Roho za mauti: Ni kitu gani hiki?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,754
Mauti ni kifo na kifo ni kikomo cha kuwa(end of existence)! Mauti yapo ya aina nyingi lakini makubwa yapo ya aina mbili
. Mauti ya jumla(mauti ya moja kwa moja)
. Mauti nusu (mauti dhana)
Roho ni kitu kisichokufa bali roho ndani ya mwili ndio huleta uzima au kifo.. Roho ndani ya mwili ni uhai na roho nje ya mwili ni kifo cha mwili...!

Kumbuka mada hizimazishi ya mtu kishirikina
roho ya kukataliwa chanzo na madhila yake
kuna familia zina laana ya asili

Tukiachana na mauti kubwa ile ya roho kutengana na mwili kuna hizi mauti nyingine
Mauti/kifo cha mapenzi
Mauti/kifo cha biashara
Mauti/kifo cha wazo nknk
Unapoandamwa na roho za mauti ambazo zina asili mbili
. Mapito ya maisha
. Matendo ya binadamu

Mambo yako mengi huharibika hakuna kinachosonga, hakuna kinachotimia na hakuna kinachokuletea tija...!
Huna ndoa ama kila ndoa yako haidumu
Huna mtoto mimba zinaharibika
Huna kazi na ukipata haidumu
Huna kipato na ukipata kinaishia kusikoeleweka ama matumizi ya hovyo!
Biashara unazijaribu zinakufa
Mawazo yako mazuri hayatimii lakini kwa wengine wakijaribu inatiki

Familia inaandamwa na mikosi ya kila aina. Magonjwa ajali na vifo visivyoeleweka.

Roho za mauti zinakuwa zimekuandama kila kona na pakutokea hupaoni wala hupajui.

Unapiga picha ya familia yako na ukoo wako ..unapiga picha ya familia nyingine na koo nyingine.. Vimeachana mbali kabisa.. Hujui suluhu na hujui ulipokosea/mlipokosea

Ni katikati ya matatizo yako hayo wanatokea washauri wabaya..washauri wa kukwambia ukasafishe nyota kwa wazee wa 'busara' ama wakakuzindue nknk...Wachache sana wanaweza kukusaidia lakini wengine watazidi kukuongezea matatizo

Roho nyingi za mauti hazisababishwi na washirikina. Nyingi hutokana na sisi wenyewe ... Matendo yetu na hata lugha zetu.. Kuneneana mabaya, kuapizana...nknk

Ugomvi wa ndugu ndani ya familia na ndani ya koo ni mbaya sana..kwasababu hutembea na vizalia ndani ya DNA.. Kuna muunganiko usiokoma..visasi hurithishwa toka kizazi hadi kizazi. Na ubaya wa hivi visasi huzaliwa, hukua na kukomaa na kuzaliana

Kwa ushauri wangu.. Nitoe rai kama wewe ni mmojawapo unayopitia haya.. Angalia familia yako na ukoo wako.. Je kuna mahali wazee wenyu ama wakubwa wenyu walishatofautiana mahali na kuapizana maagano mabaya ya visasi na kuua undugu?

Unaweza ukawa unateseka sasa kumbe makosa yalikuwa ya wengine...Na la muhimu sana wewe uliyenusurika na haya muombe sana Mungu akunusuru usije kuangukia kwenye ugomvi wa ndugu usio na suluhu.. Na wala hata kama mkitofautina msije mkafikia hatua ya kuapizana na kuneneana mabaya.. Mnazalisha roho za mauti na mapepo vitakavyokuja kuwatesa wengine
Msamaha na kutengeneza ni bora kuliko visasi na maagano...TENGENEZA SASA!
 
Mauti ni kifo na kifo ni kikomo cha kuwa(end of existence)! Mauti yapo ya aina nyingi lakini makubwa yapo ya aina mbili
. Mauti ya jumla(mauti ya moja kwa moja)
. Mauti nusu (mauti dhana)
Roho ni kitu kisichokufa bali roho ndani ya mwili ndio huleta uzima au kifo.. Roho ndani ya mwili ni uhai na roho nje ya mwili ni kifo cha mwili...!

Kumbuka mada hizimazishi ya mtu kishirikina
roho ya kukataliwa chanzo na madhila yake
kuna familia zina laana ya asili

Tukiachana na mauti kubwa ile ya roho kutengana na mwili kuna hizi mauti nyingine
Mauti/kifo cha mapenzi
Mauti/kifo cha biashara
Mauti/kifo cha wazo nknk
Unapoandamwa na roho za mauti ambazo zina asili mbili
. Mapito ya maisha
. Matendo ya binadamu

Mambo yako mengi huharibika hakuna kinachosonga, hakuna kinachotimia na hakuna kinachokuletea tija...!
Huna ndoa ama kila ndoa yako haidumu
Huna mtoto mimba zinaharibika
Huna kazi na ukipata haidumu
Huna kipato na ukipata kinaishia kusikoeleweka ama matumizi ya hovyo!
Biashara unazijaribu zinakufa
Mawazo yako mazuri hayatimii lakini kwa wengine wakijaribu inatiki

Familia inaandamwa na mikosi ya kila aina.. Magonjwa ajali na vifo visivyoeleweka
Roho za mauti zinakuwa zimekuandama kila kona na pakutokea hupaoni wala hupajui
Unapiga picha ya familia yako na ukoo wako ..unapiga picha ya familia nyingine na koo nyingine.. Vimeachana mbali kabisa.. Hujui suluhu na hujui ulipokosea/mlipokosea

Ni katikati ya matatizo yako hayo wanatokea washauri wabaya..washauri wa kukwambia ukasafishe nyota kwa wazee wa 'busara' ama wakakuzindue nknk...Wachache sana wanaweza kukusaidia lakini wengine watazidi kukuongezea matatizo

Roho nyingi za mauti hazisababishwi na washirikina... Nyingi hutokana na sisi wenyewe ... Matendo yetu na hata lugha zetu.. Kuneneana mabaya, kuapizana...nknk

Ugomvi wa ndugu ndani ya familia na ndani ya koo ni mbaya sana..kwasababu hutembea na vizalia ndani ya DNA.. Kuna muunganiko usiokoma..visasi hurithishwa toka kizazi hadi kizazi. Na ubaya wa hivi visasi huzaliwa, hukua na kukomaa na kuzaliana

Kwa ushauri wangu.. Nitoe rai kama wewe ni mmojawapo unayopitia haya.. Angalia familia yako na ukoo wako.. Je kuna mahali wazee wenyu ama wakubwa wenyu walishatofautiana mahali na kuapizana maagano mabaya ya visasi na kuua undugu?

Unaweza ukawa unateseka sasa kumbe makosa yalikuwa ya wengine...Na la muhimu sana wewe uliyenusurika na haya muombe sana Mungu akunusuru usije kuangukia kwenye ugomvi wa ndugu usio na suluhu.. Na wala hata kama mkitofautina msije mkafikia hatua ya kuapizana na kuneneana mabaya.. Mnazalisha roho za mauti na mapepo vitakavyokuja kuwatesa wengine
Msamaha na kutengeneza ni bora kuliko visasi na maagano...TENGENEZA SASA!
Hi mada ni nzito mno inahitaji akili kubwa kuielewa....
 
Kuna familia na koo hazizikani
Kuna familia na koo hazisilimiani
Kuna familia na koo hazipendani kabisa...
Hawa ndio wanadhoofisha na kuua kabisa kinga na nguvu za kiroho...badala ya kufanya ya maana ni kuwindana na kutakiana mabaya kila upande bila kujua wanajidhuru wao wenyewe kwakuwa wana muunganiko wa kiroho
 
giphy.gif
 
This is yet another best thread from our great man Mshana Jr. Heri na baraka nyingi kwako mkuu.
Hii inatukumbisha umuhimu wa kusamehe na kuondoa chuki na vinyongo katika mioyo yetu.
Pamoja na hatua zilizopendekezwa na wajumbe wengine, vitendo vya utoaji wa zaka na sadaka, kusaidia wahitaji kunaweza kuwa na nafasi kubwa sana ya kuweka mambo vizuri.
 
Blessed
 
Msingi bora ngazi ya familia huepusha mengi
 
Kuna familia na koo hazizikani
Kuna familia na koo hazisilimiani
Kuna familia na koo hazipendani kabisa...
Hawa ndio wanadhoofisha na kuua kabisa kinga na nguvu za kiroho...badala ya kufanya ya maana ni kuwindana na kutakiana mabaya kila upande bila kujua wanajidhuru wao wenyewe kwakuwa wana muunganiko wa kiroho
Hapa kwenye familia hazisalimiani ni mtihani kwa kweli. Ndugu hawapendani, ndugu hao hao huamisha chuki kwa watoto mpaka mtoto wa ma mdg na ma mkubwa hamuwezi kukaa pamoja. Hii inanitesa sana. Hata ukijaribu kuwaeleza wazazi hawaelewi. Unafanya nini tena ukiwa umejaribu kila njia mshikane
 
Msamaha huanzia kwako...usiweke vifundo usiweke visasi usiweke vinyongo..ni lazima kuwe na starting point... Kumbuka ni kwa kusamehe ndio tunasamehewa, tunasameheka!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom