KICHUNA CHANGU
Member
- Feb 5, 2016
- 16
- 4
RIWAYA: ANGAMIZO
MWANDISHI: HALFANI SUDY
SIMU: 0674 395733
WHATSAPP 0757 633010
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA JANA
Alikufa kifo kinachofanana na cha Mayasa!. Alikufa kifo kinachofanana na cha Raiya ! . alikufa kifo kinachofanaa na cha afande John. Yule jamaa nae alivuka ngozi! Kumbe yule jamaa alishika ile dawa inayoitwa Proxine pale alipotaka kumsalimia Abdul kwa mkono. Na alivyokuwa anataka kutoa kitu mfukoni alikuwa anataka kutoa dawa nyingine ili ajipake dawa kuzuia madhara ya ile dawa. Lakini alichelewa. Daniel alikuwa anamzuia kwa pigo kila alipotaka kuitoa ile dawa hiyo. Alijua atakufa! Ndomana alianza kulia kabla.
Siku zote mshahara wa dhambi ni mauti!
ISOME YA LEO SASA....
Daniel alimsogelea taratibu na kuanza kumuuliza Abdul kwa upole.
"Kuna kitu wanahisi unacho. Wanataka kukuua ili kisitoke nje. N kitu gani hiko?"
"Mimi sina kitu kaka Daniel. Sijui hata to wananitakia nini ?"
"Kipo kitu Abdul"
"Kitu gani sasa kaka Daniel ?"
"Mayasa alishawahi kukupa kitu chochote enzi za uhai wake?"
"Amewahi kunipa vitu vingi lakini siyo vya kudumu"
"Raiya alikupa nini cha kudumu ?"
"Hamna zaidi ya hii simu "
"Hebu ilete" Akampa.
Daniel aliiangalia ile simu kwa makini. Aliigeuza nyuma. Aliifungua ile simu kule nyuma. Kule inakokaa betri ilidondoka chini karatasi ndogo. Abdul alishangaa sana. Hakuwa ameweka karatasi yoyote kwa kuwa hakuwahi kuifungua simu ile tangu alivyopewa na Raiya. Daniel akaisoma kwa sauti ndogo ile karatasi.
"Kwenye laptop ya mme wangu kuna faili la limeandikwa Siri. Linahusu mpango wa kuangamiza watoto wa viongozi wa nchi hii na mambo mengine mengi ya siri sana . Abdul jaribu kulifikisha suala hili kunapohusika ili kuliokoa Taifa hili "
Abdul alishangaa sana. Sasa alimhusudu sana Raiya. Alimuona ni mtu mwenye akili kuliko mtu yeyote duniani. Raiya kumbe alikufa na siri kubwa sana. Ambayo siri hiyo aliifikisha kwa Abdul kwa siri pia. Abdul alimhusudu zaidi Daniel. Aligundua kitu alichokaa nacho miaka miwili bila kutambua . Alikiri Daniel hakuwa mtu wa karne hii. Alikuwa na akili na uwezo wa ziada.
Daniel alitoka nje na kile kikaratasi. Baada ya dakika kumi na tano waliingia askari wawili kuutoa mwili wa yule jamaa. Daniel alitoka nje kwa nia moja tu. Kumtafuta mume wa Raiya popote alipo. Ilikuwa lazima ampate popote atakapokuwa!
Upande wa kina Avast ilikuwa ni patashika na taharuki kubwa. Ilikuwa yapata saa saba ya mchana sasa, Avira hajarudi. Ilikuwa ajabu. Avira hakuwahi kufanya kazi muda mrefu namna hii. Avira hufanya mambo kwa haraka na kwa uhakika. Hiyo ndio sifa kuu ya Avira. Alitekeleza kazi ya kumuua Raiya robo saa tu alivyoenda magereza. Leo masaa zaidi ya matano alikuwa hajarudi.
Walimsubiri.
Walimsubiri sana.
Hakurudi.
Na hajarudi mpaka leo!.
Daniel alivyotoka palepale moja kwa moja alienda kwa dada yake Raiya. Alienda na kumuulizia mtaa na namba ya nyumba akiyokaa Raiya huko Dar es salaam ilipo. Baada ya kuelekezwa Daniel aliweka 'booking' ya ndege ya kwenda Dar es salaam kesho yake asubuhi.
Aliipata.
Usiku ule ulikuwa mgumu sana kwa Avast na Salehe. Wakaanza kuhisi huenda Avira amekamatwa. Wakawa wanahofia endapo Avira atakuwa kakamatwa anaweza kutoa siri. Siri pekee ambayo hawakutaka itoke ilikuwa kwenye laptop, nyumbani kwa Salehe, Dar es salaam. Wakapanga kesho Avast aende Dar es salaam kuichukua ile laptop. Ili siri isifike mikononi kwa adui!
Hawakujua kama atakutana na nini huko Dar es salaam!
Avast anaenda Dar es salaam kesho kuifata laptop yenye siri nzito. Daniel anaenda Dar es salam kesho kuifata laptop hiyo hiyo yenye siri nzito!
Wasakana.
Watakutana Dar es salaam.
BASI NASI TUKUTANE KESHO KUSHUHUDIA NINI KITATOKEA?