Riwaya: UCHU

Wiki imeisha bila bila, tusubirie weekend ijayo huenda ikakumbukwa. Asanteni wakuu wote mnaojitahidi kuandaa hii kitu.
 
KASHESHE
XV
Meja Kasubuga alipigana vikali na jeshi la
Luteni Nyamboma na kufanikiwa kuwazidi
nguvu na hivyo askari wa jeshi hilo
walilazimika kukimbilia mpakani. Luteni
Nyamboma alikuwa amepoteza askari
wengi sana, walipfika mpakani
wakitegemea kumkuta Nkubana ili
awaongezee nguvu ya askari warudi
kuendeza mapambano, lakini hakumkuta
Nkubana. Hivyo, Luteni Nyamboma
akaamua kuelekea Kibumba na masalia
ya askari wa kikosi chake waliobaki.
Luteni Nyamboma alipoangalia saa yake
ilikuwa saa nane usiku. Walitumia magari
waliyoyakuta pale mpakani, Luteni
Nyambona na askari wake waliondoka
kuelekea Kibumba.
Hata hivyo, Luteni Nyamboma alilazimika
kuwaacha askari wa jeshi la Zaire pale
mpakani kwa ajili ya ulinzi ili baada ya
kazi ya Gisenyi Luteni Nyamboma
awafuiate Kibumba.
Meja Kasubuga alipofika mpakani
aliyaona magari yanaondoka kasi eneo la
mpakani. Meja Kasubuga akagundua
kuwa magari yale yalikuwa yakielekea
Kibumba. Asingekuwa ameamriwa na Col.
Rwivanga awasubiri pale mpakani hakika
Meja Kasubuga angeyafuata magari
yaliyoondoka na kikosi kile. Baada ya
kufika mpakani, jeshi la Meja Kasubuga
lilifanikiwa kukitwaa kikosi cha jeshi la
Zaire kilichokuwa kikiwasaida wanajeshi
la Intarahamwe na hii ikawa ngome ya
jeshi lake kwa muda.
Kikosi hiki kilichokuwa mpakani mwa
Zaire na Rwanda kilikuwa kimejijenga
vizuri kivita, kikiwasaidia wanajeshi wa
Intarahamwe na kundi la Akazu lililokuwa
likifanya jitihada ya kuivamia serikali ya
RPF ili kutwaa madaraka ya kuiongoza
Rwanda kijeshi.
Baada ya kuhakikisha usalama wa eneo
hili, Meja Kasubuga alielekea sehemu
iliyoandaliwa, ambayo Col. Rwivanga
alimweleza kuwa angetua hapo kwa
Helikopta akiwa na kiongozi wa kikundi
cha Banyamulenge na kiongozi wa vikosi
vya vyama vinavyoipinga serikali ya
Zaire. Meja Kasubuga alipoangalia saa
yake ilikuwa saa nane na dakika kumi.
Muda ambao Col. Rwivanga aliahidi kuwa
atafika Gisenyi. Hivyo, Meja Kasubuga na
kikosi chake wakaamua kusubiri.
Col. Rwivanga alikuwa na matumaini
makubwa na kikosi cha Meja Kasubuga,
hivyo baada ya kuondoka Kigali kwa
Helikopta ya jeshi, walisafiri moja kwa
moja usiku huo kuelekea Gisenyi. Col.
Rwivanga hakuwa na papala wakati wote
alikuwa akitafakari jambo kabla ya
kulifanyia kazi. Alikuwa mmoja wa
maofisa wa jeshi walioheshimiwa na
kutegemewa sana na serikali ya Rwanda.
Alikuwa mtu mwadilifu asiyependa kuisalti
nchi yake, kutokana na msimamo wake
dhabiti aliogopwa sana na vibaraka
hususan wanaotaka kuigawa Afrika.
Alikuwa akijitosheleza kiulinzi, kutokana
na hali hiyo nyumba yake haikuwekewa
ulinzi kutoka jeshini, kama ilivyo kwa
maofisa wengine wa ngazi za juu kama
yeye. Alikuwa mmoja wa makomandoo wa
jeshi waliofuzu vizuri mafunzo yake, lakini
kutokana na cheo chake jeshini alibaki
kuwa ofisa wa jeshi aliyeheshimiwa sana.
Alikuwa mpole asiyependa makuu,
alikuwa na subira, hata ukimchoma kidole
machoni hatakufanya kitu. Lakini
akilazimika kuchukuzwa na upuuzi
alifanya kitu ambacho hakuna awezaye
kuamini, hakuwa na mchezo tena. Huyo
ndiye Col. Thomas Rwivanga, Afisa wa
jeshi mwandamizi.
ITAENDELEA
 
yes yes yesss! fungulia kama bomba la maji Mkuu kidi kudi.
 


Come on...............................................................
 
Tuliishia pale willy gamba katekwa . alafu bibiane anasubilia kuliwa mambo Na jean.
 
Leo Ijumaa nakuomba Willy Gamba 1, kidi kudi, mareche tafadhali sema neno juu ya mwenendo wa riwaya hii nami roho yangu itatulia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…