Rombo: Mwili wa Kijana Godwin Massawe wakutwa msituni ukiwa hautoi harufu. Wakutwa ukiwa na Rozari na Biblia

SIMANZI
53386897_2163507227078242_7657445712560390144_n.jpg

Godwin Frimin Massawe umeondoka katika Dunia hii
lakini Tutakukumbuka na Tutakuombea.Mwanangu
Godwin naamini Upo kwa Mungu unatuombea zaidi
kwa jinsi kifo chako kilivyotokea. Sijawahi kusikia kifo
cha aina hii zaidi ya kusoma kwenye vitabu vya maisha ya watakatifu. Godiwin alihitimu Kisale secondary 2012,shule ipo mkoani Kilimanjaro wilaya ya Rombo.Alipenda kuishi maisha ya sala,kusoma bibilia kila mara na alifika mahali akasema hakuna anachokitafuta duniani zaidi ya kuishi maisha yatakayomuongoza kufika mbinguni kwa kusoma na kufuata maandiko matakatifu ya bibilia.

Alienda kufanya kazi na Wilvic labour solution kama
data entry. Lakin siku moja aliamua kuacha kazi
akarudi nyumbani. Alipoulizwa kwa nn alisema
"anafanya kazi masaa mengii mnoo mpaka anakosa muda wa kwenda kwenye ibada,kusoma bibilia na
kufanya tafakar" aliendelea kusema "kuliko niendelee na kazi ambayo inaniweka mbali na Mungu halafu nikafa naiacha bora niache nikamtumikie Mungu" Akamwambia baba yake nataka kwenda kujiunga na mabrother niwe nasali mda wote. Akapelekwa.Lakini siku moja akarudi nyumban.

Alipoulizwa akasema kule nilifikiri ni sehemu ya kusali, kuimba na kusoma bibilia mda wote kumbe hapana. Bora nirudi nifanye mda wangu wote wa sala. Siku ya jumapili alienda kanisani na hakurudi nyumbani Alitafutwa kila mahali hakupatkana,Taarifa zilipelekwa mpaka kanisan na kituo cha polisi, Ni mwezi sasa umepita.

Jana taarifa za wazee wanaopasua mbao katikati ya msitu zikasema kuna mtu ameonekana alifariki mda
mrefu na ana bibilia. Taarifa zilipotufikia basi baba
yake anaondoka na polisi leo kuelekea msituni
wakiongozwa na wale wazee wapasua mbao.

Msitu upo Kule katangara,mwisho wa watu kuishi
unaingia ndani mwendo wa masaa manne. Kuna
barid kali sana na wanyama wakali pia. Ndipo
wakamkuta Godiwin amepiga magoti kwenye
gogo, akiwa na Rozary yake shingoni na biblia ipo
chini imefunguliwa kitabu cha SIRA. Godiwin ameshaoza amebaki mifupa tuu na hatoi harufu yoyote. Amevalia nguo zake vilevile. Godiwin alienda msituni kufunga na kusali mpaka akafariki.

Polisi na baba yake wakamchukua na kumpeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti kule Huruma hospital.

Taratibu za mazishi zinaendelea.Godiwin aliamua kujitoa kutuombea na kusali na Mungu aliamua tunapomtafuta tusimkute mpaka mapenz yake yatimie.Basi ni majonzi kwa familia na wazazi na wahitimu na wanafunzi wa kisale secondary, wananchi wote wa mashati rombo,kanisa Katoliki na watanzania wote kwa ujumla.

Tumuombee Godwin wakati huu akiwa na malaika na watakatifu mbinguni makao ya kusali na kumsifu
Mungu milele yote.

C&P
RIP A real believer!
 
Religion's bondage has killed more people and other animals more than anything!

Religious people are dangerous,their righteous than thou arrogance is beyond this peaceful world!

Fvck em!
The world will Fvck u too brother dont you worry a thing.
 
Poleni! Lakini ni vyema sana kama tutatafuta kulijua kusudi la Mungu juu ya zawadi hii ya Uhai aliyotupa bure!! Tukumbuke pia kuwa Mungu hakuishia kutupa uhai tu,bali pia alitupatia vitu vyote muhimu vitakavyotuwezesha kuutunza na kuustawisha uhai huo kama vile Akili,chakula,mavazi na dawa pia! Na hakuishia hapo tu bali pia alitupa uwezo wa kuzaa na kuongezeka ili kuijaza dunia na kuitiisha!! Akampa baba yetu Adam bustani nna maagizo ya kuwa aitunze(kazi) sasa hivi tukifikiri kwa kina juu ya kusudi la Mungu kwetu tutafikia mahali tukubaliane kuwa Mungu alituumba tu ili tuje kusali,kusoma neno lake,na kufunga kula na kunywa hadi tufe??? Kwamba Mungu atafurahi ikiwa binaadam wote wataifuata njia hiyo ya Godwin ya kutofanya kazi,kutokula wala kunywa hadi kifo kitufike? Je dunia yake aliyotuumbia tuijaze na kuitiisha itastawi kwa mwendo huo?? imani inapaswa kwenda sambamba na uelewa thabiti juu yake!! Vinginevyo tutaishia kufanya mambo ya kumshangaza Mungu tukidhani ndiyo tunamfurahisha!! Godwin amekwepa wajibu muhimu sana kwa Mungu na kwa dunia ya Mungu!! Godwin ameonyesha ubinafsi wa kujitazama yeye tu akiwa mbinguni bila kuwajali ndugu na jamaa zake wengine watakaobaki na majonzi ya kupoteza mpendwa wao! Amemnyima Mungu utukufu na sifa ambazo angeendelea kumpa angelikuwa hai na ndiyo maana biblia inakataza kujiua! Yeye amejiua kwa makusudi! Amefanya dhambi!! Mungu amsamehe!
Umenena vyema. Kusudi LA Mwenyezi MUNGU kwa wanadamu Ni kuabudu; na kuabudu Ni zaidi ya kusali na kufunga. Kuabudu Ni kusaidia wengine wamjue Mwenyezi MUNGU, Ni kutafuta riziki kwa njia halali, Ni kusaidia wajane, mafukara na masikini, na mengi mengineyo. Godwin amekimbia majukumu, akaliona LA kufunga na kusali tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
b1b85778530e45c6bc23d1345374c724

Rombo. Mwili wa kijana mwenye umri wa miaka 25 umepatikana katika msitu wa Katangara chini yake kukiwa na Biblia, huku ukiwa umevaa rozari shingoni na umepiga magoti.

Kijana huyo, Godwin Massawe, mkazi wa Kijiji cha Msaranga wilayani Rombo ambaye alitoweka Jumapili ya Januari 20 baada ya kuaga kuwa anakwenda kanisani, mwili wake ulikutwa porini Machi Mosi.

Baba mzazi wa kijana huyo, Frimin Massawe aliliambia Mwananchi jana kuwa, baada ya mwanaye kutoweka alitoa taarifa polisi na kanisani ili asaidiwe kupatikana kwake.

“Tulipeleka taarifa polisi mpaka kanisani, lakini hatukufanikiwa. Jana (juzi) nililetewa taarifa na wazee wanaopasua mbao katikati ya msitu (wa Katangara) wakasema kuna mtu ameonekana amefariki (dunia) muda mrefu,” alisema Massawe.

Alisema watu hao walimweleza kuwa marehemu amepiga magoti akiwa na Biblia huku amevaa rozari, ndipo alipoongozana nao kwenda polisi na baadaye msituni.

“Tukafika hadi Katangara na kuingia ndani (ya msitu) mwendo wa saa nne. Kule kulikuwa na baridi kali sana na wanyama wakali, lakini bado niliona maajabu ya Mungu.”

Alisema, “Huwezi amini nilimkuta mwanangu Godwin amepiga magoti kwenye gogo akiwa na rozari yake shingoni na Biblia ipo chini imefunguliwa kitabu cha Joshua huku akiwa ameoza.”

Mzazi huyo alisema mabaki ya mwili huo yalikuwa hayatoi harufu, jambo alilodai kuwa ni ‘muujiza’.

Baba mdogo wa marehemu, Simon Massawe alisema tukio hilo limewashangaza na kama familia wameumia kwa kuwa kijana wao alikuwa mtu wa maombi muda mwingi.

“Sisi kama familia tumelipokea kwa huzuni kubwa, hatukutegemea kumkuta amekufa. Ila kama amekufa kiimani let it be (acha iwe hivyo),” alisema.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Hamis Issah alisema mwili wa kijana huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Huruma iliyopo wilayani Rombo.

Mwananchi
 
Hizi pbm haziwakuti maskini tu..ukiwa mpenzi wa kusoma soma majarida ya wenzetu wazungu wanaongoza kwa hii shida..!hata matajiri zinawakuta sana zaidi!8
Matajiri wengi hiyo hali huwakuta hasa wakiwa na stress za madeni ya kampuni , Upinzani mkubwa wa kibiashara ambao huwa hawajui solution nk mfano bilionea wa viwanda vya simenti duniani na mwenye hisa kubwa twiga Cement pia alijiua kisa hisa zake kuporomoka mfululizo masoko ya hisa.Stress management kwa maskini , Matajiri , wafanyakazi,wakulima na watoto ni kitu cha muhimu.Mkulima hata mkubwa hiyo hali yaweza mkumba mfano amelima hekari elfu kumi za mahindi mvua ikagoma kunyesha mazao yote yakakauka.Kumkuta akisali mfululizo na hataki kulima tena anatamani kusali na kwenda mbinguni tu usishangae.Kifupi huyo kijana alikuwa na stress ambazo hazikuwa managed
 
b1b85778530e45c6bc23d1345374c724

Rombo. Mwili wa kijana mwenye umri wa miaka 25 umepatikana katika msitu wa Katangara chini yake kukiwa na Biblia, huku ukiwa umevaa rozari shingoni na umepiga magoti.

Kijana huyo, Godwin Massawe, mkazi wa Kijiji cha Msaranga wilayani Rombo ambaye alitoweka Jumapili ya Januari 20 baada ya kuaga kuwa anakwenda kanisani, mwili wake ulikutwa porini Machi Mosi.

Baba mzazi wa kijana huyo, Frimin Massawe aliliambia Mwananchi jana kuwa, baada ya mwanaye kutoweka alitoa taarifa polisi na kanisani ili asaidiwe kupatikana kwake.

“Tulipeleka taarifa polisi mpaka kanisani, lakini hatukufanikiwa. Jana (juzi) nililetewa taarifa na wazee wanaopasua mbao katikati ya msitu (wa Katangara) wakasema kuna mtu ameonekana amefariki (dunia) muda mrefu,” alisema Massawe.

Alisema watu hao walimweleza kuwa marehemu amepiga magoti akiwa na Biblia huku amevaa rozari, ndipo alipoongozana nao kwenda polisi na baadaye msituni.

“Tukafika hadi Katangara na kuingia ndani (ya msitu) mwendo wa saa nne. Kule kulikuwa na baridi kali sana na wanyama wakali, lakini bado niliona maajabu ya Mungu.”

Alisema, “Huwezi amini nilimkuta mwanangu Godwin amepiga magoti kwenye gogo akiwa na rozari yake shingoni na Biblia ipo chini imefunguliwa kitabu cha Joshua huku akiwa ameoza.”

Mzazi huyo alisema mabaki ya mwili huo yalikuwa hayatoi harufu, jambo alilodai kuwa ni ‘muujiza’.

Baba mdogo wa marehemu, Simon Massawe alisema tukio hilo limewashangaza na kama familia wameumia kwa kuwa kijana wao alikuwa mtu wa maombi muda mwingi.

“Sisi kama familia tumelipokea kwa huzuni kubwa, hatukutegemea kumkuta amekufa. Ila kama amekufa kiimani let it be (acha iwe hivyo),” alisema.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Hamis Issah alisema mwili wa kijana huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Huruma iliyopo wilayani Rombo.

Mwananchi
Wewe JOSHUA huku ameoza .....mwenzako nae SIRA huku ameoza haya

Haya bhana maendeleo hayana chama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kifupi ni kuwa ukiona mtu wa kawaida hataki kufanya kazi au kusoma kutwa yuko anasoma vitabu vya dini tu na kushinda makanisani au misikitini wakati ni tegemezi kwa wengine kwa mahitaji ya maisha ujue huyo ana tatizo la kisaikolojia kubwa kama alilokuwa nalo huyo kijana.A anatakiwa kupewa tiba ya kisaikolojia kwa upole Akifokewa aweza tokomea porini kama huyo kijana kwa kuona kuwa hata Familia ni wapagani wapinga mtu wa Mungu anayeshinda akisali!!! Wakati wao wanaendekeza kazi za kufufua!!! Anajisemea Kuwa Heri nikajikalie peke yangu na Mungu Porini nikisali wasininyanyase na chakula chao na huduma wanazonipa ambavyo ni vitu vya duniani tu.Niko tayari kukaa na Mungu Porini.
 
Alisema, “Huwezi amini nilimkuta mwanangu Godwin amepiga magoti kwenye gogo akiwa na rozari yake shingoni na Biblia ipo chini imefunguliwa kitabu cha Joshua huku akiwa ameoza.”

Mzazi huyo alisema mabaki ya mwili huo yalikuwa hayatoi harufu, jambo alilodai kuwa ni ‘muujiza’.

Hakuna muujiza hapo, suala ni kwamba huyu kijana alienda porini kufunga na kuomba, na akafa kwa hypothermia kutokana na baridi kali ambayo ilimfanya apate kitu kama usingizi akiwa katikati ya maombi na hakuamka tena.

Na suala la kutonuka ni kutokana na uhifadhi wa baridi kali pia - kwani ukiweka vitu kwenye friji vinatoa harufu ya kuharibika?

Watu tuwe na kiasi katika mammbo haya. Tusiwe moto sana wala baridi.
 
Ukonl sahihi mwili wake hauwezi nuka sababu uko eneo la baridi Kali ni kama ulikuwa kwenye freezer kutonuka sio muujiza huo
 
Back
Top Bottom