Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Mfanyabiashara Rostam Aziz kwaniaba ya Sekta binafsi nchini Tanzania Alhamisi Julai 17, 2025, amebainisha kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 ni Dira ya wananchi, akimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kwa kusimamia na kuufanya mchakato wa uandaaji wa Dira 2050 kuwa wa uwazi na shirikishi.
"Sisi sekta binafsi sio tu tulipewa nafasi ya kutoa maoni yetu, tulisikilizwa na siyo kwamba tulisikilizwa tu, maoni yetu yametumika katika kuiunda Dira hii. kwa mfano wakati rasimu ya kwanza ilipotoka Tume ilipendekeza uchumi wetu ufikie Dola za Marekani Bilioni 500-700 ifikapo 2050, sisi wafanyabiashara tulitofautiana nao, tukapendekeza kurejea tena katika jambo hili na baadaye ikakubalika kuwa uchumi wetu utafikia Trilioni 1. Huu ni mfano tu wa jinsi sekta binafsi ilivyoshirikishwa." Amesema Rostam.
Katika maelezo yake mfanyabiashara huyo pia amesisitiza umuhimu wa kuandaa Dira hiyo kama mpango wa maendeleo wa taifa kwa miaka 25 ijayo, akiomba nidhamu katika utekelezaji wake kama hatua muhimu ya kuweza kufikia matamanio ya Watanzania kwa miaka 25 ijayo.
Rostam kadhalika ameipongeza Wizara ya Mipango na Uwekezaji kupitia kwa Waziri wake Prof. Kitila Mkumbo na Katibu Mkuu Bi. Tausi Kida pamoja na timu ya wataalamu wa mchakato wa Dira 2050 wakiongozwa na Dkt. Asharose Migiro, akisema umahiri wao ndio uliofanikisha Tanzania kuwa na Dira 2050 iliyo na ushirikishwaji mkubwa wa wananchi wa Tanzania.