Robert Mugabe: Raila Odinga akikanyaga Zimbabwe nitamkamata na kumhasi

Status
Not open for further replies.

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amemshambulia kwa maneno mwanasiasa mkongwe wa Kenya ambaye pia ni kiongozi wa chama cha CORDS huku akimpiga marufuku kukanyaga ardhi ya nchi hiyo.

Akizungumza huko Marondela katika hafla iliyowahusisha wanajeshi walioshiriki katika vita mbalimbali, Mugabe alimtuhumu Raila kwa kutaka kumpindua kwenye nafasi yake kwa kuwapandikiza wapinzani nchini humo.

Hivi ndivyo alivyosema:

"Raila Odinga ni mwanasiasa muongo wa Kenya, mwanaume mnafiki ambaye yuko katika mkakati wa kuwapandikiza marafiki zake kuwa marais kwenye nchi zote za Afrika ili awe mwenyekiti mwenye nguvu kwenye Umoja wa Afrika (AU), siku moja watamuangusha kwenye sanduku la kura.

"Angalia alichokifanya Nigeria, Tanzania, Ivory Coast na anataka kufanya hivyo pia Uganda kwa kumtumia rafiki yake Kiiza Besigye ambaye leo anapewa sifa na ushupavu ambao anapata kutokana tu na amri za Raila barani Afrika.

"Hapa hatutamruhusu kuwageuza marafiki zake wa zamani Tendai Biti na Morgan kuniondoa mimi, hakuna kwa namna yoyote. Nitatawala kwa miaka 90 zaidi. Nimekiamuru kikosi maalum cha jeshi kuangusha ndege yoyote itakayokuwa imembeba huyo mwendawazimu Raila na kundi lake la mipango ya uchakachuaji wa kura dhidi ya marais wanaoendelea kutawala Afrika.

"Nimewaamuru walinzi wangu kuhakikisha wanakuwa makini kuhakikisha Raila hajipenyezi bila kubainika.

"Tutashindwaje kukosa usingizi kwa sababu tu ya Raila, yeye ni kitu gani? Tutamkamata na kumhasi kabla yeye na timu yake hawajamsaidia Morgan na Biti kunipindua kwenye Urais."

Hii sio mara ya kwanza kwa Mugabe kushambulia Kenya kwa maneno, wiki chache zilizopita alidai kuwa wananchi wa Kenya ni wezi kutoka damuni na kwamba anadhani wanasomea shahada ya wizi. Alitahadharisha wananchi wake kutokubali kukaa karibu na wakenya kwa madai kuwa wanaweza kuwaambukiza wizi.

Mwezi Juni mwaka 2008, Raila Odinga aliwasilisha pendekezo lake mbele ya Umoja wa Afrika akitaka Umoja huo kumsimamisha uanachama Rais Mugabe hadi pale atakaporuhusu uchaguzi wa huru na haki nchini kwake.


Zimbabwe's President Robert Mugambe has banned CORD's Leader Raila Odinga from visiting Zimbabwe. He has ordered the much feared Anti-Terror Police to keep a keen eye to ensure the CORD Leader does not sneak in the Country to inspire Opposition and plot his defeat.

Speaking at a function in Marondera, where he was addressing the war veterans of the Independence Struggle, President Mugambe was clear through his speech while punching the air with his left fist…

"Raila Odinga is a rogue politician from Kenya, a treacherous man who is on a mission to plant his friends as Presidents all over Africa so that he become a powerful AU Chairman, one day should they defeat him there in the ballot. See what he did in Nigeria, Tanzania, Ivory Coast and is on the verge of doing so in Uganda with his Kiiza Besigye who today has achieved a Cult-like status with near fanatical support that only Raila commands in the whole of Africa.

Here we will not at all let him turn his erstwhile friends Tendai Biti or Morgan to kick me out; No way, I will rule for 90 more years. I have ordered the Airforce to down any plane carrying that Lunatic Raila and his gang of ballot Coup plotters against sitting Presidents in Africa. I have ordered the border Guards to be very keen to ensure Raila doesn't sneak through undetected", he said, amid cheers from War Veterans.

"How can we miss to sleep just because of Raila, who the hell is he and who does he is ?. We will arrest him and Castrate him long before he (and his Team) helps Morgan or Biti to overthrow me as President", Concluded Mugabe amid cheers of "ban ! ban ! ban !" from the War Veterans.

Source: I will castrate you if you step foot in Zimbabwe
 
Mugabe alivowaponda Wakenya watu walifurahi sana sijui na leo wanafurah tena,hivi odinga ameifanya nini Tanzania mbona comrade mugabe anasema "see what he did in Tanzania?
 
Labda kuna kitu kaona maana ni mwanasiasa huyu tena miongoni mwa wanasiasa wasomi kupita wetu hapa ana degree saba
 
kuna tuhuma kwamba vijana wa IT wa Raila walikuwa wamepangiwa Golden tree hotel kumsaidia ma komeo
 
Mugabe alivowaponda Wakenya watu walifurahi sana sijui na leo wanafurah tena,hivi odinga ameifanya nini Tanzania mbona comrade mugabe anasema "see what he did in Tanzania?
Rafiki yake Magufuli ameteuliwa kuwa rais wa TZ
 
kwa kauli hii, nadhani ni kweli amezeeka. halafu anatukosea adabu watz, tumeheshimiana naye sana tangu uhuru sana naona anaanza kutuzoea vibaya. anawezaje kusema rais wa tz amepandikizwa na raila?

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha. Umenivunja mbavu. Huyo babu naona anazeeka vibaya.
 
Ni habari za uongo wana JF zipuuzeni. Kenya kuna magazeti ya "satire" (yaani utani) ndo yameandika habari hizi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom