Kichwa Kichafu
JF-Expert Member
- Apr 13, 2017
- 44,604
- 188,819
Habari,
Robert Lewandowski amefungua mwaka vyema kwa kuendelea kushinda tuzo yake ya mchezaji bora wa mwaka zinazotokewa na FIFA ambapo alikuwa akichuana na washiriki wenzake ambao ni Lionel Messi na Mohammed Salah.
Lewandowski ameshinda tuzo ya FIFA ya mchezaji bora wa kiume kwa mwaka wa pili mfululizo sasa ambapo sherehe hizi zimefanyika makao makuu ya FIFA huko Zurich siku ya jumatatu leo 17.01.2022.
Mshambuliaji huyu wa Bayern Munich amewapiku waliokuwa wanawania tuzo hiyo ambao ni Lionel Messi na Mohammed Salah kama ilivyokuwa mwaka wa mwisho alivyochukua tuzo ya mchezaji bora wa FIFA December 2020.
Lewandowski alifunga magoli 58 katika mechi 47 kwenye mashindano yote mwaka 2021 ambapo kuliambatana na kuvunja rekodi mbili zilikuwa zikishikiliwa na mshambuliaji legendary wa kijerumani Gerd Muller. Ambazo ni kufunga magoli 41 ndani ya msimu mmoja wa Bundesliga katika timu ya Bayern Munich na magoli 43 ndani ya Bundesliga katika kalenda ya mwaka.
Hadi Sasa amekwisha funga magoli 34 ndani ya mechi 27 kwenye msimu huu, ukijumlisha magoli 9 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi.
Nawasilisha Mzee Mkoloni.
Cc: Kichwa Kichafu.