JAMII-ASM
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 1,305
- 524
Mara ya kwanza nilipoina video ya huyu robot sikuamini macho yangu,kwamba sasa binadamu sio tu ameanza kuunda robot yenye uwezo wa kutembea lakini pia ina uwezo wa kufikiri haraka na kuchukua maamuzi ambayo hayana tofauti na maamuzi ya kiumbe mwenye uwezo mkubwa sana wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi.
Huyu robot anaitwa Atlas, katengenezwa na GOOGLE kupitia kampuni wanayoimiliki inayoitwa Boston Dynamics.
Huyu Atlas anauwezo wa kufungua mlango ,kubeba mizigo , kutembea msituni,kwenye barafu na kwenye miteremko.
Kwa uwezo mkubwa alionao anaweza kutumika katika mazingira hatarishi,kama uokozi kwenye matukio ya moto, mashambulizi ya kigaidi n.k.
Lakini robot huyu anaweza kutumiwa kudhuru, kwa kum-program na kumpa silaha au mabomu. Atlas anafanana sana na Cyborg.
Google Schaft