Willy Gamba 1
JF-Expert Member
- Jan 5, 2015
- 352
- 377
RIWAYA: TANZIA
MTUNZI: MAUNDU MWINGIZI
SEHEMU YA KWANZA
Ilikuwa ghafla tu, Pepo kali zilipovuma karibu kila
kona ya wilaya ya Kibondo, mkoani kigoma.
Taratibu mawingu mazito yakalifunika anga kiasi
cha kuifanya saa tisa ile ya alasiri ifanane na usiku
wa manane, usiku wa kiza, usiku wa hofu.
Ingawaje ilikuwa ni msimu wa kiangazi na kwamba
ni aghalabu mvua kunyesha, lakini hakuna
aliyeipuuza dalili ya mvua ile ambayo ni mawingu.
Kilichowafanya wakaazi waogope zaidi ni jinsi giza
lilivyozidi kuumeza mwanga, maana hata kama
ndo dalili yenyewe ya mvua, hii sasa ilizidi!
Baadhi ya wafanyabiashara wakaanza kufunga
maduka yao, wanafunzi wakikimbilia makwao, na
hata mifugo nayo ikaanza kurejea mabandani ikijua
kuwa usiku umewadia. Wale wenzangu na mimi
wenye nyumba za udongo zilizosheheni mawakili
karibu katika kila ukuta walianza kudhikiri
vyumbani mwao wakimuomba mola awasitiri
maana bila hata ya mvua tu, kila siku ukuta
unakuuliza Nikuuwe? sasa je ikishuka si kuta
zitageuka biskuti?
Upepo mkali uliendelea kuvuma mithili ya
kimbingunga huku baridi kali ikiwa imeshtadi
kwelikweli, cha jabu hapakuwa na mingurumo, radi,
wala manyunyu ni upepo, Baridi na giza tu.
***
Wakati hali hiyo ya hewa ikizidi kuchafuka, katika
wilaya hiyohiyo ya Kibondo nyumba ya Bi
Masonganya binti Kalukalange ilifurika umati
mkubwa wa wana-ukoo kutoka sehemu mbalimbali. Watoto, wajukuu, vitukuu na vilembwe
wakiwa wamekusanyika kwa kukizunguka kitanda
cha chuma alipolala Bi Masonganya.
Ni wana-ukoo hao pekee ndiyo waliokuwa wakijua
siri ya hali ya hewa kubadilika ghafla katika eneo
lote la kibondo. Ni kwamba bibi na mama yao
kipenzi, Bi Masonganya alikuwa akikaribia kukata
roho baada ya kuishi kwa takribani miaka miamoja
na sitini! Kwa kawaida kifo huja ghafla tu na hakuna anayeweza kupata taarifa kabla ila kwa
wana-ukoo hawa walikitumainia kifo cha mama na bibi yao yule.
Yreeeeeeeew! Watemi woseeee! mizimu yoose!
Makulwa na madoto, na makashindyeee!
Mumsaidie mtu wenu. Maneno hayo yalitamkwa
kwa sauti kali na babu mmoja aliyekuwa
amesimama pamoja na wana-ukoo wale kisha
akatoa chafya kwa nguvu na sauti kali sana!
Nje ya chumba hicho, usawa wa dirisha alikuwa
amesimama binti wa mwisho wa Bi Masonganya,
akiwa ameshika mwichi mkononi akisubiri ishara
aliyoelekezwa ili atekeleze zoezi muhimu na ishara
hiyo ilikuwa ni ile chafya aliyoisikia ikitokea ndani.
Kitendo bila kuchelewa akauinua juu ule mwichi
aliokuwa ameushikilia, kisha akaukita kwa nguvu
chini ya ukuta ambao kwa ndani amelala mama
yake akiwa amezungukwa na wana-ukoo.
Baada tu ya kuukita mchi ule chini ya ukuta, kule
chumbani wana ukoo wakashuhudia mama yao
akihangaika kitandani kwa sekunde kadhaa huku
akikakamaa kama askari wa kikoloni akijiandaa
kupiga saluti kwa bwana wake, haikuchukua hata
dakika mbili, Bi Masonganya akanena kwa sauti
kavu ya kukoroma.
Akkh wana-ngu mme-niwe-zaa mme-ni-u-
waaa! Hapohapo Bi Masonganya akakata roho.
Sauti za vigeregere, nderemo na vifijo kutoka kwa
wana-ukoo vilizizima chumbani humo, japo
havikuwa vigeregere vya furaha bali viashiria vya
kukamilika kwa kifo kile kilichowabidi
kukilazimisha. Laiti wangejua kilichokua
kikiwanyemelea, wala wasingenyanyua vinywa
vyao kupiga vigeregere. Lakini ndo hivyo tena
hakuna aijuaye kesho hata mtunzi wa kalenda.
Baada tu ya Bi Masonganya kukata roho, muda
huohuo hali ya hewa ikabidilika tena, mwanga
ukarejea na upepo ukatulia kiasi cha
kuwastaajabisha wakazi wa Kibondo.
***
Sifa kubwa ya Bi Masonganya ilikuwa ni uchawi.
Uchawi uliokubuhu, aliorithishwa na marehemu bibi
yake mzaa mama ambaye kwa asili ni mtu kutoka
Kongo. Uchawi huo ulimfanya Bi Masonganya
aheshimike na kuogopwa karibu na kila mtu. Wapo
aliowaangamiza kutokana na uchawi wake, na
wapo aliowasaidia, lakini mchawi ni mchawi tu
hana muamana asilani.
Ilikuwa Bi Masonganya akaikwambia kuwa
hautoliona jua la jioni basi kimbia haraka
ukamtake radhi, vinginevyo utakufa kweli. Na hata
uwe na kesi ya namna gani endapo utamfuata
kumtaka msaada na akaamua kuivalia njuga basi
piga geuza utashinda tu. Mpaka viongozi wakubwa
serikalini wanaouhusudu ushirikina huwasili kwa Bi
Masonganya kufanyiwa ndumba.
Kuna madhila yaliwahi kumpata Jaji aliyekuwa
akisikiliza kesi ya ubakaji iliyokuwa ikimkabili
mjukuu wa Bi Masonganya aitwaye Ndoza, hiyo
nayo ikawa ni historia ya kushangaza na
kusikitisha! Ni kweli Ndoza alibaka haswa tena saa
saba mchana watu wakishuhudia dhahiri
akimngangania binti wa watu aliyekuwa akipita
na safari zake, akamvutia kwenye pagara lilikouwa
jirani na kumfanyia ushenzi. Sasa kesi ilipoonesha
dalili zote za kumuelemea Ndoza, ndipo Bi
Masonganya akaibuka na kuikingia kifua.
Akamfuata jaji, akamkanya kwa maneno makali ya
vitisho kuwa endapo ataendelea na mpango wake
wa kutaka kumfunga jela mjukuu wake basi
atakiona kilichomfanya kuku aanze kuota manyoa
mkiani Jaji akapuuza, pengine kwakuwa naye
alikuwa amejiganga.
Siku ya hukumu sasa Jaji akiwa anaingia
mahakamani baada ya umati kufurika ndipo ghafla
walipoibuka nyuki hata wasijulikane walipotokea,
ikawa ni patashika ya nguo kuchanika kila mmoja
akitafuta njia yake. Kama Nyuki nao huwa na
kichaa, basi hawa nao walihitaji chanjo. Walikua
wanauma ovyoovyo, na wakikuuma, hayo maumivu
yake ni kama umegongwa na koboko.
Matokeo ya hila za nyuki wale ni pamoja na
mafaili yote yaliyobeba kesi ya Ndoza kupotea japo
hilo halikuwa kubwa sana. Lililoshitua zaidi ni
kitendo cha wale nyuki kumfakamia Jaji licha ya
kelele za kutaka msaada alizokuwa akipiga bila
mafanikio mpaka walipomtoa roho.
Kifo cha Jaji kwa kuumwa na nyuki mahakamani
kikazagaa kama moto wa pumba, huku kila mmoja
akijifanya ni fanani wa mkasa ule.
Kesi ya ndoza ikatulia kama maji ya mtungi.
ITAENDELEA......