Upanga Mkali
Member
- Dec 24, 2014
- 96
- 83
Na Mwandishi Wetu
Rostam Aziz aliyejiuzulu Ubunge wa Igunga mwaka 2011 kwa shinikizo kutokana na kashfa ya ufisadi, amerudi kwenye siasa kwa nguvu kubwa huku akiapa kuwa ni lazima ahakikishe anamuingiza Rais wake kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka 2015 kwa kutumia fedha alizonazo.
Katika kuitimiza azma yake hiyo ya kuingia Ikulu kwa mlango wa nyuma, tayari amekuwa akiratibu vikao mbalimbali vya kimikakati nyumbani kwake Oysterbay, ili kuhakikisha kuwa mgombea wake ambaye amejijengea sifa ya kuwa mgawaji fedha maarufu kwenye harambee na tafrija mbalimbali, anapitishwa na CCM na hatimaye kuwa Rais wa Tanzania.
Pamoja na kuwa jina lake na la mgombea amtakaye tayari yameshachafuka sana mbele ya macho ya Watanzania, kutokana na kashfa zao za ufisadi zilizowahi kuwakumba huko nyuma; wawili hao wamepanga kutumia kiasi kikubwa cha fedha kununua vyombo vya habari ambavyo watavitumia kuendesha kampeni ya kujisafisha na hatimaye waonekane ni watu safi kabisa mbele ya wananchi.
Tayari mgombea huyo wa Rostam amesikika akiwaambia watu wake wa karibu kuwa kambi yake imeshavishika vyombo vya habari karibu vyote hapa nchini.
Karibu vyombo vya habari vyote vya Tanzania tumeviweka mkononi. Simuoni mtu wa kuzuia harakati zangu, mimi ni kama mafuriko sizuiliki, mgombea huyo alisikika akitamba.
Katika kufanikisha harakati zao, wawili hao, wamekuwa wakitumia fedha nyingi kutengeneza ushawishi kwa makundi mbalimbali ya kijamii. Tayari mgombea huyo wa Rostam ameonekana akishiriki harambee mbalimbali na kutoa fedha nyingi na pia amekuwa akitoa kauli zenye kuashiria kujipigia debe ili apitishwe kugombea Urais na CCM.
Pia, mgombea huyo ameendesha harakati za chini kwa chini za kuwagawa wabunge na wanachama wa CCM katika makundi ili afanikishe azma yake ya kuupata Urais. Wawili hao ambao wamekuwa pamoja katika harakati za muda mrefu wanadaiwa kujivunia nguvu kubwa ya fedha waliyonayo kufanikisha mambo yao.
Mdau mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake amedokeza: Hawa jamaa wanaamini kuwa kwa fedha walizonazo wanastahili kabisa kuinunua nchi. Wanadhani kuwa sifa ya kuwa na fedha nyingi ndiyo sifa ya kipekee kabisa ya wao kupata Urais, masuala ya uadilifu na uaminifu kwao siyo muhimu kabisa.
Mtazamo wa wachambuzi wa mambo.
Hata hivyo, pamoja na nia yake hiyo, wachambuzi wa mambo, wameyatathmini maisha ya Rostam na kubaini kuwa ni mtu hatari sana ambaye amefanikiwa kupata utajiri mkubwa kutokana na kujihusisha na dili za kifisadi ambazo zimeliacha taifa katika umaskini mkubwa.
Huyu mtu ameshiriki katika ufisadi mkubwa ambao umechangia kudhoofisha uchumi wa nchi hii halafu anarudi kwa kutumia fedha alizozipata kifisadi kutaka kuwarubuni Watanzania na kuchukua uongozi tena, hii haikubaliki, mmoja wa wachambuzi ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini alisema.
Rostam ametajwa kwenye orodha za matajiri wakubwa Afrika na Jarida la Forbes. Pia inadaiwa kuwa miongoni mwa makampuni anayoyamiliki yeye na familia yake kuwa ni pamoja na: Africa Tanneries Ltd- Mwanza, Tanzania Leather Industry Ltd- MOROGOR, African Trade Development Group (Tz), Tanzania Packages Manufacturing, Caspian construction, New Habari corporation na Wembere Hunting Safari company.
Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa mara nyingi Rostam hutumia staili ya kuanzisha makampuni kwa kutumia mawakala kufanikisha dili zake. Inadaiwa kwa hufanya hivi ili yakitokea matatizo aweze kuruka kwamba hahusiki.
Tabia ya kukwepa kujibu tuhuma za ufisadi
Pia, wachambuzi wamesema kuwa Rostam Aziz amekuwa na tabia ya kukimbia kujibu hoja mbalimbali za ufisadi zinazoibuliwa dhidi yake kwa kutoa matusi kwa watoa hoja hizo.
Kuna kipindi Rostam alibanwa kila kona kuhusu ushiriki wake katika dili kadhaa za kifisadi. Baada ya kuzidiwa alitumia staili ya kuwaita majina mabaya wale wote ambao walikuwa wakiongelea kuhusu dili zake chafu za kudidimiza uchumi wa nchi huku akizunguka nyuma na kujifanya kuwa yeye ni mtu mwema, anaendelea kueleza mchambuzi huyo.
Imeelezwa kuwa bado taifa halijasahau namna ambavyo Mchungaji Mtikila alipoambiwa arudishe hela alizokopa pale alipoibuka na kuuzungumzia ufisadi wa Rostam.
Kilichomponza Mtikila ni kitendo chake cha kuandika kijarida kilichobeba kichwa cha "Hatima ya Mwajemi Sakarir" alichokitoa mwezi juni mwaka 2008, ambacho kilizungumzia namna ambavyo nchi inatafunwa na pia kikagusa kuhusu maisha na uraia wa Rostam Aziz, mchambuzi mwingine anaeleza.
Katika kijarida hicho Mtikila alimtaja Rostam kuwa ni kiini cha uporaji mkubwa wa rasilimali za nchi unaoendelea kufanyika. Mtikila alimtaja Rostam kuwa ni mbunifu mkuu na nahodha wa mikakati iliyo mingi ya wizi wote uliofanyika katika Benki Kuu na Hazina. Sehemu ya kijarida hiyo inaeleza:
Mwajemi huyu jina lake halisi alilopewa pamoja na utambulisho wake alipozaliwa kule kwao Iran ni SAKARIR mwana wa AZIZ. Sakarir alipokuja Tanzania kuipora Nchi ya 'mataahira' kama anavyopenda kutudharau yeye mara nyingi, alijipa jina la 'Rostam'. Wazazi wa Sakarir hawajawahi kuishi hapa, wapo kwao Iran, wakiwa na biashara kubwa ya nyama na kufuga ngombe. Sakarir alipozaliwa alipata elimu yake ya msingi kwao Iran, na baadaye akapata elimu ya juu Uingereza ambako pia anao ndugu.
Mtikila alitahadharisha kuwa Watanzania wawe makini kwasababu Rostam anazo hati za kusafiria (passport) mbili ambazo anazitumia kusafiria maeneo mbalimbali na kwamba mambo yakiharibika nchini anahamia nchi nyingine.
Nilipoanza kuzungumzia uraia wa 'Rostam' Aziz alibabaisha kuwa alizaliwa Ndala Mission, lakini ni mwongo 'Rostam' amepata kudanganya kwamba alisoma shule ya msingi Mwisi, alipoona atagundulika upesi akasema alisoma Mwamala, Nzega, lakini siyo kweli. Rostam Aziz anazo Passport mbili za kusafiria, yaani ya nchi yetu ambayo aliipata kwa udanganyifu, anayoitumia kusafiria hadi Nairobi, na ya kwao Uajemi yaani Iran ambayo husafiria kutoka Nairobi kwenda kwao, Dubai na kwingine alikolimbikiza mapesa aliyaipora Nchi yetu, Mtikila alieleza katika kijarida hicho. Mtikila alimalizia kwa kuitaka Serikali imkamate na kumweka ndani Rostam.
Siku chache baada ya kutoa tuhuma hizi, Rostam aliibuka na kuitisha mkutano na vyombo vya habari ambako alisema kuwa Mtikila anamwita yeye fisadi wakati alikuwa amemkopesha shilingi milioni tatu na akasema kuwa anabaguliwa kwa kuzingatia misingi ya rangi yake.
Hoja hizi zilipingwa na wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa kuwa ni nyepesi ambapo wadau mbalimbali walisema kuwa nchi hii ina maelfu ya wafanyabiashara wenye asili ya Kiasia; Kizungu, Kiarabu ambao wana mafanikio makubwa sana kibiashara lakini hawakuwahi kuhusishwa na ufisadi wa kutisha kama alionao Rostam, sasa kwanini yeye aonewe?
Ugomvi na Mengi
Mbali na Mtikila, Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi, pia alikumbwa na mkono mkali wa Rostam pale alipomtaja kuwa ni miongoni mwa mafisadi papa wanaoididimiza Tanzania. Badala ya kuongelea kuhusu tuhuma zake, Rostam aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuanza kumshambulia Mengi kwa kusema kuwa Mengi ni fisadi nyangumi ambaye amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kuwachafua wenzake
Katika hali ya kushangaza, Rostam alienda mbali zaidi na kuyatumia magazeti na vyombo vya habari anavyovimiliki kuandika habari, makala na tahariri zilizoonyesha kuwa Mengi ni mtu asiyefaa katika Jamii na kwamba wananchi wamchukie. Rostam alisema kuwa Mengi aliifilisi Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kukopa deni lililofikia 28 Bilioni.
Wakati akimtuhumu Mengi alisahau kuwa na yeye aliinunua kampuni ya ngozi iliyokuwa chini ya umiliki wa Serikali.
Hata pale Rostam aliposhauriwa na watu kuwa kama anaona anazushiwa aende mahakamani kushtaki, alisema kuwa hawezi kwenda mahakamani kwa kuwa tuhuma dhidi yake ni za kutungiwa. Uamuzi wake huu ulitafsiriwa na wengi kuwa ilikuwa ni kama amezikubali tuhuma alizotupiwa za wizi wa mabilioni ya kodi za Watanzania kupitia EPA, Richmond na Dowans.
Pia, baada ya kuona ufisadi wake umeanikwa aliamua kuwaandama Dk. Harrison Mwakyembe kama kulipiza kisasi kwa sababu Kamati Teule ya Bunge aliyoiongoza kuanika wizi katika mkataba wa Richmond, ambao Rostam alikuwa na maslahi nayo. Vyombo vyake vikawa vikiwaandama Spika wa Bunge, Samwel Sitta, na viongozi wengine kutokana na sababu hiyo hiyo.
Kutokana na hali hiyo wadau wengi wametahadharisha harakati hizo za wawili hawa kurudi tena kwenye nafasi za uongozi wa nchi kuwa sawa na nchi kuruhusu awamu mpya ya uchotwaji mkubwa wa fedha za wananchi.
Huyu Rostam alipokuwa akijiengua kwenye Ubunge alisema kuwa ameamua kuachana na siasa za Tanzania kwakuwa ni siasa uchwara, sasa anapoamua kumuandaa mgombea Urais maana yake ni kushiriki katika siasa hizo hizo ambazo yeye aliziita kuwa ni uchwara. Inaonekana kuwa wakifanikiwa sasa hivi wataifilisi nchi kabisa, mchambuzi mwingine wa kisiasa alisema.