Rombo; Kilimanjaro Baba aua mtoto wake na Kisha kuchimba shimo na kumfukia

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
10,414
Reaction score
18,438
Baba mmoja ajulikanae Kwa jina la Edward mwenye umri mwenye umri wa miaka 66 anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Rombo kwa kosa la kumuua mtoto wake wa kiume Kwa shoka na Kisha kuchimba shimo na kumzika mwenyewe usiku.

Hali ya Taaharuki imeikumba Kijiji Cha Kilema katika kata ya Olele,tarafa ya mashati wilayani Rombo baada ya baba Mmoja ajulikanae Kwa jina la Edward kumuua mwanae wa kumzaa ajulikanae Kwa jina la Oscar mwenye umri wa miaka 40.

Hali inayooendelea muda huu kijijini hapa ni kuwa polisi wanafukua shimo alilofukiwa kijana huyo wakati Baba mzazi akiwa tayari kituo Cha polisi Kwa ajili ya Taratibu nyingine.

Hali jinsi ilivokuwa Hadi kujulikana....

Jana jioni Mzee Edward akiwa kwenye pombe baada ya pombe kumkolea ndipo alipomueleza mama mmoja ambae alikuwa anakunywa nae pombe hapo kilabuni. Ndipo mama huyo alipoita watu na kuwaelezea na Kisha watu hao kumuhoji Baba huyo na ndipo walipopiga simu polisi.

Majirani wanasema kuwa Baba huyo alikuwa akiishi yeye na mwanae huyo ambae Sasa ni marehemu na kwamba Mke wa Mzee Edward alishafariki siku nyingi.
 
Binadamu tumekua katili zaidi ya wanyama.
Sad Feelings GIF.gif
 
Duuuh, hatari Sana, hivi kijana wa 40 years bado upo Kwa baba?, au NI nyumba ya kijana anamlea Baba Yake?

Vipi kijana hakuwa na make???
Unajua mila na maisha ya uchagani? Wachaga wana mashamba ya ndizi + kahawa yanayoitwa ''vihamba'' ambako hujenga nyumba. Mara nyingi, mtoto wa kwanza wa kiume ndiye anarithishwa hilo eneo na kama mama yake na baba yake bado wako hai, anakaa nao na kuwatunza. Wazazi na mtoto wanakuwa na nyumba tofauti zinazojengwa kwenye hilo shamba.
 
Baba mmoja ajulikanae Kwa jina la Edward mwenye umri mwenye umri wa miaka 66 anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Rombo kwa kosa la kumuua mtoto wake wa kiume Kwa shoka na Kisha kuchimba shimo na kumzika mwenyewe usiku.

Hali ya Taaharuki imeikumba Kijiji Cha Kilema katika kata ya Olele,tarafa ya mashati wilayani Rombo baada ya baba Mmoja ajulikanae Kwa jina la Edward kumuua mwanae wa kumzaa ajulikanae Kwa jina la Oscar mwenye umri wa miaka 40.

Hali inayooendelea muda huu kijijini hapa ni kuwa polisi wanafukua shimo alilofukiwa kijana huyo wakati Baba mzazi akiwa tayari kituo Cha polisi Kwa ajili ya Taratibu nyingine.

Hali jinsi ilivokuwa Hadi kujulikana....

Jana jioni Mzee Edward akiwa kwenye pombe baada ya pombe kumkolea ndipo alipomueleza mama mmoja ambae alikuwa anakunywa nae pombe hapo kilabuni. Ndipo mama huyo alipoita watu na kuwaelezea na Kisha watu hao kumuhoji Baba huyo na ndipo walipopiga simu polisi.

Majirani wanasema kuwa Baba huyo alikuwa akiishi yeye na mwanae huyo ambae Sasa ni marehemu na kwamba Mke wa Mzee Edward alishafariki siku nyingi.
Kwamba dogo alikuwa anadai urithi au?!!
 
Wajomba zangu ni watu wakubwa bwashee nikikutajia unaweza sema ni chai ila nikukuthibitishia unaweza tetemeka😅😅 baba yangu japo hakua na kitu ila hakua Fala kuoa familia za kizembe🤣
Kama ni hivyo mzee alicheza kama pele

Hongera kwake

Lakin nimekuchek kule juu ndugu yangu angalia
 
Back
Top Bottom