Riwaya: UCHU

Riwaya: UCHU

Tuliishia pale willy gamba katekwa . alafu bibiane anasubilia kuliwa mambo Na jean.

lzm jean alikaribisha kifo ndani na kuhusu Willy gamba ndo ulikuwa mwisho wake.

kwani kuna riwaya zaidi baada ya uchu?
 
KASHESHE
XVI

Anatoile Kabuga alimwangalia Willy kwa
jicho baya sana, alimuona kuwa ndiye
kikwazo na adui wao namba moja kwa
kuwachelewesha Inyenzi na washirika
wao kushika madaraka ya nchi ya
Rwanda. Hata hivyo aliamini kuwa hakuna
mtu mwingine zaidi ya Willy atakayeweza
kupena na kuingia katika ngome yao.
"Nitakupa historia kidogo", Anatoile
Kabuga alianza kumweleza Willy Gamba.
"Willy Gamba, lazima ufahamu kuwa
sehemu hii ya Maziwa Makuu katika
Afrika watu wa kwanza wa asili ni
wabantu. Wabantu ndio walioishi eneo hili
la Maziwa Makuu kwa karne nyingi sana
tena wakiishi kwa raha mstarehe bila
migogoro wala matatizo mpaka
walipokuja watu wenye asili ya Kihemetiki
ambao baada ya kufika eneo hili walianza
kuleta chokocoko, vita wakitokea
Kaskazini na Mashariki mwa Afrika. Kwa
ufupi, Watutsi wamo kwenye kundi hilo.
Tangu wafike katika sehemu hii amani
imekosekana kabisa. Karne mbili
zilizopita walianza kuweka Ufalme wao
katika eneo hili baada ya vita vikali na
wabantu wa sehemu hii na kuwashinda.
Waliweka wafalme wao waliowaita
wafalme wa Kihima ambao walitawala
kutoka Bahari ya Hindi mpaka Atlantiki,
sehemu ambayo sasa ni Zaire, Rwanda,
Burundi, Tanzania, Uganda na Kenya",
alinyamaza kidogo kisha akaendelea.
"Willy Gamba. Nitakueleza kwa kifupi sana
maana hatuna muda wa kupoteza. Lakini
kwa sababu wao walikuwa wachache na
wakawa wanaendeleza utawala wa
mabavu na unyanyasaji kwa wabantu
ambao ndio waliokuwa wengi, hali
inayoendelea mpaka sasa, mapigano ya
kuukataa utawala huo yaliendelea
sehemu zote, hatmaye ufalme huo
ukaangushwa katika sehemu zingine na
kubaki sehemu ambayo sasa ni Rwanda
na Buurundi. Na hali hii iliendelea mpaka
wakati wa Ukoloni ambapo katika Rwanda
utawala wa ukandamizazi wa Watutsi
dhidi ya Wahutu na wabantu ambao ndio
wengi katika Rwanda, uliendelea. Miaka
yote hii mpaka vita vya pili vya dunia
Watutsi wachache waliendelea kutawala
na kuwanyanyasa Wahutu wakihakikisha
kuwa hawapati elimu, madaraka na hata
mali. Ni mpaka juzi tu, mwaka 1957,
Wahutu walipojikomboa na kushika
madaraka, na hawa Inyenzi wakakimbilia
nchi jirani ikiwemo Tanzania. Wakati wa
utawala wetu tulijaribu sana kuwaweka
karibu lakini siyo wote waliotaka
kutawaliwa na walio wengi sababu wao
walijiona wana hadhi ya juu kuliko sisi.
Vilevile, waliapa kuwa lazima watatafuta
njia mbadala warudi kututawala maana
sisi ni watumwa wao. Na kwa taarifa yako
kila Mtutsi anamuona kila Mbatu kama
mtumwa wake. Ndivyo wanavyokuona
wewe hata kama unawasaidia kwa
sababu wewe ni Mbantu na ndivyo
wanavyoniona hata mimi. Sasa basi
tatizo kubwa lilikuja wakati nchi jirani
ilipopata kiongozi mwenye asili hiyohiyo
ya Kitutsi, na akawa na nguvu na
akaahidi kuwasaidia Wahutu ili wautoe
utawala wa wabantu katika Rwanda,
Yaani watu wenye asili ya Kitutsi tu ndio
watawale sehemu hii ya maziwa makuu
ikiwemo Zaire, Rwanda, Burundi,
Tanzania, Uganda na Kenya. Sisi
tulipopata habari hizi tukajua eneo lote
hili la maziwa makuu halitapata amani
ikiwa hawa Watutsi wanazidi kuzaliana na
kuwa wengi eneo hili. Njia pekee ya
kuleta amani ni kuhakikisha mmewaua
waume, wake kwa watoto, ili kuua kabisa
nguvu yao. Leo hawa tusipowaangamiza
nakueleza wewe Willy Gamba, Tanzania
haitakuwa na amani na wala Zaire,
Uganda na Kenya hawana amani maana
hawa wana asili ya kujipanua. Ni watu
hatari ajabu, na kama mngejuwa kuwa
hawa ni watu wa kuteketezwa kabisa hata
mmoja asionekane katika sehemu hii".
"Ngoja nikukata kauli, umesema watu
wengi katika eneo hili la maziwa makuu
ni wabantu, hawa Watutsi wachache
watatawala vipi", Willy aliuliza huku
akisogeza vidole vya mkono wake wa
kulia kujaribu kama vingeweza kuifikia
saa yake aliyovaa mkono wa kushoto.
"Unasema nini, tunavyozungumza nani
anatawala Rwanda, Burundi na Uganda,
watu wengi katika nchi hizi ni watu gani,
sisi wabantu, sasa nini kitawashinda
kutawala Zaire, Tanzania na Kenya kama
wameweza katika nchi hizo, njia pekee ni
kuwateketeza ili waishe, wasiendelee
kutunyanyasa na kuleta vita vya mara
kwa mara katika eneo letu. Hawa na
Wayahudi hawana tofauti. Ngoja
nikwambie Willy Gamba, hawa Watutsi
hata kama ukiona Mtutsi amezaa na
wewe lazima atatembea na Mtutsi
mwenzie ili azae Mtutsi, kazi yako wewe
itakuwa ni kukuza damu isiyokuwa yako.
Na wamehakikisha wanawake wao
wamesambaa dunia nzima, lakini kila
mwanamke wa Kitutsi ahakikishe mahali
alipo anapewa mimba na Mtutsi mwenzie
tu. Huku wanawake wao kusambaa ni njia
mojawapo ya kujipanua ili waweze
kufanya kampeni yao kwa kuhurumiwa na
mataifa mengine. Hivyo, mauaji haya
tuliyofanya ni kwa niaba ya wabantu wote
na sasa hivi tuko tayari kuurudisha
utawala wetu Rwanda na Burundi ili
heshima ya mbantu katika eneo hili
ipatikane. Baada ya kuichukua tena
Rwanda mara hii tutataka viongozi wote
katika eneo hili waelewe ukweli huo na
watuunge mkono kuwatokomeza Watutsi
hawa. Vinginevyo nakwambia Willy
Gamba watatawala tena sehemu yote hii,
la sivyo hakuna amani katika eneo hili.
Vita vitaendelea kwa miaka mingi. Sisi
Akazu ndio tumaini pekee la sehemu hii,
bila sisi kesho tawala zote za sehemu hii
zinazotawaliwa na wabantu zitatikiswa na
kumalizwa. Hivyo, wewe Willy ni msaliti,
unawasalti wabantu kwa kuwasaidia
Inyenzi ili waweze kutawala ardhi halali
ya wabantu. ndio sababu tumekuhukumu
kifo. Na, wote wawe wabantu au taifa
lingine, wakibainika wanasaidia Inyenzi
lazima wauawe. Na sasa wewe utauawa
ili Akazu ifanye kazi yake ya kuwakomboa
wabantu", Kabuga alisema kwa sauti nzito
iliyoashiria hasira ya ajabu ambayo kila
mtu pale ndani alihisi kapagawa.
"Yote hayo uliyoyasema yanaweza kuwa
na ukweli mwingi tu, lakini ukweli huwa
hautoi uhalali wa kuangamiza kabila
zima. Hii ni kinyume na haki za
binadamu. Njia nyingine itafutwe
kuwadhiti na si kuwaangamiza", Willy
alijibu huku kidole chake cha karibu na
gumba kwenye mkono wa kulia kikiwa
kimefika kwenye ufunguo wa saa yake na
kukandamiza ufunguo wa saa na kusubiri
kuona kifo chake ama kifo cha jeshi la
Akazu.
"Unasema haki za binadamu, sisi
wabantu hatuna haki mbona............",
Kabuga hakumaliza sentensi yake
teknolojia ilianza kufanya kazi yake.
ITAENDELA
 
Shukran kidikudi kwenye uhondo ndio tumepafikia usipotee sana ndg hatukushurutishe ila kwa ihsani yako.
 
Hivi inyezi ni watu gani tena hapa kwa hii story?
 
kidikudi umerudi kutuburudisha endelea usitutelekeze
 
Ndio kwanza ni SAA nane Na nusu usiku . willy anajaribu mambo yake .
 
Kidi kudi Fanya mambo. Leo Na hiki kimvua mvua walau tujipumzikie Na uchu
 
Duh! kidikudi amekuwa kama kakakuona! akijitokeza mnajua neema ingawa ni imani za kale!
 
Hii riwaya kuja kuisha kila MTU inabidi akapime vidonda vya tumbo,maana uchu halafu hushibi....
 
KASHESHE-
XVII
Col. Rwivanga, Mpinda na Meja Tom
Kabalisa waliwasili mpakani mwa nchi za
Rwanda na Zaire katika sehemu
waliyokuwa wamekubaliana na Meja
Kasubuga mnamo saa nane na dakika
arobaini usiku.
Hali ya usalama ilikuwa imeimalishwa
katika eneo hili, ambapo vijana wa Meja
Kasubuga walikuwa makini kwa kila
jambo, baada ya Helikopta ya jeshi la
Rwanda waliyosafiri hadi mpakani kutua,
Col. Rwivanga alikuwa wa kwanza
kushuka akifuatiwa na Mpinda, kasha
Meja Kabalisa.
"Mambo yakoje hapa", Col. Rwivanga
alimuuliza Meja kasubuga wakati
wakisalimiana baada ya heshima ya
kijeshi.
Meja Kasubuga alieleza kwa urefu jinsi
mapambano yalivyokuwa, kisha
akamalizia, "Huyu Willy atakuwa kauawa
kule Kibumba maana kajipeleka mahali
ambapo panatakiwa vikosi vyote husika,
huyu Willy ingawaje Afande unamsema ni
hatari lakini hana akili ya tahadhari,
angesubiri twende wote, ndipo angeweza
kuwa msaada kwetu maana maiti haina
msaada wowote.
"Nakubaliana na wewe lakini yule ni mtu
mwenye maisha mengi, unaweza
kumuona kaibuka", Col. Rwinga alisema
wote wakacheka kwa utani huo.
"Kweli, akiibuka tena atakuwa mtu wa
maisha mengi", Meja Tom Kabalisa wa
Banyamulenge alijibu kwani na yeye
alijua nguvu za Intarahamwe kule
Kibumba na ndio sababu alikuwa
hajathubutu kufanya lolote. Kisha
akaendelea. "Col. Rwivanga, nafikiri sasa
tumweleze Meja Kasubuga mipango ikoje
ili....", Kabla Meja Kabalisa hajamaliza
kusema sentesi yake, mripuko mkubwa
usio kifani ulisikika mpaka huko
walikokuwa.
"Ooh Willy Gamba, kweli u-hatari", Meja
Kasubuga aligwaya.
ITAENDELEA
 
asante kidi kudi, natambua jitihada zako asante sana.
 
Back
Top Bottom