Rose Muhando akamatwa na polisi kwa tuhuma za kutapeli wanakwaya

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,245
2,000
Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia muimbaji Rose Mhando kwa tuhuma za kujipatia shilingi 950,000 kwa njia za udanganyifu

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida Deborah Magirimba amethibitisha hilo, na kuongezea msanii huyo alikamatwa Juni 1 mchana wilaya ya Ikungi baada ya waumini wa kanisa la AICT Singida kutoa taarifa za kuonekana kwake

Rose Mhando anadaiwa mnamo tarehe 3/11/2016 huko wilayani Singida alipokea shilingi 800,000 kutoka kwa Massawe Japhet kwa makubaliano atatokea kwenye uzinduzi wa kwaya ya ACT Singida lakini hakutokea,

kabla ya tarehe ya kufanyika kwa uzinduzi huo alidai tena 8/11/2016 alipokea 150,000 baada ya kudai nauli ya kutkea Dodoma kwenda Singida
Siku ya uzinduzi hakufika na waumini walipata taarifa yupo Shinyanga Kahama

 

griffin griffith

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
505
500
Dah! Shetani anashambulia watumishi wa Mungu kwa kasi ya ajabu. Ona sasa alivyomgalagaza Rose Muhando!
Utakua hujui watumishi wa mungu in wepi,toka mda mrefu na hata juzi hapa Singda wakati amelewa aliulizwa ww mhando ,iwaje upge gambe,utumie drug abuses na utapeli watu,akasema ofcoz nimekuwa nikifanyA gospel ila mm ni mfanya business
 

ISIS

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
91,521
2,000
YESU KRISTO AMEAMUA KULITETEA JINA LAKE MWENYEWE! NA BADO WAPO WENGI! ATAWAVURUGA WOTE. BINADAMU HANA CLUE NA HILO JINA NDIYO MAANA WANALICHEZEA, SASA AMESHUKA MWENYEWE WATU KAMA HAWA WATAISOMA NUMBER!
 
  • Thanks
Reactions: PNC

ISIS

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
91,521
2,000
Tulikuwa tunamwamini sana huyu dada na nyimbo zake murwaa, dadeki walahi!
 
  • Thanks
Reactions: PNC

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
5,129
2,000
Wasanii tumieni vizuri kipindi cha mavuno, maana kiangazi kikifika hata mchicha hamtauona
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom