Rostam amwanika Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam amwanika Pinda

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Dingswayo, Aug 12, 2010.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Na Mwandishi wetu
  12th August 2010


  [​IMG]
  Barua mbili zilizoandikwa na Waziri Mkuu Pinda


  Mbunge wa Igunga (CCM) mkoani Tabora aliyemaliza muda wake, Rostam Aziz, bila kujua au kwa sababu ya kutafuta kura tu, ameanika udhaifu wa kiutendaji wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

  Udhaifu huo unajieleza katika nyaraka za serikali ambazo Rostam kwa kutumia njia zake binafsi alizipata na kuzitumia kujinadi kisiasa katika jimbo la Igunga kuomba kura za maoni kutoka kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi hivi karibuni.

  Rostam amechukua barua mbili zilizoandikwa na Waziri Mkuu Pinda kwenda kwa mawaziri wawili, akiwaagiza utekelezaji wa miradi ya umeme na barabara katika mkoa wa Tabora, wilayani Igunga, na kuzifanya vielelezo katika kitabu chake cha "Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi mwaka 2005 hadi 2010."


  Katika kitabu hicho chenye kurasa 27 kikiwa na picha kubwa ya Rostam kwenye jalada, pia kinajieleza kuwa "Igunga ya mwaka 1964 si Igunga ya sasa Tuendelee kushirikiana kujenga Igunga yetu", barua hizo licha ya kutokunakiliwa kwa Rostam, zina kumbukumbu namba moja.


  Barua ya kwanza ambayo iliandikwa na Waziri Mkuu Pinda na kuweka saini yake, ni ya Machi 8, 2010 ikiwa na kumbukumbu namba PM/P/567/31 kwenda kwa Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, ikiwa na kichwa cha habari; Ujenzi wa barabara ya Shinyanga – Igunga kupitia Ukenyenge.


  Barua hiyo imenakiliwa kwa Rais Ikulu na kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa.


  Katika barua ya pili ambayo pia iliandikwa na Waziri Mkuu Pinda Mei 6, 2010, miezi miwili baada ya ile ya kwanza, ina kumbukumbu namba ile ile yaani PM/P/2/567/31 ikielekezwa kwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, na nakala yake kupelekwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mwinyimsa. Barua ya pili ina kichwa cha habari; "Miradi ya umeme mkoani Tabora" kama ya kwanza nayo haikunakiliwa kwa Rostam, lakini amezitumia kwenye kitabu chake, akinakili kumbukumbu namba zake kama zilivyo bila kuonyesha kuwa zina mgongano.


  Baadhi ya wakazi wa Igunga waliozungumza na NIPASHE juu ya kitabu hicho, walisema ndicho alikuwa akitumia Rostam kujinadi wakati wa kusaka kura za maoni katika jimbo hilo ambako aliibuka mshindi kwa kishindo.


  Rostam katika sehemu ya utangulizi ya kitabu hicho, ameandika kuwa tatizo la muda mrefu la kijiji cha Simbo kutokuwa na umeme limepatiwa ufumbuzi, baada ya yeye kufuatilia kwa Waziri Mkuu ambaye alimwagiza Waziri Ngeleja ahakikishe umeme unafika kwenye kijiji hicho kama ilivyokusudiwa kwa barua yenye kumbukumbu namba MP/P/2/567/31 ya Mei 6, mwaka huu.


  Kadhalika, aliandika kuwa kwa tatizo sugu la daraja la mto Mbutu lililoko Igunga, Waziri Mkuu alikwishamuandikia Waziri Kawambwa barua yenye kumbukumbu namba MP/P/2/567/31 ya Machi 8, mwaka huu ili wizara ichukue hatua za kuipandisha hadhi barabara hiyo kuwa ya Mkoa.


  Alipotafutwa kuelezea utata wa barua hizo, Mwandishi wa habari wa Waziri Mkuu, Said Nguba, alisema hawezi kutoa maelezo ya aina yoyote kuhusiana na barua hizo.


  "Sina Comment (kauli) kabisa, mimi kama mwandishi wa Waziri Mkuu sina cha kukueleza kuhusu suala hilo na nisingependa uandike maelezo yangu ila kama unataka andika tu," alisema Nguba.


  Alisema ni vyema mwandishi akawasiliana na Rostam mwenyewe kwani yeye hakuwa na jibu lolote kuhusiana na barua hizo mbili.


  "Umeshawasiliana na Rostam Aziz, ni vyema ukamuuliza mimi sina cha kukueleza kabisa," alisema Nguba.


  Hata hivyo, alipotafutwa kwa simu kwa wiki moja sasa, Rostam hakupatikana na simu zake zote zilikuwa zikiita bila kupokelewa. NIPASHE itimtumia ujumbe mfupi sms, lakini hakujibu.


  Mkanganyiko wa barua hizi unaacha maswali kama Waziri Mkuu anaweza kuandika barua mbili tofauti kwa nyakati tofauti na zikawa na kumbukumbu namba moja. Hali hii pia inaacha maswali juu ya usahihi wa taarifa mbalimbali za serikali na jinsi zinavyoweza kutumiwa na watu ambao hawakulengwa, kama zilivyo barua hizi.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Patamu zaidi....wao kwa wao...na muhimu zaidi sisi kwa wao pia
   
 3. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2010
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mbona karatasi zina nembo ya ccm? ni barua za kiserikali ama za kichama?
   
 4. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  What is happening here!?

  Where is the credibility and nobility of RA?

  Hivi kutaka kuchaguliwa ubunge lazima upitie uchochoro kama huu? Wako wapi viongozi safi wanaojiamini kwa kazi zao nzuri, hekima na ubinadamu wao? ...Wasio hitaji nguvu kubwa namna hii ku impress wapiga kura .... kama kiongozi ni safi ni safi tu ... YOU DONT NEED ALL THIS SIR!!
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Maskini Pinda na wasaidizi wake... barua mbili, kumbukumbu moja, agizo la fisadi uanlitekeleza kwa haraka mpaka unasahau hata folio namba? Kweli hii inahuzunisha...

  Kinachoniudhi sana ni pale ambapo sisi kajamba nani tunauana kwa bunduki kama AK47 tukinyang'anyana pikipiki za mchina huko kimara, au toyota GX100 salasala... na tunaacha watu kama hawa wakiwatuma mawaziri wetu kama ma-house boys!

  :mad2:
   
 6. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  huyu jamaa anadhihirisha alivyokuwa na access na "sirikali"..
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  ikiwa walimtosa EL watashindwa Pinda?
   
 8. M

  MJM JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Fake letters! Kaandika na kujijibu huyo si unajua uwezo wake ulivyo mkubwa katika kudanganya? Pia chama hiki ni fake hakuna utaratibu wa kutumia nembo za chama katika barua yaani yeyote tu anatumia hata kama siyo mtendaji wa ofisi za chama? Waziri mkuu atumie, Mbunge atumie, Diwani atumie, Mawaziri yaani kila mtu!
   
 9. Mwanamosi

  Mwanamosi Member

  #9
  Aug 12, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HAYA MAAJABU YA DUNIA....HEBU SOMA HII NUKUU HALAFU NIKWAMBIE NILICHOGUNDUA..!!!!

  Nadhani iko haja ya kuacha ushabiki na kujihakiki wenyewe kabla hatujachangia...hivi hatuoni namba hizo ni tofauti???PM/P/567/31 na PM/P/2/567/31 hivi hakuna tofauti hapo?

  Nadhani mwandishi ana maana fulani kuweka 2 katika barua ya pili may be akimaanisha ni mwendelezo wa barua ya kwanza juu ya swala lile lile linalohusu wizara 2 tofauti. Nionavyo mimi kwa kuwa masuala yanayohusu barua hizo mbili ni mtambuka basi ilibidi barua 2 kwenda wizara husika zitoke...sioni utata kwenye hilo la matumizi ya kumbukumbuku namba hizo kama nilivyojaribu kuonesha.

   
 10. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ninajua RA ni very smart na bila ubishi ameghushi barua hizi, si kama nasema MKP hawezi kufanya madudu haya, la hasha anaweza sana maana si ni walewale! lakini hebu tujiulize zaidi kweli hata kama ni mambo ya ufisadi, PM anaweza kuwa mjinga kiasi gani atumie nembo ya CCM kuandika barua ya Kiserikali? Au kama ofisi ya waziri mkuu haina letterhead zake na inatumia zile za chama sawa, lakini kwa mantiki tu ya kawaida hii haiingii akilini.

  RA ameghushi barua hizi kama alivyogushi Kagoda na Richmond!
   
 11. F

  Froida JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  MMH kwani barua hazina saini sahihi ya Pinda mtoto wa mkulima anajikomba kwa Rostam ili amgawie ngawila za kampeni nchi immeozwa kama nilivyosoma huko nyuma Rostam anahitaji kunyongwa kwa kupigwa risasi pale mnazi mmoja kiwanja cha mashujaa,mshenzi sana,hawezi kujipenyeza kwa viongozi wa wakuu kwa kiasi hiki nawanainchi tukawa tunakenua meno tuu
   
 12. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  dhu jamaa kaghushi pm hawezi kutoa maelekezo ya kiserikali kwa headed paper za chama na amefanya hivi makusudi akijua chama chake hakinaga utaratibu wa kuwaadhibu wanachma na hasa mafisadi kama yeye kama aliweza kughushi akajichotea fedha na hajachukuliwa hatua za sheria mpaka sasa sembuse hii kugushia kujizolea kura za kishindo tu sana sana watamsifu kwa ubunifu
   
 13. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Superfisadi umenichekesha "Sana sana watamsifu kwa ubunifu". Huo ubunifu ungekuwa wa kuendeleza nchi na siyo kuweka mitego (mirija) ya kinyonyaji mbona ingekuwa bomba!!
   
 14. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  PM/P/567/31 na PM/P/2/567/31 tofauti ipo. Ila ukweli ni kuwa Mwandishi wa IPPMEDIA alikosea na kusahau kuandika 2 baada ya P kwenye sehemu ya kwanza. Ukisoma hadi chini utakuta hilo tatizo kalisahihisha. Siku nyingine kuwa na subira maana Wahaya wanasema "usijigambe mbere ya Wagambirwa........."

  Umenikumbusha Mwalimu wa Siasa aliyepelekewa kusimamia mtihani wa form 4 na juu ya karatasi pameandikwa "Q no. 20 solve without using table" na yeye akawaamuru wanafunzi wote watoke nje wakafanye bila kutumia MEZA. Kama angelifanya utafiti wa kusoma swali lenyewe, labda angelifahamu TABLE ninini.

  Ngoja nikuwekee hiyo sehemu ili uone maajabu ya dunia ya JF.


  Bado una swali? Hakuna, Kawawa funika kikombe (Nyerere, Kizota).


   
 15. Kidege

  Kidege Member

  #15
  Aug 12, 2010
  Joined: Jul 18, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hivi huko Igunga hakuna mpizani wa kumuangusha fisadi huyu?
   
 16. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #16
  Aug 12, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Who is smarter here?

  [​IMG]
   
 17. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45

  Ha ha haa, imechukua sekunde kadhaa kuelewa.
   
 18. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hivyo anaweza kuwa pm mwakani kama uwezo wake ni mkubwa!
   
 19. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,189
  Trophy Points: 280
  Waandishi wa bongo badala ya kutuambia barua inasema nini kibaya, ku validate authenticity ya barua, au kutuambia kuna conflict of interest Waziri Mkuu kuandika barua kwa letterhead ya chama, wanatuambia kuhusu namba ya barua yenye utata usio utata !

  I bet nikizisoma hizo barua kuna issues kibao nyeti za kuzungumzwa.
   
 20. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hapa ndipo JF somtimes na sisi tunakuwa kama wao. Rostam kaandika kijitabu cha kuomba achaguliwe kwenye kura za maoni. Katika kurasa za kitabu hicho kila page ina nembo ya CCM, kama wanavyovaaga yale magwanda ya kifisadi(kijani).

  Barua imepachikwa hapo, mwenye kitabu ka-scan page katoa na nembo ya CCM. Sasa sisi tunaanza kujadili nonsense badala ya kujadili mantiki ya barua na uhuru wa waziri mkuu kama taasisi. Tunarudi kulekule kwa TAKUKURU kutumiwa kama ambavyo Waziri mkuu katumiwa.
   
Loading...