila kujua namna wasanii hao wanavyoharibu utamaduni na maadili ya watanzania
ukifuatilia comments nyingi za wachangiaji mitandaoni kuhusu sakata hilo, wengi wanaikosoa serikali kuacha nyimbo za matusi zitambe na kuzipa majukwaa huku nyimbo zinazowakemea viongozi na kutetea jamii zinafungiwa na waimbaji kukamatwa
Kama jamii hatuna budi kukemea jambo hili kwa kuweka wazi mashairi ya wasanii wa kizazi kipya yanayoharibu maadili ya vijana wetu na kuhamasisha ngono kiasi cha kuifanya kuonekana kitu cha kawaida sana hata kwa watoto wadogo kitu ambacho zamani hakikuwepo
RPC aliyeamuru akamatwe ametusaidia kujua tabia ya viongozi wetu hivyo hatuna budi kumtetea mtuhumiwa aachili huru kwa kuonyesha mashairi ya wasanii wanaokumbatiwa na serikali kwa kuhamasisha ngono kwenye jamii hasa watoto ambao wanakua wakiwa wanaona ngono ni jambo la kawaida sana
Unaweza kuongeza mengine ili kuionyesha serikali inavyoshabikia uvunjifu wa maadili