'nimesoma gazeti la jambo leo limemnukuu nape akisema roho yake ameikabidhi kwa mungu katika wakati huu mgumu wa vita dhidi ya mapapa ccm
Sijui kwa nini hakuleta habari kamili soma hii kutoka Raia Mwema.Da! Mkuu Achebe mbona short cut sana kiongozi??
Kikwete aipa nguvu Sekretariati mpya
Katika kikao hicho cha CC, Rais Kikwete alirudia kuipa nguvu Sekretarieti ya chama hicho kwa kuwapinga moja kwa moja wanaoibeza wakiwamo baadhi ya wenyeviti wa mikoa ambao wamekuwa wakisema inapotosha uamuzi wa NEC.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, Rais Kikwete alitamka ndani ya kikao cha Kamati Kuu akisema; "there are some stupid guys (wajinga fulani)," wanaosema Sekretariati hiyo inakivuruga chama kwa namna wanavyosimamia utekelezaji wa uamuzi wa NEC; hasa wa kujivua gamba.
Katika kile kinachoweza kutafsiriwa moja kwa moja kuwa ni kuwapuuza baadhi ya viongozi wanaodai kuwa Sekretariati imekuwa ikisimamia uamuzi wa kujivua gamba, kinyume cha matakwa ya Halmashauri Kuu, Kamati Kuu imeipongeza Sekretariati hiyo.
Hatua hiyo inatajwa kuwa ni pigo kwa baadhi ya viongozi wa sasa wa chama hicho, wakiwamo wanaopaswa kujiuzulu nafasi za uongozi katika chama hicho - Chenge na Lowassa; huku Rostam naye akijiuzulu kwa kulalamikia Sekretariati hiyo akisema inaendesha siasa uchwara.
Wengine katika orodha ya kuishambulia Sekretariati hiyo na hasa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ni John Guninita, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM-Dar es Salaam na Hamisi Mgeja Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, wote wakitajwa kuwa karibu na viongozi wanaotakiwa kujiuzulu.
Taarifa kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu zinaeleza kuwa Rais Kikwete ni kati ya viongozi walioweka wazi msimamo wao kuhusu mwenendo wa Sekretariati, akimtaja kwa jina Nape Nnauye.
<br />kigeu geu .. wananigeukia <br />
kigeu geu wananigeukia
We mungu kaona naye wapi? mpaka amkabidhi ROHO YAKE.?Nimesoma gazeti la JAMBO Leo limemnukuu Nape AKISEMA Roho yake ameikabidhi kwa MUNGU katika wakati huu MGUMU WA vita dhidi ya mapapa CCM
Mwenye madhambi/ufisadi wake ( nape) auanike hapa tuuone