kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,710
- 17,204
Kuna dhana inayojengeka kuonesha kuwa Rostam Aziz ni mwizi na fisadi, hii ni dhana potofu kabisa. Huyu jamaa ni mtanzania na mfanyabiashara wa siku nyingi aliyekuwa akijitafutia riziki zake halali ya kijasiliamali. Kosa kubwa ni la CCM ambayo ilikuwa inachukuwa hela kutoka kwa wafanyabiashara katika kukiendesha chama na kugharamia chaguzi zake. Hata Sumaye alipokuwa waziri mkuu aliwahi kuitoboa hii siri kwa kuwaambia wafanyabiashara wanaotaka mambo yao ya biashara yawe sawa wabaki CCM. Wafanyabishara nao akiwemo Rostam walikuwa na haki ya kuwauliza CCM namna watakavyofaidika na kuzirudisha pesa zao wanazoipa CCM. CCM ilikuwa inawalipa kwa kuwapa misamaha ya kodi, kupata upendeleo kwenye kupata tender mbalimbali serikalini na ndani ya chama kwenyewe na kupewa nafasi za uongozi kama vile ubunge na uwaziri. Kwahivyo Rostam Aziz alikuwa anatekeleza maagano yao na CCM ya namna ya kufaidika kwa kubaki CCM na kurejesha mabilioni yake aliyokuwa anaipa CCM kuendeshea chama kwa kufanya vitu hivi leo vinavyowafanya tuwaite mafisadi. Ukweli ni kwamba kwenye serikali ambayo ina vyombo vya usalama, sheria na magereza kama akina Rostam wangekuwa mafisadi na wezi kweli basi hivi sasa wangeshafungwa kama akina Mramba. Tuache kuupotosha ukweli hapa na kuufisha ukweli pale. Ningekuwa mimi Mbowe ningewakaribisha chadema hata akina Rostam, Dewji, Karamaji, Mengi, Mosha, Azam, Sabodo, Manji n.k ambao wanaishi kwa hofu na vitisho ndani ya CCM na kulazimishwa kuchangia kwa nguvu hata kama hawapendi. Chama chochote kinahitaji watu matajiri wenye moyo wa kutoa kwa hiari yao sehemu ya faida zao katika kugharamia ujenzi wa demokrasia kwenye taifa lao, lakini isiwe vitisho au kuahidiwa kutolipa kodi.
Rostam sio fisadi hata kidogo ila fisadi ni CCM, na kama akiomba kuhamia Chadema, CUF au NCCR msisite kumchukua kwa mikono miwili pia. Maana UKAWA atakutana na mazingira yasiyoruhusu kufanya vile alivyokuwa akifanya kule CCM ambako walikuwa wakiombwa pesa kwa nguvu na vitisho vya kufirisiwa biashara zao kama hawatoi fedha kwa CCM.
Rostam sio fisadi hata kidogo ila fisadi ni CCM, na kama akiomba kuhamia Chadema, CUF au NCCR msisite kumchukua kwa mikono miwili pia. Maana UKAWA atakutana na mazingira yasiyoruhusu kufanya vile alivyokuwa akifanya kule CCM ambako walikuwa wakiombwa pesa kwa nguvu na vitisho vya kufirisiwa biashara zao kama hawatoi fedha kwa CCM.