Roboti moja 'yageuka mtu nchini Urusi

maforce

JF-Expert Member
Mar 18, 2017
660
615
_104755442_robotman.gif
Haki miliki ya pichaMBK MEDIAImage caption"Roboti" mtu au mtu Roboti!
Roboti moja iliyokuwa kwenye tamasha la maonesho yaliyofadhiliwa na taifa ilishangaza wengi kwa uwezo wake wa juu.

Roboti Boris aliyeonyeshwa katika kipindi cha runinga nchini humo, alionesha uwezo mkubwa wa kutembea, kuongea na kucheza dansi.

Lakini muda mfupi baadaye, waandishi habari wakahoji uwezo mkubwa wa roboti hiyo.

Katika picha ambayo ilichapishwa baadaye kwenye mitandao ya kijamii, shingo ya binadamu, ilionekana bayana.

Loh, ukweli ukabainika kuwa halikuwa roboti bali mtu aliyevalia magwanda ya plastiki tu.

Vazi hilo liitwalo Alyosha the Robot, lililoundwa na kampuni iitwayo Show Robots na linagharimu dola 2,975.

_104770818_76e4646d-9708-4be9-9b2f-7b320f3d2f67.gif
Haki miliki ya pichaSHOW ROBOTSImage captionMagwanda ya roboti yazua taharuki kubwa, huku baadhi ya watu wakiamini kuwa ni roboti kamili
Huku waandalizi wa tamasha la teknolojia ya Proyektoria - wakiwalenga vijana chipukizi katika maonyesha hayo, wakiwa bado hawajatangaza kuwa kwa hakika hilo lilikuwa Roboti- matangazo ya runinga ya Russia-24, yalitangaza kuwa ni roboti halisi.

Tovuti ya mtandao wa TJournal nchini Urusi, ndio iliyokuwa ya kwanza kushuku iwapo hiyo ilikuwa ni roboti halisi au la....ikiuliza maswali chungu nzima ikiwemo:

  • Ni kwa nini muundo wa roboti hiyo haina vifaa vya kutuma na kupokea ujumbe maarufu kama sensors?
  • Jinsi gani wanasayansi wa Urusi walifaulu kuunda roboti haraka hivyo, huku kukiwa hakuna taarifa au ripoti zozote zilizochapishwa kwenye vyombo vya habari kuhusiana na maandalizi ya uundaji.
  • Je, mbona hakuna taarifa zozote za utalamu huo wa kisasa kwenye mitandao ya kijamii?
  • Mbona roboti ilikuwa ikifanya ishara nyingi pale lipokuwa ikicheza muziki?
  • Kwanini ilikuwa na umbo ambalo binadamu anaweza kuingia ndani na kutoshea barabara?
  • Kwanini sauti yake ilikuwa imerekodiwa badala ya kutoa sauti moja kwa moja mbele ya umati?
Katika tovuti ya kampuni hiyo iliyounda vazi hilo la Alyosha Robot, bidhaa hiyo inaelezewa kama iliyo na uwezo "sawa kabisa na roboti halisi".

SOURCE:BBC NEWS
 
Back
Top Bottom