Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,730
- 4,924
Katika mahojiano maridhawa ya Mwanahabari nguli Tido Muhando wa TBC na Mfanyabiashara "guru" Rostam Abdulrasul Aziz pamoja na kuongea mengi juu ya biashara na siasa, Watanzania tumeshauriwa kutokuuona Umasikini kama jambo la fahari au la kawaida.
Watanzania wengi imesemekana tunauona Umasikini kama hali ya kawaida kabisa na mtu akifanikiwa kutoka kwenye lindi la Umasikini tunatamani kumvuta arudi nyuma tena.
Kuhusu makaa ya mawe: Mfanyabiashara guru amedai kuwa hisa alizonunua hakuuziwa na Serikali ila alizinunua kutoka kwenye kampuni ya nje iliyokuwa inamulikiwa na Mzungu (INTRA ENERGY CORPORATION) ya Australia tena kwa kuzingatia hesabu za soko la hisa za Australia. Katika eneo hili aliongezea kusema kuwa kuna migodi zaidi ya 16 inayomilikiwa na kampuni mbalimbali na yeye bado hajaanza kuvuna makaa hayo katika eneo lake, anakamilisha baadhi ya vitu
Kuhusu Mwadui: Mfanya biashara huyu alisema kuwa hisa alizozinunua zimezingatia ithibati ya soko la hisa la "London" Uingereza London Stock Exchange (LSE) kwa sababu alizinunua kutoka kwenye kampuni ya Uingereza.
Tuje hapa, ule uvumi kuwa Serikali ndiyo iliyomuuzia kwa bei chee kwa maelezo ya Guru huyo wa biashara ni dhahiri unakwenda kukosa mizizi thabiti na kubaki kama aina nyingine ya vumi za kurudishana nyuma.