Sehemu ya 14*
Na alipomtazama bwana yule aliempiga risasi akaona bado anahangaika kujizuia ili damu zisimtoke,lakini alipotazama alipodondokea yule mtu aliepigwa na koplo Mina akamwona akiwa anajiandaa kunyanyuka ili aendeleleze mpambano.
Konstebo Tito akageuka alipo Koplo Mina akashangaa kumuona akiwa barabarani akikimbizana na pikipiki iliokuwa na watu wawili, akataka kumfuata lakini akaona inafaa awadhibiti kwanza hawa watu wawili waliochini.
Akaipachika bastola yake kiunoni kisha kwa hatua za haraka akamfikia Yule aliepigwa na koplo Mina,akamnyanyua kisha akamshindilia kichwa na kumpasua pua.
Alipoona bwana yule akiwa hoi akigugumia maumivu ya pua akataka kutoa pingu na hilo likawa kosa,akajikuta akitupwa chini kwa pigo safi alilopigwa nyuma ya mgongo.
Baada ya kuanguka Konstebo Tito akataka kunyanyuka lakini akajikuta akiwa chini tena na maumivu ubavuni ni baada ya mtu aliempiga kumwongeza teke lingine upande wa mbavu.
Konstebo Tito akaona akizubaa basi adui yake atafanikiwa kumzimisha kizembe hivyo alihitajika kufanya jitihada za haraka ili aweze kujiokoa.
Mbali ya maumivu aliyoyapata,lakini akaamua kufanya hila akiwa pale chini.
Aligeuka na kulala chali na hapo akashuhudia yule bwana aliempiga risasi ya bega akija kwa kasi kama nguruwe aliejeruhiwa, alipomfikia akaruka juu ili ammalize kabisa lakini hila yake iligunduliwa na konstebo makini kabisa.
Tito akajipindua kidogo na kulalia ubavu na hapo pigo la bwana Yule likakutana na ardhi tupu.
Ikawa zamu ya konstebo Tito kushambulia,na hapo kwa ufundi wa kishaulin akatumia mkono mmoja kusimama huku guu lake la kulia likimshindilia teke la mgongo bwana Yule aliekuwa anajaribu kujiinua kutoka chini baada ya hesabu za kumuua Tito kugonga mwamba.
Teke lile lilimrudisha chini bazazi yule huku,konsetebo Tito akiwa amesimama tayari na kujipanga ili kukabiliana na yule mwingine aliekuwa anajaribu kuishika bastola yake vyema kumlenga konstebo Tito.
Si Tito ama bwana mmoja aliekuwa chini akigalala aliejua kimetokea nini,isipokuwa walishuhudia tu yule bwana alieshika bastola akidondoka chini huku tundu la risasi likiwa upande wa moyo.
Kosntebo Tito akiwa bado anashangaa akajikuta akipitiwa na kitu kama kimbunga na kujikuta akidondoka chini ya tairi za gari na alipotizama aliemwangusha akagundua ni koplo Mina.
Baada ya kujirusha na kumpitia konstebo Tito,koplo Mina alijikuta hana bastola alioishika mkononi,hivyo kufanya shabaha yake aliokuwa ameikusudia kutokufanya kazi na aliposimama akamshuhudia Tito akiwa anamrushia bastola nae akaidaka kiweledi kabisa na alipokaa sawa kulenga kule shambulizi lilipotoka tayari watu wale walikuwa wamedandia pikipiki na kuondoka.
Haraka koplo Mina akamfikia mvamizi mmoja aliehisi bado yupo salama,ila tofauti na alivyotegemea alikuta nae risasi kadhaa zikiwa zimemkaa mwilini,lakini alikuwa bado anapumua kwa mbali mtu yule hivyo akamvua haraka kile kificha uso alichokuwa amekivaa na hapo akapigwa na butwaa.
Sajenti Zaka!! Alisema Mina kwa mshangao,maana hakutaka kuamini mkubwa wake kikazi anaweza kumsaliti ama kukisaliti kiapo na kuwasaidia wahalifu.
Koplo Mina akageuka ili aende kwa yule alitangulia kushambulia na hapo akakutana mshangao kutoka kwa Konstebo Tito nae alikuwa nashangaa kama yeye,haraka akaenda ilipo ile maiti nae hakusita kushangaa tena.
Inspekta zogo!! Mungu wangu ni nini hiki" alisema koplo Mina kwa wahka mkubwa huku akiwa amejishika kiuno
"Mafoo,wafoo....mmmmh... " ilisikika sauti ya maumivu kutoka kwa sajini zaga na haraka kama wakimbiao nyuki Wote wawili wakapiga hatua kumfikia na hapo koplo Mina akajua kuna kitu alitaka kusema hivyo akainama na kumwekea sikio mtu yule aliekuwa askari mwenzao na walimtaja kwa jina la sajini zaga.
"Mafoo,wafoo" koplo Mina aliambulia tu kusikia hayo maneno na hapo akajua askari yule alikuwa anawapa taarifa juu ya hao mafoo au wafoo.
Tofauti na alivyodhania koplo Mina ya kuwa mafoo ni watu wawili mapacha kama alivyoambiwa na Temba lakini hapa akapata kutambua wafoo na mafoo ni tofauti kabisa japo wapo pamoja na hivyo hii ilimpa taarifa ya kuwa wanapambana na zaidi ya watu wawili.
Wakiwa wanajiandaa kutoka eneo lile baada ya kuhakikisha sajini Zaga hawezi tena kusema wakajikuta wanakutana na mitutu ya bunduki ikiwa imekokiwa.
Walikuwa ni askari polisi waliowazingira na kuwaweka chini ya ulinzi,walifika saa ngapi,haieleweki.
Konstebo Tito na koplo Mina wakafungwa pingu na haraka gari la polisi likafika na wakapakiwa na muda wote huo hakuna aliewasemesha.
Gari lile la polisi kabla halijaondoka wakapata kusulhuhudia may mmoja aliekuwa kavaa kiraia akishuka kutoka mbele ya difenda ile ya kipolisi na kusogea hadi kule ilipo miili ya sajini zanga na inspekta zogo na haraka akaikoki bastola yake na kuwashindilia risasi askari wale wasio watiifu kisha akatema mate chini na kurudi hadi ilipo difenda na kabla hajapanda akasema
"mmekamatwa kwa kuhusika na vifo vya askari waadilifu" kisha akapanda ndani ya gari na ikaanza safari.
Koplo Mina akamgeukia konstebo Tito na hapo wakazungumza kwa ishara na wakaelewana ya kuwa hawapo katika mikono salama lakini hawakuwa na njia ya kufanya maana askari wanaowalinda wako makini kuwalinda.
*****
Walikuwa wamekwenda umbali wa kama kilomita sita hivi na hapo dereva wa difenda ile akaona kitu nyuma yao na alipojaribu kutazama vizuri akaona kuna gari ibakuja kwa kasi nyuma yao,lakini haikuwa gari peke yake kulikuwa na kitu mfano wa tufe kikiserereka kwenye lami.
Dereva akapiga ukunga kuwaarifu wenzie wapo matatani lakini walikuwa wamechelewa si yeye wala wenzie waliojua kifuatacho zaidi aliishudia gari yake ikipaa juu na kile kitu mfano wa tufe kikipasukia uvunguni mwa gari yao na kisha gari ikajipigiza chini kwa nguvu na kilichofuata hakujua tena.
Ile gari alioiona dereva wa difenda ile ikasimama nyuma ya difenda ile iliokuwa inafuka moshi mzito.
Kilianza kiatu kizito kukanyaga chini kisha yakafuatia mate yaliotemwa na mwenye kiatu kile na kikafuatia kichwa kilichokuwa kimenyolewa nywele zote na kisha ukafuatia mwili mzima na kusimama na hapo ikashuhudiwa miwani pana ilioficha macho ya mtu yule aliejazia kimazoezi.
Mate yalitemwa chini kwa kutangulia mbele na yeye akafuata na kuyapita mate yake na kisha akalifikia difenda lile lilokuwa limesimama kiupande baada ya tairi moja ya nyuma kupasuka.
Yule mtu akapanda kwenye difenda ile na kuipangua miili ya askari polisi waliokuwa hawana fahamu na kisha akamchukua koplo Mina na kushuka nae hadi kwenye gari yake.
Akataka kuondoka lakini akaona si vyema akashuka tena na kumchukua konstebo Tito aliekuwa hoi bila fahamu na kumweka kwenye gari yake kisha akatema tena mate chini na bila kusema neno akawasha gari na kutimka huku nyuma akiacha difenda ile ikishangaliwa na watu waliokuwa wameanza kujaa eneo lile.
"PAPASO nimekwisha papasa mh" akajisemea mtu yule na kutema tena mate na kuyaacha yasambaratike barabarani kwa upepo mkali uliotokana na kuendesha gari kwa kasi ya ajabu huku akiyapita magari kadhaa.
Asalaaam kudo.