mkerewe halisi
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 299
- 152
Mfumo ni nini
Kwa kifupi sie tunachotaka ni majimbo na watu, na mie kama mwenyekiti wa chama nataka nipige mpunga wa kina Rostam, Chenge, Karamagi na Mzee wa machache a.k.a Media tycoon sasa hapa kinachotakiwa ni tunaita press conference alafu mie si unajua ninavojua kuongea na kupanga maneno, nitasema siasa ni dynamics, watu tunabadirisha gia hadi angani, sasa nitatangaza kuwapokea Rostam, Chenge, Karamagi na wengineo alafu nitasema ugomvi wao na familia ya Kikwete ndo ulisababisha wachafuliwe, tuna misukule mingi itatuelewa tu na haitafikiria maneno tuliosema mwanzo. Alafu habari itakuwa imeisha.
Dunia ina maajabu mengi sana lakini nafikiri saivi watanzania lazima watangazwe kuwa ajabu jipya la dunia.
Hata Chenge ni msafi tatizo ni mfumo
Ona sasa, badala ya kutumia hekima ya kukaa naye ili atueleze vizuri maana ya kusema hivyo ni vijisenti tu ili atupe faida ya akina nani waligawiwa nyingi sisi tukaanza kumuita fisadi fisadi kila kona. Sasa tumepata nini? CCM inapobanwa mahali kwa uhalifu ina tabia ya kuwatosa lakini bila ya kuwapeleka mahakamani wale watakaokamatwa na ngozi ili yenyewe ionekane safi kwa watu na sio sehemu ya tatizo, imefanya hivyo kwa chenge, Warema, Lowassa, Tibaijuka, Karamaji, Mbilinyi...........Chenge alisema yeye amepewa kidogo (vijicent ) hii kauli nyuma ya pazia kuna waliochukua nyingi ukilinganisha na alichopata yeye.
Mfumo ni nini
Mfumo ni kitu chenye uwezo wa kusababisha twiga mzima hai apakiwe kwenye ndege bila kuonekana, mtu aliyekamatwa na meli yenye makontena ya meno ya tembo kuendelea kundunda uraiani lakini aliyeiba kuku yuko gerezani, aliyegawiwa 20mil anafahamika lakini aliyegawiwa hela za kubeba kwenye mifuko ya sandarusi hajulikani hadi leo. huu ndo mfumo kwa tafsiri ya level yako.
kila raia yuko huru hadi hapo mahakama itakoporidhika pasipo kuacha mashaka yoyote kuwa mtuhumiwa analo kosa. Tangu 2008 kama akina Rostam na EL kungekuwa na mtu, chombo au taasisi yenye ushahidi wa ufisadi wao si wangepelekwa mahakamani na kupoteza sifa ya kuhamia chadema wala kutangaza nia kupitia chama chochote hapa nchini. Lakini mmebaki kuwaita mafisadi, magamba, n.k mbona mmeshindwa kuwapeleka mahakamani au kuwavua magamba yao? usidanganywe kilaini soma siasa ili ufanye siasa. Rostam akijaribu kurejesha pesa zake alizoimiminia CCM kufanyia kampeni wanamwita fisadi, gamba, na kuchafuliwa heshima yake ili CCM kuficha uso wake mbele ya jamii. Dhambi hii itairudia CCM maana jasho la mtu ni sumu haifai kuliramba. Ndo maana ninawashauri wafanyabiashara wote watoke ccm ili waende wakafanye biashara zao kwa uhuru, uwazi na kulipa kodi stahili kwa taifa badala ya kuendelea kukamuliwa na CCM kisha inawageuka pale wanaposhtukiwa na wananchi.Na kwa kiwango chako,mfumo ni kinyume chake maana wanaofanya hayo ni dhambi za kawaida wanatakiwa kusamehewa baada ya kujieleza.aliye msafi ampige mwenzake jiwe by freeman mbowe.sasa unalalamika nini?kuna maana gani ya kulilia mfumo umnaoutukuza wenyewe?
kila raia yuko huru hadi hapo mahakama itakoporidhika pasipo kuacha mashaka yoyote kuwa mtuhumiwa analo kosa. Tangu 2008 kama akina Rostam na EL kungekuwa na mtu, chombo au taasisi yenye ushahidi wa ufisadi wao si wangepelekwa mahakamani na kupoteza sifa ya kuhamia chadema wala kutangaza nia kupitia chama chochote hapa nchini. Lakini mmebaki kuwaita mafisadi, magamba, n.k mbona mmeshindwa kuwapeleka mahakamani au kuwavua magamba yao? usidanganywe kilaini soma siasa ili ufanye siasa. Rostam akijaribu kurejesha pesa zake alizoimiminia CCM kufanyia kampeni wanamwita fisadi, gamba, na kuchafuliwa heshima yake ili CCM kuficha uso wake mbele ya jamii. Dhambi hii itairudia CCM maana jasho la mtu ni sumu haifai kuliramba. Ndo maana ninawashauri wafanyabiashara wote watoke ccm ili waende wakafanye biashara zao kwa uhuru, uwazi na kulipa kodi stahili kwa taifa badala ya kuendelea kukamuliwa na CCM kisha inawageuka pale wanaposhtukiwa na wananchi.[/QUOT
Kuku wewe
Waswahili walisema 'ukipenda chongo unakiita kengeza'. CHADEMA ya Mbowe sasa imeamua kukumbatia 'magamba' na sasa yanabadilishwa jina na kuitwa 'wajasilimali safi'.
Swali, je si ni bora ya shetani tumjuaye, CCM, kuliko huyu anayehalalisha madhambi, CHADEMA, kabla hata ya kunusa madaraka?