Riwaya: UCHU

KASHESHE-
XVIII

Wakati huo Jean alikuwa ameanza
kumvua nguo Bibiane ili atimize ahadi
yake kama alivyoahidi kuwa atafanya nae
mapenzi kabla ya kumuua, wakati
akikaribia kutimiza ahadi yake, ghafla
mlipuko mkubwa ulitokea eneo hilo na
kuleta hofu, palepale nyumba ile
ikasambaratika vipande. Bahati nzuri
nyumba hii ilikuwa imetengenezwa kwa
mbao tupu ili likitokea tatizo kama hili
Kamanda Morris asihatarishe maisha
yake.
Kwa vile Bibiane alikuwa akiutegemea
mlipuko kama huo, ulipotokea tu
hakuzirai kama wengine. Alizitupa mbao
zilizomwangukia mwilini mwake,
akainuka na kuanza kumsaka Willy
ambaye wakati huo alikuwa amefungwa
kwenye kiti pale ukumbini. Kumbe mlipuko
ulipotokea kile kiti kilirushwa pamoja na
Willy Gamba mpaka nje kwenye bustani.
Bibiane aliangalia huku na huko kwa
tahadhari kubwa, maana watu wote
walikuwa wamelala chini kwa hofu. Vilio
vilisikika eneo lote la kambi hii mara
akamuona Willy Gamba na kiti chake
akiwa nusu amezirai.
Milipuko ile iliendelea kuleta hofu na
kusababisha mwanga mkubwa katika
eneo lote. Milio na mwanga ilionekana na
kusikika mpaka Goma, Gisenyi na
sehemu nyingine kwani sasa mizinga na
makombora nayo nayo yalianza kulipuka
bila mpangilio na kusababisha Jean na
wenzake kupatwa na taharuki. Bibiane
alitoa kisu chake kidogo alichokuwa
amekifika kwenye nywele zake, akiwa
tayari kabisa kummaliza Jean. Na kwa
kutumia hiki kisu alifanikiwa kuzikata
kamba alizokuwa amefungwa Willy
Gamba kisha akamtingisha hadi Willy
akapata fahamu. Baada ya Willy
kuzinduka Bibiane akamshika mkono.
Willy alisimama wakakimbia kuelekea
sehemu ile ya Magharibi ya kambi mahali
ambapo kulikuwa na mstu mkubwa.
Walipokimbia kama mita hamsini hivi
Bibiane alitoa bomu la kurusha kwa
mkono akalitupa kwenye ile nyuma kisha
wakajitupa chini. Bomu hilo liliporipuka
likasambaratisha eneo hilo halikubakiza
mtu wala kitu kilichokuwa ndani ya
nyumba hii au mita thelathini kuzunguka
nyumba hii. Wakati wanaelekea kwenye
ule mstu mabomu, mizinga na
makombora yaliyokuwa ndani ya
maghala makubwa ya kuhifadhia silaha
yaliendelea kuripuka yenyewe.
"Kazi ipo Willy, wamelikoroga acha
walinywe sasa", Bibiane alisema kwa
kebehi.
"Kazi yenyewe si kidogo, wamelala
matajiri wataamka masikini", Willy alijibu
wakiwa wemeingia kwenye msitu.
"Naona sasa tumechoka, kazi hii inatosha
kabisa kwa siku moja ya leo", Willy
alieleza wakiwa wametokeza kwenye
sehemu ya majani mazuri chini ya
mbaramwezi. "Hapa panafaa kupuzika,
au vipi", Willy aliuliza.
"Hapa tumetafutiwa na Mwenyezi Mungu
ili tupumzike baada ya hii kasheshe.
Nilikuwa natamani ufike muda nipate
mahali ambapo dunia itakuwa mimi na
wewe tu. Na mahali hapo ni hapa, yaani
mimi, wewe, mbaramwezi, nyota, malaika
na Mungu", Bibiane alieleza.
Willy alivua gwanda lake la juu akatandika
chini kwenye majani, Bibiane akavua pia
na kusema. "Hili tutajifunika".
Willy akamwinua na kumbeba mikononi
kisha akambusu na kumlaza juu ya
gwanda lake.
ITAENDELEA
 
kidi kudi asante sana, kumbuka kutuwahishia ukisha andaa kipande kingine.
 
ahhhh nini kinaendelea hapo juu ya magwandwa? ni usingizi? asante tupe raha tafadhali
 
Yaani Jean muda wote alikuwa hajamaliza kazi?----- sana
 
Mpaka muda huu bao kama tatu hivi!si haba bandu bandu humaliza gogo!
 

Mkuu
Hukuonyesha willy na bibiane walivyokamatwa
Tunasubiri kumalizia uhondo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…