Rombo: Mwili wa Kijana Godwin Massawe wakutwa msituni ukiwa hautoi harufu. Wakutwa ukiwa na Rozari na Biblia

SIMANZI
53386897_2163507227078242_7657445712560390144_n.jpg


Godwin Frimin Massawe umeondoka katika Dunia hii
lakini Tutakukumbuka na Tutakuombea.Mwanangu
Godwin naamini Upo kwa Mungu unatuombea zaidi
kwa jinsi kifo chako kilivyotokea. Sijawahi kusikia kifo
cha aina hii zaidi ya kusoma kwenye vitabu vya maisha ya watakatifu. Godiwin alihitimu Kisale secondary 2012,shule ipo mkoani Kilimanjaro wilaya ya Rombo.Alipenda kuishi maisha ya sala,kusoma bibilia kila mara na alifika mahali akasema hakuna anachokitafuta duniani zaidi ya kuishi maisha yatakayomuongoza kufika mbinguni kwa kusoma na kufuata maandiko matakatifu ya bibilia.

Alienda kufanya kazi na Wilvic labour solution kama
data entry. Lakin siku moja aliamua kuacha kazi
akarudi nyumbani. Alipoulizwa kwa nn alisema
"anafanya kazi masaa mengii mnoo mpaka anakosa muda wa kwenda kwenye ibada,kusoma bibilia na
kufanya tafakar" aliendelea kusema "kuliko niendelee na kazi ambayo inaniweka mbali na Mungu halafu nikafa naiacha bora niache nikamtumikie Mungu" Akamwambia baba yake nataka kwenda kujiunga na mabrother niwe nasali mda wote. Akapelekwa.Lakini siku moja akarudi nyumban.

Alipoulizwa akasema kule nilifikiri ni sehemu ya kusali, kuimba na kusoma bibilia mda wote kumbe hapana. Bora nirudi nifanye mda wangu wote wa sala. Siku ya jumapili alienda kanisani na hakurudi nyumbani Alitafutwa kila mahali hakupatkana,Taarifa zilipelekwa mpaka kanisan na kituo cha polisi, Ni mwezi sasa umepita.

Jana taarifa za wazee wanaopasua mbao katikati ya msitu zikasema kuna mtu ameonekana alifariki mda
mrefu na ana bibilia. Taarifa zilipotufikia basi baba
yake anaondoka na polisi leo kuelekea msituni
wakiongozwa na wale wazee wapasua mbao.

Msitu upo Kule katangara,mwisho wa watu kuishi
unaingia ndani mwendo wa masaa manne. Kuna
barid kali sana na wanyama wakali pia. Ndipo
wakamkuta Godiwin amepiga magoti kwenye
gogo, akiwa na Rozary yake shingoni na biblia ipo
chini imefunguliwa kitabu cha SIRA. Godiwin ameshaoza amebaki mifupa tuu na hatoi harufu yoyote. Amevalia nguo zake vilevile. Godiwin alienda msituni kufunga na kusali mpaka akafariki.

Polisi na baba yake wakamchukua na kumpeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti kule Huruma hospital.

Taratibu za mazishi zinaendelea.Godiwin aliamua kujitoa kutuombea na kusali na Mungu aliamua tunapomtafuta tusimkute mpaka mapenz yake yatimie.Basi ni majonzi kwa familia na wazazi na wahitimu na wanafunzi wa kisale secondary, wananchi wote wa mashati rombo,kanisa Katoliki na watanzania wote kwa ujumla.

Tumuombee Godwin wakati huu akiwa na malaika na watakatifu mbinguni makao ya kusali na kumsifu
Mungu milele yote.

C&P
Hahahaha mm nimeishia kucheka tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo alikuwa na matatizo ya akili.Yawezekana utotoni aliishi maisha ya mateso makubwa kiasi kuwa tamanio lake kubwa ni kukaa na Mungu tu sio wanadamu waliompa mateso makali waweza kuwa wazazi au aliishi maisha magumu mno kutokana na umaskini mkubwa wa kifamilia nk Hiyo hali huwapata wengi hasa wanaopitia mateso makali ya maisha hupenda tu wakae wakisali tu ukimwambia inatakiwa Kazi na Sala haelewi anataka asali tu.Ndio maana hata alipopelekwa kanisani kwa ma brother alishindikana hakujua kuwa kule ni kazi na Sala sio Sala tu.Ushauri.kila mzazi ajitahidi kutompa mateso ya Aina yeyote ya kimwilii,kiakili au kisaikolojia mtoto hasa akiwa mdogo yaweza pelekea shida mbele
 
Kuna watu wao pesa na maisha si Mali kitu kwao, Kuna watu ambao wameyadharau maisha haya, na ukitafakari sana utagundua kuwa maisha ni utumwa na kuishi ni sawa na kujirisha upepo, lakini Kuna wengine ambao fikra zako na furaha zao wameziweka katika pesa, hawa huwa wanapata tabu sana, kwani pesa ni namba na namba hazina mwisho, nenda Godwin wajinga watakubeza kwa kuwa hawaoni na hawatoweza kujua chochote, kwani moyo wa mtu ni kiza kinene, HERI KUFA KULIKO KUISHI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliwezekane kuwa amepiga magoti wakati alishaoza? Lakini nadhani huyo kijana alikosa ushauri wa kisaikolojia
 
Kuna watu wao pesa na maisha si Mali kitu kwao, Kuna watu ambao wameyadharau maisha haya, na ukitafakari sana utagundua kuwa maisha ni utumwa na kuishi ni sawa na kujirisha upepo, lakini Kuna wengine ambao fikra zako na furaha zao wameziweka katika pesa, hawa huwa wanapata tabu sana, kwani pesa ni namba na namba hazina mwisho, nenda Godwin wajinga watakubeza kwa kuwa hawaoni na hawatoweza kujua chochote, kwani moyo wa mtu ni kiza kinene, HERI KUFA KULIKO KUISHI

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa hiyo Mungu ni mjinga alivyotupatia hivi vitu vyote huku duniani?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana taarifa za wazee wanaopasua mbao katikati ya msitu zikasema kuna mtu ameonekana alifariki mda

mrefu na ana bibilia. Taarifa zilipotufikia basi baba

yake anaondoka na polisi leo kuelekea msituni

wakiongozwa na wale wazee wapasua mbao.



Msitu upo Kule katangara,mwisho wa watu kuishi

unaingia ndani mwendo wa masaa manne. Kuna

barid kali sana na wanyama wakali pia. Ndipo

wakamkuta Godiwin amepiga magoti kwenye

gogo, akiwa na Rozary yake shingoni na biblia ipo

chini imefunguliwa kitabu cha SIRA.

Kwanza hao wazee wakamatwe na waoneshe vibali vya kupasua mbao katikati ya msitu

Pili,hapo nilipokopi pamenichanganya ninavyojua hiyo misitu haikauki mvua au umande na upepo wa hapa na pale ila ya Mungu ni mengi.
M.H.S.R.I.P Godwin
😂😂😂😂😂😂 Sihami Bongo mm aisee khaaa eti wakamatwe kama wana vibali..jaman nimechek sana..hii ndo Tanzania zaidi ya uijuavyo..!hapa kazi tu😂😂
 
Hiyo sio sifa nzuri na wala sio mfano wa kuigwa, marehemu alikua na matatizo ya akili, alistahili atibiwe awe mwanadamu wa kawaida... Religious extremist wapo wa aina nyingi, wapo wanaojilipua mabomu, wapo wanaopinga elimu dunia, wapo wanaona kusali masaa 24 ndio njia sahihi ya kuishi
Upo so smart. Marry me before u end up with someone stupid

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo alikuwa na matatizo ya akili.Yawezrkana utotoni aliwahi maisha ya mateso makubwa kiasi kuwa tamanio lake kubwa ni kukaa na Mungu tu sio wanadamu waliompa mateso makali waweza kuwa wazazi au aliishi maisha magumu mno kutokana na umaskini mkubwa wa kifamilia.Hiyo hali huwapata wengi hasa wanaopitia mateso makali ya maisha hupenda tu wakae wakisali tu ukimwambia inatakiwa Kazi na Sala haelewi anataka asali tu.Ndio maana hata alippopelekwa kanisani kwa ma brother alishinfikana hakujua kuwa kule ni kazi na Sala sio Sala tu.Ushauri.kila mzazi ajitahidi kutompa mateso ya Aina yeyote ya know ili kiakili au kisaikolojia mtoto hasa akiwa mdogo yaweza pelekea shida mbele


Hizi pbm haziwakuti maskini tu..ukiwa mpenzi wa kusoma soma majarida ya wenzetu wazungu wanaongoza kwa hii shida..!hata matajiri zinawakuta sana zaidi!8
 
Back
Top Bottom