Rostam - Parapanda

Rostam - Parapanda

Leo nimeiskiliza hii nyimbo ni balaa yani ni bonge la idea full kung'ata na kupulizaaa yani wameimba kama PANYA.😎😀

Wimbo wa taifa anaekubali agonge like

[/

Eti Nyimbo
 
Mimi kwenye huu wimbo ukiacha uimbaji wa Roma na Stamina lakini mixing ya beat imechangia sana wimbo huu kuwa mzuri hasa kwenye chorus na sauti fulani zina sikika kwa mbali kwenye beat....heeee heeee
 
HAWA JAMAA NI PANYA SANA,WAMENG'ATA NA KUPULIZA
Lyrics1:
NYERERE:Karibu Mzee kingunge,kwenye makazi ya milele
Mi huku na mji wangu,tayari unaitwa Nyerere
Nimeshtuka kukuona huku,nini chanzo cha msiba?
KINGUNGE:Ni mipango ya mungu,na nmekumiss swahiba
NYERERE:Vipi nchi yangu mtawala ni chama gani?
KINGUNGE:Bado CCM ingawa kuna upinzani
NYERERE: Unamaana gani,kwani Rais ni nani?
KINGUNGE:Rais ni John,ndo anaongoza usukani
NYERERE: John Mallecela?
KINGUNGE:No,Magufuli,ulimwacha mbunge wa chato sijui unamkumbuka vizuri?
NYERERE: Aaah!ngoja kwanza,unajua haya mambo haya,
Mi nlidhani alipotoka Mkapa angefata Jakaya
KINGUNGE:Jakaya alitawala,akaja akaretire
Nimeacha mambo mengi,yani mambo ni moto,mambo ni fire
NYERERE: Aa'aaa!mbona naskia mambo si sawa
Na ni akina nani wanaojiita hawa,ambao wanajiita ukawa?
KINGUNGE:Ni wapinzani waloungana, lakini hawakumshinda magu
Wengine chama walihama,na bado wakapata tabu (sana)
Kakomesha ufisadi,kaongeza ukusanyaji kodi,hakika wamepata mkomboZi ambae atawafikisha nchi ya ahadi
NYERERE: Niliskia skuizi bunge halioneshwi kwenye TV
Inamaana hoja za viongozi wananchi hawaziskii
Mitandao ya kijamii je?vipi inasaidia?
KINGUNGE: Kuna dada anaitwa Mange,please hide my ID
Lyrics2:
NYERERE: Je vipi kaburi langu,tayari wamelijengea?
Na vipi kuhusu mke wangu,Maria wanamtembelea?
KINGUNGE: Kuhusu kumtembelea,hilotoa shaka
Wanamjali na kumlea,tena kwa heshima ya mamlaka
NYERERE: Nimwona shemeji yangu,ama kweli mnapendana
Penzi la kweli kufa na kuzikana
Vipi mwanangu Makongoro,analinda mali zangu?
KINGUNGE:Bora wakwako mwenzie yupo busy na Tunda
Hivi Julias ulikua simba au yanga?
NYERERE: Kiukweli niliipenda yanga,ila simba ni kisanga
KINGUNGE:hahaa!mwalimu unajua hadi kisanga
NYERERE: Acha hilo naskia mengi,kibamia hadi kudanga
KINGUNGE: HahaHAa
NYERERE:Na mwona komba huju,nyimbo za chama anatunga nani?
KINGUNGE:Mi naskia wataisoma namba ila sijui ametunga nani?
NYERERE: Sijakuelewa kwani anaesimamia baraza nani?
KINGUNGE: lipo baraza ila wasanii wanaishi uani
Chorus
Wanamiliki vicent,
Mambo yamebuma mipango haielewekii
Kuna manabii fekii,Ramani hakuna kila kitu hakielewekii
Parapanda italia parapanda
Parapanda italia parapanda
Lyrics3:
NYERERE: vipi kuhusu muungani upo au umechuja?
KINGUNGE: Mpemba anauza kariakoo,mzaramo anamiliki duka unguja
NYERERE:Ujinga,Maradhi,Umaskinu bado maadui wataifa?nipe taarifa
KINGUNGE: Ujinga angalau,hao wengine janga la taifa
NYERERE: Kuhusu barabara?
KINGUNGE: zipo
NYERERE: Madaraja?
KINGUNGE: Yapi
NYERERE: kama ni hivyo uchumi umepanda
KINGUNGE: Wadai cherehani mbili ukiwanazo ni kiwanda
Vyuma bado vipo still na hospitali hakuna vitanda
NYERERE: Bado na maswali mengi vipi mwenendo wa katiba
KINGUNGE: Mchakato waliusitisha inasemekana walimpiga
NYERERE: Walimpiga nani?na ni akina nani,na ninani alifanya?
KINGUNGE: Mwalimu sijui ila ni watu wasiojulikana
NYERERE: walompiga risasi Lissu?
KINGUNGE: ni watu wasio julikana
NYERERE:na ni akina nani waliomteka Roma?
KINGUNGE: ni watu wasiojulikana
NYERERE: na wanaoteka waandishi wa habari
KINGUNGE: E eeh!sijui ni watu wasio julikana, hahahaa....
FB_IMG_1533628685414.jpg
 
Roma naona akili imekaa sawa sasa au amesha update kwa Babu.

BonGe la creativity
 
Back
Top Bottom