Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
RIZIKI NI MAJALIWA.
1
Haku muumba kilema, aka mkosesha mwendo
Huyo ni Mola Karima, mfalme wa vishindo,
Usijifanye yatima, fungua yako mafundo,
Rauka ufanye hima, nyumbani haliji windo.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
2
Mwenye kupewa ukwasi, katu hakupendelewa,
Fukara ondoa wasi, sababu hukuonewa,
Mitihani ya Qudusi, mola wa majaliwa,
Alichopewa pungusi, chaa hakuruzukiwa.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
3
Damka wahi kazini, upate yako ijara,
Changamoto za windoni, na zikufanye imara,
Toa simanzi moyoni, tena sifanye harara,
Bosi avimbe kichwani, tuli sipoteze dira.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
4
Subiri mja subiri, hebu acha kusonona,
Mzoee mwaajiri, kama wataka kunona,
Usimletee shari, japo dhiki waiona,
Naomba sitakabari, lisilo mwisho hakuna.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
5
Niseme nawaajiri, wenye pembe vichwani,
Wana kifanya kiburi, hawana heri moyoni,
Mbaya hawatafakari, shida hana maskani,
Tabu haina tajiri, wala si ya masikini.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
6
Ewe ndugu mwajiriwa, sema na wako moyo,
Jukumu ulilopewa, litimize pasi choyo,
Ridhika na unachopewa, shika wangu mgogoyo,
Rushwa katu si ngekewa, yataka ushinda moyo.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
7
Wote wategemeana, mwajiri na mwajiriwa,
Kubwa kuheshimiana, mwerevu kanielewa,
Pia mkiaminiana, kazi haitachezewa,
Tara mkifanyiana, lengo halitafikiwa
Riziki ni majaliwa, kuipata si ngekewa.
Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5.)
Whatspp/call 0622845394 Morogoro
1
Haku muumba kilema, aka mkosesha mwendo
Huyo ni Mola Karima, mfalme wa vishindo,
Usijifanye yatima, fungua yako mafundo,
Rauka ufanye hima, nyumbani haliji windo.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
2
Mwenye kupewa ukwasi, katu hakupendelewa,
Fukara ondoa wasi, sababu hukuonewa,
Mitihani ya Qudusi, mola wa majaliwa,
Alichopewa pungusi, chaa hakuruzukiwa.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
3
Damka wahi kazini, upate yako ijara,
Changamoto za windoni, na zikufanye imara,
Toa simanzi moyoni, tena sifanye harara,
Bosi avimbe kichwani, tuli sipoteze dira.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
4
Subiri mja subiri, hebu acha kusonona,
Mzoee mwaajiri, kama wataka kunona,
Usimletee shari, japo dhiki waiona,
Naomba sitakabari, lisilo mwisho hakuna.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
5
Niseme nawaajiri, wenye pembe vichwani,
Wana kifanya kiburi, hawana heri moyoni,
Mbaya hawatafakari, shida hana maskani,
Tabu haina tajiri, wala si ya masikini.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
6
Ewe ndugu mwajiriwa, sema na wako moyo,
Jukumu ulilopewa, litimize pasi choyo,
Ridhika na unachopewa, shika wangu mgogoyo,
Rushwa katu si ngekewa, yataka ushinda moyo.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
7
Wote wategemeana, mwajiri na mwajiriwa,
Kubwa kuheshimiana, mwerevu kanielewa,
Pia mkiaminiana, kazi haitachezewa,
Tara mkifanyiana, lengo halitafikiwa
Riziki ni majaliwa, kuipata si ngekewa.
Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5.)
Whatspp/call 0622845394 Morogoro