KICHUNA CHANGU
Member
- Feb 5, 2016
- 16
- 4
RIWAYA: ANGAMIZO
MWANDISHI: HALFANI SUDY
SIMU: 0674 395733
Whatsapp 0757 633010
Sehemu ya Kwanza.
Ilikuwa jumatatu tulivu sana katika mitaa ya jiji la Arusha, jiji lilipo kaskazini mwa nchi ya Tanzania. Jumatatu iliyoanza kwa manyunyu ya mvua na radi kidogo katika Jiji hilo la Arusha. Kutokana na manyunyu hayo ya mvua, hali ya ubaridi iliongezeka katika jiji la Arusha. Baridi iliyowafanya watu wengi kuyakumbuka makoti yao na kuyatia mwilini. Siku hiyo ilikuwa ya furaha sana kwa Abdul Washiro, ilikuwa siku ambayo alikuwa anatimiza ndoto kubwa sana katika maisha yake. Alichaguliwa kujiunga na chuo cha Udaktari wa Binadamu Jijini Arusha. Na jumatatu hiyo ndio Ilikuwa siku yake ya kuripoti pale chuoni. Abdul Washiro alikuwa na furaha sana. Hata ile hali ya baridi haikumchukiza kabisa. Hakuwa anaihisi baridi kabisa. Mawazo yake yote yalikuwa juu ya kutimiza ndoto hiyo kubwa sana katika maisha yake. Wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza walikusanyika katika ukumbi wa Chuo kwa ajiri ya usajili. Walikuwa wanafunzi wengi sana. Toka mikoa mbali mbali Tanzania, waliokwenda jijini Arusha kuisaka elimu. Baada ya maelezo ya awali ya utambulisho toka uongozi wa chuo, pale ukumbini, sasa ulifika muda wa kupanga foleni ili usajili uanze. Kila mtu alikuwa anagombea nafasi ya kukaa mbele ili angalau asisote sana kwenye foleni. Ilikuwa ni fujo sana . Abdul Washiro alikaa kwenye kiti cha plastiki akiangalia vurugu zile. Hakuwa na wasiwasi wowote, alijua maadamu amechaguliwa kujiunga na Chuo kile, basi atasajiriwa tu. Baada ya fujo kutulia, Abdul naye alienda kujiunga kwenye foleni. Alikuwa mtu wa mwisho katika foleni ile ya usajili. Alikaa kwenye foleni huku akiwaza safari yake ya elimu ilipotokea.
Abdul aliwaza jinsi alivyosoma kwa shida shule ya Sekondari Bagamoyo. Wazazi wake hawakuwa na uwezo wa kumsomesha. Hivyo alipata shida sana kupata mtu mwenye moyo wa kumsomesha. Ilibidi mchana asome sana, ili jioni afanye biashara ndogondogo ya kuuza karanga ili aweze kupata hela ya mahitaji madogomadogo ya shule. Baba yake Abdul alikuwa mvuvi . Lakini pesa akizopata kutokana na kazi yake ya uvuvi zilitosha kuilisha familia yake tu. Hii ilitokana na Mzee Washiro kuwa na familia kubwa ya watoto saba. Mama yake hakuwa na kazi zaidi ya kuchuuza samaki mtaani, samaki wa mumewe. Inamaana ilikuwa sawa na kusema, baba na mama yake Abdul walikuwa wanafanya biashara moja. Baba anavua samaki, tena kwa zana dhaifu za uvuvi na mama anawauza kwa kuwachuuza mtaani. Katika watoto wote saba wa baba na mama Abdul. Abdul pekee ndio alikuwa anasoma shule. Wengine wote hawakutaka hata kusikia neno shule. Hawakuona umuhimu wa shule. Waliona kaka yao akivyoteseka kwa ajiri ya kusoma. Kupata sare, madaftari na michango midogomidogo ilikuwa shida. Nduguze Abdul wote walikuwa wanashinda pwani wakijitafutia ridhiki. Hata hivyo hawakuwa wanapata ridhiki ya kutosha. Pamoja na shida zote hizo, Abdul alijitahidi sana katika masomo ili afanikiwe, na kuisaidia familia yake iliyotopea katika dimbwi la umaskini. Ukweli ni kwamba alikuwa anafanya vizuri sana darasani. Siku zote alikuwa anaamini elimu ndio mkombozi wake. Elimu ndio silaha pekee ya kuishika kwa maskini kama yeye. Na aliishika kweli elimu. Mungu hamtupi mja wake, alifanikiwa kumaliza kidato cha nne pale shule ya Sekondari Bagamoyo, na kufaulu vizuri sana. Abdul alichaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano katika shule ya Sekondari Ndanda. Pamoja na kuijua thamani ya elimu, lakini alipofaulu kwenda Ndanda, Abdul pia aliitambua thamani ya pesa. Alijua kwamba kumbe pesa na elimu vilikuwa vinaenda sambamba. Abdul hakuwa na pesa kabisa ya kuweza kumpeleka shule. Kwanza nauli kutoka Bagamoyo hadi Mtwara, mkoa iliyopo shule hiyo Ilikuwa mtihani. Hapo hujajumulisha pesa ya ada pamoja na vitu vingine vya shule. Ndoto yake ya kusoma Abdul ilikomea hapo. Alihisi hawezi tena kuendelea na kusoma. Hata wazazi wake walimwambia hivyo. Baba yake alikuwa na jukumu zito la kuhakikisha familia inakula, familia inatibiwa, familia inavaa pia . Hakuwa na kipato cha kutosha kumuwezesha Abdul kwenda Mtwara kusoma. Abdul alikuwa na akiba ya shilingi elfu kumi iliyotokana na biashara zake za kuuza karanga jioni. Kumbuka Abdul ndiye alikuwa mkubwa katika familia hii. Alikuwa na ndugu sita nyuma yake, wote wakimwangalia yeye. Aliamua kuzifuta kabisa fikra za kukata tamaa. Aliamini kukata tamaa ni dhambi kubwa sana katika maisha. Aliyakumbuka vizuri maneno ya Mwalimu wake wa Kiswahili wakati anasoma pale Bagamoyo sekondari. "Usipende kukata tamaa ukiwa bado unaishi, pambana hadi pumzi yako ya mwisho, hakuna linaloshindakana chini ya jua". Maneno hayo ya mwalimu wake yalijirudia katika kichwa chake. Aliapa lazima asome kwa njia yoyote ile. Alikuwa anajiona mwenye wajibu wa baadae kuwasaidia wazazi wake. Kusaidia ndugu zake pia.
"Lazima nisome"
Alihisi maneno hayo anayesema polepole maneno hayo. Haikuwa hivyo, yalisikiwa na mtu aliyekuwa mbele yake katika foleni ile ndefu ya usajili.
"Unaonekana una mawazo sana kaka" Sauti nyororo ya dada aliyekuwa mbele ya Abdul ilipenya kwenye masikio yake.
"Hapana, sina mawazo dada" "Mbona unaongea peke yako sasa ?" Abdul hakujibu.
"Naitwa Mayasa"
"Naitwa Abdul"
"Tunaweza kuonana baadae sehemu tofauti na hapa?"
"Bila shaka" Walibadilishana namba zao za simu palepale kwenye foleni. Zoezi la usajili lilichukuwa saa zipatazo tano.
Hatimaye Abdul akasajiriwa kama mwanafunzi wa udaktari katika chuo cha udaktari Arusha.
HIVI NDIVYO ANGAMIZO LINAVYOANZA, TUKUTANE TENA SAA SITA MCHANAI TUENDELEE KUSOMA SIMULIZI HII.