Rose Muhando: Situmii Madawa ya kulevya

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,374
2,000


Msanii mkongwe wa nyimbo za Injili nchini Rose Muhando amekanusha taarifa ambazo zilizagaa mitandaoni ikiwemo hapa JF kuwa ameingia katika matumizi ya Madawa ya kulevya.

Muimbaji huyo alidai taarifa hizo zilisambazwa na watu ambao hawamtakii mema katika maisha yake kutokana na kwenda nao tofauti katika makubaliano ya kufanya nao kazi.

“Situmii madawa na sitatumia, kama waliona ndiyo skendo itakayonimaliza wameshindwa, wanaofanya hivyo ni watu wanaotaka kunimaliza walitaka nifanye kazi zao, nikakataa.” Rose alisema.

Aliongeza, “Sijajiingiza na mambo hayo na wanavyozungumza nasikitika kwa sababu wanaiumiza familia yangu kisaikolojia, mimi ni mama wa watoto watatu na nina ndugu zangu, naambiwa mambo yote hayo kwa sababu sina mtu wa kunitetea,”

Katika katua nyingine muimbaji huyo alizungumzia kuhusu ukimya wake pamoja na ujio wake mpya.

“Nipo hata hivyo kuna kazi nyingine nimeandaa ipo kwa Alex Msama bado haijatoka kutokana na mambo mbalimbali, ingawa naandaa kazi nyingine ninayotegemea kuikamilisha mwezi wa tatu mwakani tutakapojaaliwa. Nimeshaanza kuandaa baadhi ya nyimbo na nyingine naendelea kutunga, unajua kazi hizi huwa nasikiliza sauti ya Mungu aniambie niimbe nini.”

“Pia, nimekuwa nafanya huduma ya kuimba katika mikutano tofauti ndani na nje ya nchi kama hivi jana umenikuta natoka kijiji cha jirani kuimba na wiki iliyopita, nilikuwa Kenya ambako nilifanya huduma, Kisumu na Mombasa, nimeamua kufanya hivyo kwa sababu zangu,” anasema Rose.

Source: Mwanaspoti
 

muhomakilo jr

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
11,165
2,000
Wakati wanaanza kubwia huwa wanakataa hivihivi...ila pambano linapopamba moto...kila kitu mwanu...kila la kher mdada..
 

KIOO

JF-Expert Member
Mar 3, 2013
6,144
2,000
Niliskia huwa anaonekana mara kwa mara kwenye kituo cha mabasi ya mwendokasi Mwanamboka Kinondoni.

Niliskia pia yupo na mtoto wa mchungaji gani sjui ana mi-tatoo kwa kwenda mbele mbapo wote ni wanachama wa chama hiko.
 

kalagabaho

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,300
2,000
Angekua hatumii madawa asingekua anaruka ruka kwa manguvu na kukata mauno namna ile...eti utamu wa yesu....utamu wa yesu???..nani kamwambia yesu anataka kutingishiwa mattako??..
 

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
8,313
2,000
TZ ukitaka upige pesa mpaka uchanganyikiwe basi we tumia mgongo wa dini kujinufaisha hasa dini ya kikristo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom