RIWAYA YA ANGAMIZO 10

Feb 5, 2016
16
4
RIWAYA YA KIPELELEZI: ANGAMIZO
MWANDISHI: HALFANI SUDY
SIMU 0674 395733
WHATSAPP 0757 633010

SEHEMU YA KUMI

ILIPOISHIA JANA

Abdul nae alianza kutetemeka mwili mzima kwa hofu. Alimwangalia Daniel kule nyuma ya mlango, alimshangaa hakuwa na hofu kabisa mwanaume yule !. Kwa hakika Daniel hakuwa binadamu wa kawaida. Kila hatari inavyomkaribia yeye anazidi kuwa mtulivu na tabasamu lisiloisha usoni mwake. Wale jamaa waliingia ndani ya Mgahawa. Pale nyuma ya mlango sasa Daniel Alikuwa ameshika bastola mbili mkononi. Ndani ya nusu dakika watu wote kumi walikuwa chini. Wote walikuwa wameuwawa na Daniel ! Wanafunzi wote walisimama na kumpa mkono wa pongezi Daniel. Alikuwa shujaa kwao. Alikuwa shujaa zaidi kwa Abdul. Walimhusudu sana Daniel. Abdul alimhusudu zaidi Daniel ! Walitoka eneo la Chuo huku Daniel akiwapigia simu Polisi waje kutoa maiti zile. Wao walielekea moja Kwa moja kituo cha Polisi Arusha.
SASA ENDELEA
Katika nyumba moja iliyopo mtaa wa Mikocheni, jijini Dar es salaam. Kulikuwa na kikao. Kikao kilihusisha watu watano. Wanajeshi wanne wenye vyeo vikubwa jeshini na raia mmoja wa kawaida. Wanajeshi wale walikuwa wana vyeo vikubwa sana jeshini. Walikuwa wanajadili mpango wao walioupa jina la Angamizo. Lengo la awali la mpango huo ni kuwaangamiza watoto wote wa viongozi wa Tanzania. Ili kusafisha njia kwa Mpango wa Angamizo! Katika kikao kile mtu mmoja tu ndiye ambaye hakuwa mwanajeshi. Mumewe Raiya. Alikuwa anaitwa Salehe, yeye ndiye aliyesababisha siri za mpango huu zivuje Kwa mtu asiyehusika. Kwa bahati mbaya lakini, siri za mpango huu wa Angamizo zilimfikia mkewe, Raiya.
Ilikuwa siku ya ijumaa. Mumewe Raiya alichelewa kurudi nyumbani. Raiya alijisikia uchovu sana. Alichukua laptop ya mumewe ili apoteze mawazo . Kipindi hicho Raiya alikuwa na wakati ngumu sana katika maisha ya ndoa yake. Mumewe alikuwa bize sana. Vikao visivyoisha hadi saa tisa ya usiku. Kutokana na ubize huo Raiya akahisi anasalitiwa kwa kutopewa haki yake ya ndoa. Kumbe hakuwa anasalitiwa. Mumewe alikuwa bize na Mpango haramu, ulioitwa Angamizo!
Hakuwa anampa haki yake ya ndoa mkewe. Alibadilika kabisa. Muda mwingi alikaa peke yake kuipanga sawa mipango yake.
Siku moja hiyo akiwa anachezea laptop ya mumewe. Ndani ya laptop ya mumewe Raiya aliliona faili liliandikwa Siri. Akalifungua bila wasiwasi wowote. Ndani ya faili hilo ndimo alikutana na mambo yaliyomtisha sana. Mpango wa Angamizo ulipangwa utekelezwe baada ya miaka miwili. Ulikuwa Mpango hatari ulioratibiwa na watu hatari sana!
Siku alipoliona faili lile lenye siri toka Kwenye laptop ya mumewe kesho yake ndipo alipokutana na Abdul. Akiwa anatoka Bagamoyo kwa miguu, na kuanzisha uhusiano haramu. Ulikuwa uhusiano haramu lakini ulioleta faida kubwa kwa Taifa baadae.
Siku zilivyosonga mbele Salehe alihisi mabadiliko toka kwa mkewe. Akahisi huenda anatoka nje ya ndoa yao.
Anamsaliti!
Siku zote alikuwa anamlalamikia kuhusu suala la unyumba. Lakini Sasa alikuwa halalamiki tena. Akaanza kumchunguza. Na zaidi Raiya akaanza kumuogopa sana mumewe. Salehe akachunguza. Akagundua kila walichokuwa wanafanya na Abdul. Mbaya zaidi Salehe aligundua pia kuwa Raiya amegundua mpango wao wa Angamizo! Na akajua kwa vyovyote Raiya lazima atamsimulia mtu wake wa karibu. Ambaye ni Abdul! Sasa Salehe alianza kumfatilia Raiya kwa kila hatua aliyopiga. Siku Aliyomuaga kuwa anakwenda Arusha alimkubalia lakini hakumwacha peke yake. Alimfatilia!
Ndipo alipogundua kwa kina kila kitu kuhusu uhusiano wao na kuamua kuwaangamiza wote kwa sumu kali na hatari iitwayo Proxine!
Ndani ya kikao kile ilikuwa ni kutupiana lawama. Wanajeshi wote wanne walikuwa wanamtupia lawama Salehe. Kwa kuweka rehani Mpango wao hatari!. Salehe alijitetea sana.Lakini hakueleweka kabisa. Wakati wanaendelea na mazungumzo yao, simu ya Salehe iliita.
"Halo"
"Bon, Arusha"
"Nambie Bon"
'Mambo mabaya sana"
"Kuna nini tena ?"
"Tumepoteza wapiganaji kumi na tano leo"
"Unasema !!!"
"Ndio hivyo Salehe, kumi na tano wameuwawa "
"Sisi tumefanikiwa lakini !
"Hatujafanikiwa "
"Kwanini Bon..hadi sasa anapumua?"
"Ni msumbufu sana kaka"
"Inamaana ni Abdul ndiye aliyewauwa wapiganaji wetu kumi na tano"
"Ndio Abdul, ila yuko na mwenzie. Ni watu hatari sana"
"Nakuja na Avira na Avast kwa ndege ya jioni, kummaliza"
"Itakuwa poa kaka"
Hali ilikuwa tete ndani ya kundi hili lenye Mpango wa Angamizo.
Jioni ya siku ile Salehe akiongozana na Avast na Avira walikuwa wanaelekea jijini Arusha.Kwa kazi moja tu.
Kuhakikisha Abdul anauwawa!
Avast na Avira walikuwa wauaji hatari. Wauaji wanaojua aina zote za mauaji. Walikuwa makomandoo toka Nigeria walioletwa kwa ajili ya kuleta Angamizo nchini Tanzania. Ni hawa wauaji wanaotumia sumu hatari ya Proxine kuwaua watu kinyama. Asubuhi ya leo walikuwa Arusha kutekeleza kifo cha Raiya akiwa gerezani.Na sasa wanarudi tena Arusha kukatisha maisha ya Abdul. Hawakuwahi kushindwa wanapoamua kuuwa mtu. Walikuwa makini sana na kazi yao. Walitua jijini Arusha saa moja kamili usiku. Walipanga asubuhi ndio waanze kazi yao ya kumsaka Abdul. Hawakuwa na wasiwasi hata kidogo. Walikuwa na uhakika hata kama askari wote Arusha watakaa nje ya kituo cha Polisi alikokuwemo Abdul, waliamini lazima watamuuwa. Walikuwa na mbinu na hila zote za kijasusi.Waliamini watamuua tu!
Walijiamini.
Waliaminiwa pia!
Daniel Mwaseba alimwacha Abdul amemfungia katika chumba cha siri pale Polisi. Chumba kikichojulikana na baadhi tu ya Polisi. Kilikuwa chumba kinachotumiwa kwa nadra sana. Tena kwa sababu maalumu. Daniel alienda kufanya kazi. Aliyanasa maongezi ya Kwenye simu kati ya Bon na Salehe kutoka Kwa rafiki yake aliyekuwa anafanya kazi katika kampuni ya simu waliyotumia Bon na Salehe kuwasiliana. Alihisi kuna kitu kutoka kwa mumewe Raiya. Hivyo aliongea na rafiki yake anase na kurekodi simu zote za Salehe kwa kifaa kiitwacho telemax. Hivyo alisikia simu zote zilizoingia na kutoka katika simu ya Salehe. Ikiwemo simu aliyopiga Bon kwenda kwa Salehe. Na Daniel alikuwa anawasubiri wageni wake.
Daniel aliiona ndege waliyopanda Salehe, Avast na Avira ikitua pale uwanja wa ndege wa Arusha. Aliwaona watu wale watatu wakishuka kwa kujiamini sana. Macho ya Daniel yalikuwa makini sana na wale majamaa mawili, Avast na Avira. Macho yake yalimwambia hawakuwa watu wa kawaida! Aliwaona walivyoshuka kwenye ndege na kupanda kwenye gari aina ya Noah nyeusi. Sawa na zile alizofukuzana nazo asubuhi. Aliifuata nyuma Noah ile akiwa na pikipiki yake. Avast na Avira hawakuwa watu wa kawaida. Huwa wanaweka tahadhari kabla ya jambo halijatokea. Leo walivyoshuka tu kwenye gari walihisi watafuatwa. Walikuwa makini sana! Wakati Daniel akiwafata akina Avast na Avira kutoka uwanja wa ndege, kina Avast walikuwa makini sana na magari yaliyokuwa nyuma yao. Baadae kidogo waliitilia shaka pikipiki iliyokuwa inawafata nyuma. Wakawa wanasubiri muda muafaka wamtie mikononi mfuatiliaji. Wakawa wanaendesha gari taratibu wakiipigia hesabu ile pikipiki. Walikuwa na sumu yao hatari ya Proxine.Tayari kwa kuitumia muda wowote itakapobidi. Msafara uliwafikisha kwenye mzunguko wa Azimio la Arusha wakielekea stendi kuu Arusha.

DANIEL ANAWAFUATA WAKINA AVIRA, NAO WASHAGUNDUA KAMA WANAFUATWA, JE NINI KITATOKEA, SEHEMU YA KUMI NA MOJA NDIO YENYE MAJIBU....
 
Back
Top Bottom