Royal baggies” zavuta hisia sabasaba 2025 – ubunifu wa posta wazidi kupaa

Royal baggies” zavuta hisia sabasaba 2025 – ubunifu wa posta wazidi kupaa

PendoLyimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2014
Posts
1,059
Reaction score
1,133
📍 SABASABA, Dar es Salaam
🗓️ 5 Julai, 2025

“ROYAL BAGGIES” ZAVUTA HISIA SABASABA 2025 – UBUNIFU WA POSTA WAZIDI KUPAA


Katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA 2025), Shirika la Posta Tanzania limekuwa gumzo baada ya kuanzisha huduma mpya ya usafiri wa ndani ya viwanja kwa kutumia Royal Baggies gari maalum za umeme zenye muonekano wa kifahari, ufanisi na hadhi ya kitalii.

Huduma hii imelenga kuwawezesha washiriki na wageni wa maonesho kuzunguka kwa urahisi katika mabanda mbalimbali bila usumbufu wala kuchoka. Royal Baggies zinachukua abiria hadi 27, zikiwa na mwonekano wa kuvutia na muundo rafiki kwa mazingira, kwani zinatumia nishati safi ya umeme.

Huduma hii inaendelea kutolewa kila siku ndani ya Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, hadi tarehe 13 Julai 2025.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania

IMG-20250705-WA0127.jpg
IMG-20250705-WA0123.jpg
IMG-20250705-WA0126.jpg
 

Attachments

  • IMG-20250705-WA0124.jpg
    IMG-20250705-WA0124.jpg
    479.4 KB · Views: 18
  • IMG-20250705-WA0125.jpg
    IMG-20250705-WA0125.jpg
    609.3 KB · Views: 20
  • IMG-20250705-WA0121.jpg
    IMG-20250705-WA0121.jpg
    610.3 KB · Views: 20
  • IMG-20250705-WA0122.jpg
    IMG-20250705-WA0122.jpg
    655.7 KB · Views: 15
  • IMG-20250705-WA0119.jpg
    IMG-20250705-WA0119.jpg
    546.1 KB · Views: 19
  • IMG-20250705-WA0118.jpg
    IMG-20250705-WA0118.jpg
    356.8 KB · Views: 22
  • IMG-20250705-WA0120.jpg
    IMG-20250705-WA0120.jpg
    474.9 KB · Views: 19
  • IMG-20250705-WA0117.jpg
    IMG-20250705-WA0117.jpg
    503.9 KB · Views: 18
  • IMG-20250705-WA0116.jpg
    IMG-20250705-WA0116.jpg
    390.4 KB · Views: 17
Shirika lifungwe tu wawaachie madekenya...labda tutatumia kupokelea persel zetu maana hakuna Cha maana wanachofanya...mizigo inappotea hovyo...
 
Back
Top Bottom